Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 27.06.2020: Guendouzi, Hart, Forster, Pereira, Ronaldinho

Mkufunzi wa Arsenal amekataa kutoa hakikisho kwamba Matteo Guendouzi atasalia katika klabu hiyo msimu ujao kufuatia ripoti kwamba kiungo huyo wa kati wa Arsenal na raia wa Ufaransa anataka kuondoka. (Guardian)
Manchester United wameonesha hamu yao ya kutaka kumsajili Guendouzi, huku Barcelona, Paris St-Germain, Inter Milan na Atletico pia wakivutiwa na mchezaji huyo mwenye umri mdogo. (L'Equipe, via Mail)
Arsenal inamnyatia kiungo wa kati wa Portugal Danilo Pereira, huku Porto ikiwa tayari kukubali Yuro milioni 20 (£18.2m) kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 -year-old, mbali na kwamba bado klabu hiyo ya London inamtaka kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ghana Thomas Partey, 27. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Celtic inafikiria kumsajili kipa Joe Hart, 33, baada ya kuachiliwa na Burnley, iwapo mabingwa hao wa Uskochi watashindwa kupata saini ya kipa mwengine wa England Fraser Forster,32, kwa mkopo mwengine kutoka Southampton. (Telegraph)
Beki wa Senegal Kalidou Koulibaly, 29, anataka kuondoka Napoli mwisho wa msimu huu ili kuichezea klabu ya Pep Guardiola Manchester City. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Inter Milan inakaribia kumsaini beki wa kushoto wa Real Madrid na Morocco Achraf Hakimi, 21, ambaye amekuwa kwa mkopo katika klabu ya Borussia Dortmund, kwa takriban dau la €40m (£35.8m) na marupurupu. (Guardian)
Mchezaji anayelengwa na Arsenal Layvin Kurzawa, 27, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya wa miaka minne na klabu ya Paris St-Germain wakati kandarasi ya beki huyo wa kushoto wa Ufaransa itakapokamilika 30 June. (RMC Sport, via Sun)
Kiungo wa kati wa Birmingham Jude Bellingham, ambaye amehusishwa na Manchester United na Borussia Dortmund, anaweza kutia saini kama mtaalamu wakati atakapofikisha umri wa miaka 17 siku ya Jumatatu lakini bado hajamwambia mkufunzi wa Blues Pep Clotete kwamba tayari ameamua kuhusu hatma yake. (Mirror)

Mchezaji ambaye yupo Arsenal kwa mkopo Dani Ceballos amesema kwamba huenda akajiunga na klabu yake ya zamani Real Betis baada ya kiungo huyo wa Uhispania, 23, kusema kwamba atarudi katika klabu yake ya Real Madrid mwisho wa msimu huu. (Marca)
Mkufunzi wa klabu ya Gimnasia y Esgrima La Plata Diego Maradona anatumai mchezaji wa Brazil Ronaldinho, 40, atarudi katika ulingo wa soka ili kuichezea klabu hiyo ya Argentina. (Marca)
Mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 19, hafikirii kuhusu kuondoka klabu ya Borrussia Dortmund , licha ya kuhusishwa na Real Madrid na Manchester United . (Westdeutsche Allgemeine Zeitung - in German)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham imetoa ofa ya kandarasi mpya kwa winga Maurizio Pochettino, 19, ambaye ni mwanawe mkufunzi wa Spurs Mauricio. (Standard)
Ushindi wa Liverpool wa taji la ligi ya Premia utaipatia Southampton £2.5m, kwa kuwa wachezaji wanne wana sheria ya kifungu cha marupurupu ya ziada baada ya klabu hiyo kuwauzia mabingwa hao wapya wachezaji wanne. (Telegraph)
Liverpool huenda ikalipa zaidi ya £10m kama marupurupu ya ziada, huku Arsenal, Hull City na Charlton pia zikitarajiwa kufaidika. (Mail)
Mkufunzi wa Juventus Maurizio Sarri hajui iwapo kiungo wa kati wa Bosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, 30, atasalia katika klabu hiyo licha ya kuivutia Barcelona. (Sky Sports Italia, via Goal)
Mshambuliaji wa Argentina Carlos Tevez, 36, hajakata tamaa ya kurudi katika klabu ya West Ham wakati kandarasi yake itakapokamilika na klabu ya Boca Juniors. (Radio La Red - in)































