Popo watoto wasikika wakiongea kama binadamu

Chanzo cha picha, Michael Stifter
Popo hao ambao hutoa sauti ambayo ikiwa inajirudia inaunganisha silabi za maneno ambapo zinaenda sawa na sauti ya mtoto mdogo ambaye anajifunza kuongea.
"Wanaongea hivi hasa kwenye kipindi jua linachomoza na linapozama,inaonesha ni kama wanajifunza kitu kwenye sauti wanazozitoa," Amesema muongozaji wa Utafiti Dkt. Ahana Fernandez.
Dkt Fernandez, ambaye anafanya kazi katika makumbusho inayojihusisha na historia ya mambo ya asili huko Berlin, pia amesomea uchunguzi wa sauti za wanyama hasa kwa Popo mwenye mabawa, Saccopteryx bilineata.
"Popo hawa wanaimba kama wanavyofanya ndege wengine,lakini namna wanatoa sauti zao kuwasiliana ni jambo linalonishangaza sana, ni kama muunganiko wa aina za silabi." anasema.
Akishirkiana na wataalamu wenzake wameweza kuandika chapisho la kisayansi la kiuchunguzi ,ambapo humo wamechambua kwa undani kinachosababisha sauti hizo za popo na chanzo chake.
Mambo waliyoangazia ni yafuatayo:
- Kurudia rudia kwa silabi muhimu katika mazungumzo
- Mikogo na marudio ya sauti ya "da-da-da" ambayo inafanana na sauti anayoitengeneza mtoto mdogo.
- Wanasayansi wameanza kufanya uchunguzi wa kusikiliza kwa makini sauti za popo wadogo wanaotoka Costa Rica baada ya kugundua kuwa wanauwezo wa kuongea kama binadamu.

Chanzo cha picha, Michael Stifter
Sauti ya binadamu ni rahisi kuigundua kwa kutumia vifaa mbalimbali.
Sauti ya mtoto mchanga anayoitoa inamfanya ajifunze kupangilia maneno kirahisi,ndio utafiti unasema kuwa hata kwa popo hutokea sawia.
"Tunajua aina zote za silabi zinazozalishwa na popo wakubwa,"amesema Dkt. Fernandez.
"Pamoja na nyingine zinazotolewa na mbwa mdogo-kwahiyo tunaweza kuthibitisha."
Popo mkubwa wa mabawa ni aina pekee ya popo inajulikana kufanya hivi sana.
"Aina takribani 1,400 za wanyama Duniani zinafanyiwa uchunguzi kuwa wanaweza kutoa sauti amesema."Dkt Fernandez.
Utafiti huu umebainisha muundo ambao unaweza kuwa muhimu kwa mamalia wengi ambao wanapaswa kujifunza kuwasiliana kwa sauti, pia anasema kuna mengi ambayo yamebaki kuelewa juu ya spishi hii maalum ya popo wanaongea .
"Watoto husikilizana sana wanapokuwa wakiongea," Dkt Fernandez .
"Mmoja huanza, anaongea kwa kuimba ndani ya dakika 15 au zaidi, na ninaweza kuona wazi masikio ya watoto wengine wakisikiliza na kufuatisha.































