Kombe la FA: Mchuano kati ya Sheffield United na Arsenal

Nicolas Pepe
Maelezo ya picha, Pepe akionesha makala yake na kuipatia Arsenal ushindi kipindi cha kwanza
Iliyochapishwa

Katika mchuano wa leo, Nicolas Pepe ameanza na kurusha mpira uliokwenda kwa Kieran Tierney beki wa kushoto na huyo huyo ndiye aliyeiweka Arsenal kifua mbele katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Wachezaji wawili Jack Robinson wa Sheffield United na Nicolas Pepe wa Arsenal - waligongana katika eneo la penalti la Blades. Pepe akataka kupewa penalti lakini haikuwezekana na badala yake free-kick ikamwendea mrama.

Kisha kukatoke tena mgongana, safari hii alikuwa ni Kieran Tierney na George Baldock lakini wote wakaonekana kuwa sawa.

Pepe alifanikiwa kuiweka Arsenal kifuambele baada ya Alexandre Lacazette kusemekana kucheza visivyo kupitia VAR.

Baada ya dakika 45 za kwanza, Sheffield United ilikuwa na dakika 45 zingine za kuendeleza matumaini yao katika kombe la FA.

Huku Gunners wakiongoza baada ya penalti safi kutoka kwa Nicolas Pepe pale Chris Basham alipotambuliwa na VAR kwamba amemchezea Alexandre Lacazette vibaya.

McGoldrick scores late equaliser for Sheff Utd
Maelezo ya picha, McGoldrick aifungia Sheff Utd

McGoldrick ameifungia Sheffield United bao na kuanza kuibuka kwa maswali ikiwa hilo ndo lingewapeleka Arsenal katika muda wa ziada.

Kufikia wakati huo, Sheffield United pengine ilifikiri inaweza kushinda kirahisi tu, Billy Sharp, akapiga mpira kutoka mbali lakini Martinez akapangua mpango huo.

Dadika chache tu baada ya David McGoldrick kusawazisha, bila shaka mchezo ulikuwa unaingia katika muda wa ziada lakini bao la Dani Ceballos dakika za majeruhi likaikatia Gunners tiketi hadi Wembley kwa nusu fainali.

Arsenal inasonga mbele Sheffield United nje
Maelezo ya picha, Ceballos aipatika Arsenal fursa ya kusonga mbele katika kombe la FA

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta, akizungumza na BBC Spoti ameweka wazi kwamba hii ni fursa nzuri kwa timu hiyo kushinda taji:

"Nimefurahishwa sana na mchezo. Hili ni eneo gumu kuja na kupata ushindi. Tumerejea Wembley. Nimefurahishwa sana na ari ya wachezaji na mchezo wao.

"Ni fursa nzuri ya kujaribu na kushinda taji na kucheza Ulaya. Tumecheza michuano minne ugenini tangu kuanza tena kwa mchezo. Shukrani kwa Ligi ya Primia kwa kalenda yetu ya kucheza kila baada ya siku tatu. Lakini bado tuna mchuano Jumatano."

Kwa upande wake kocha wa Sheffield United Chris Wilder, akizungumza na BBC Spoti: "Mchezo wa leo ulikuwa mzuri kuliko miwili iliopita. Kama wataalamu hatupendi kushindwa na tumekwenda mashindanoni. Tumekatishwa tamaa na ushindi wao. Nilidhani kwamba sisi ndio tunaoendesha mpira. Kuna mambo kadhaa ambayo hayakutuendea vizuri. Bao ambalo halikuruhusiwa na kisha penalti waliopata. Kasi ya (Chris Basham). Tulikosa kujiamini kwa namna hiyo, jambo ambalo linatokea unapopoteza michuano miwili 3-0. Tuna wachezaji wazuri ambao pengine wanachohitaji ni kujiamini zaidi.

"Ni tabia yetu kuchukua ushindi na tulihisi kwamba wanaenda kukosa matumaini. Kasi yao uwanjani ni ya kupigiwa mfano lakini pia nasi tulionesha makali yetu. Wakati mwengine inabidi urudi kwenye yale ya msingi na kidogo hii leo tulikuwa tunacheza moja kwa moja lakini mbinu hii ilitufanyia kazi. Tunahitajika kukaza kamba kidogo ili tuweze kubadilisha hali hasa mambo yanapokuwa yamepamba moto na kubadilisha kushindwa kwa bao moja kuwa 1-1 na pengine kusonga mbele hadi kuwa 2-1. Lakini leo hii tuliwaruhusu watushambulie, moja ya uwezo wao.

Arsenal inasonga mbele Sheffield United nje.

Historia

Sheffield United inapokabiliana na Arsenal katika robo fainali ya kombe la FA, BBC inaangazia timu hizo mbili.

Mwaka 1999, ilikuwa ni mara ya tano ya timu hizo kutoka sare. Mchezaji mmoja alipata jeraha na Sheffield United ikapiga mpira nje. Wakati huo, Ray Parlour alipiga mpira kuurejesha lakini mambo yakabadilika tofauti na walivyokuwa wanatarajia.

Nwankwo Kanu aliukimbilia akampita Marc Overmars na mpira na huo ukaingia nyavuni huku wachezaji wa Blades wakisusia na kocha wao Steve Bruce akitishia kuondoa wachezaji wake uwanjani.

Kocha akiwa ni Arsene Wenger Arsenali iliibuka na ushindia lakini kocha huyo akaahidi kurejelewa kwa mchezo huo na kama ujuavyo liandikwalo halifutiki, na Arsenal ikashinda tena 2-1 kupitia tena mchezaji wao Overmars.