Tetesi za soka Ulaya Jumapili 20.02.2022: Sterling, Azpilicueta, Dalot, Carvalho, Ronaldo, Bielsa, Morata

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wako tayari kufanya mazungumzo ya kandarasi na mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Raheem Sterling mwishoni mwa msimu huu - lakini wanaweza kuamua kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ikiwa hatakubali mkataba mpya.(Times via City Xtra)
Chelsea wamemwambia Cesar Azpilicueta kwamba watamsubiri mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kuamua hatma yake iko wapi. Beki huyo wa Uhispania amepewa mkataba wa miaka miwili na chaguo la kuongeza msimu mwingine kutoka Barcelona. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Reuters
Beki wa Ureno Diogo Dalot, 22, yuko tayari kurefusha muda wake wa kusalia Manchester United, na kuacha mustakabali wa beki wa kulia wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka, 24, katika shaka kubwa. (Star)
Hata hivyo, Fiorentina wanadaiwa kumtaka Dalot lakini watalazimika kumshawishi beki huyo wa pembeni kupunguza mshahara wake ili kufanikisha uhamisho huo. (La Nazione via Sportwitness)
Manchester United wanaweza kuteka nyara jaribio la Liverpool ya kumsajili winga wa zamani wa England wa Chini ya umri wa miaka 18 Fabio Carvalho, 19, kutoka Fulham katika msimu wa joto wakati mkataba wake utamalizika. (Star)
Manchester United pia haitamzuia fowadi wa Ureno Cristiano Ronaldo ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 atataka kuondoka mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Meneja wa Leeds United Marcelo Bielsa, 66, anatazamiwa kuondoka katika klabu hiyo msimu wa joto baada ya kusema kuwa haiwezekani kushindana katika Ligi ya Premia bila kujitolea kabisa.(Mirror)
Arsenal wanavutiwa na mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 29, huku Atletico Madrid wakiwa tayari kumuuza. The Gunners wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka kwa Juventus, ambapo Morata yuko kwa mkopo kutoka upande wa La Liga. (Tuttomercato - in Italian)
The Gunners pia wanafanya ukaguzi wa muda kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Napoli na Uhispania Fabian Ruiz, 25. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Italia Jorginho, 30, anasema alikuwa karibu kujiunga na Manchester City kabla ya kuhama kutoka Napoli hadi Stamford Bridge, na bado ana matarajio ya kucheza chini ya Pep Guardiola. (Express)
Kiungo wa kati wa Everton na Ivory Coast Jean-Philippe Gbamin, 26, anawindwa na CSKA Moscow na anaweza kuondoka kwa mkataba wa mkopo kwani timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Urusi bado zinaweza kufanya uhamisho hadi Februari 22. (Liverpool Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Baba ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, nyota wa zamani wa Leeds na Manchester City Alf-Inge Haaland, anatekeleza jukumu kubwa katika udalali wa hatua ijayo ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mirror)
Chelsea wameelekeza macho yao kwa mlinzi wa Real Madrid na Brazil Eder Militao na wameomba kukutana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ili kujadili uwezekano wa kuhamia Stamford Bridge.(Marca - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Tottenham Rodrigo Bentancur, 24, anasema wachezaji wenzake wa Uruguay Luis Suarez na Edinson Cavani walimsaidia kutimiza "ndoto" yake ya kuhamia Ligi ya Premia. (Sky Sports)
































