'Watu hawaamini kama nina uwezo wa kutengeneza gari'-Masoud Kipanya
Iliyochapishwa
Mchora katuni maarufu nchini Tanzania Masoud Kipanya amezindua gari lake alilolitengeneza mwenyewe kupitia kampuni yake iliyopo nchini Tanzania.
Licha ya watu kutomuamini kama yeye ndiye aliyelitengeneza anasema ametumia gharama kubwa kulitengeneza lakini anatamani kuliuza kwa gharama ndogo ili liweze kuwa msaada kwa vijana wabeba mizigo na wasambazaji wa bidhaa
Gari hili linatumia umeme na lina uwezo wa kubeba Kilo 500, Je ungependa kujua gharama yake?
Mwandishi wa BBC frank Mavura ameandaa taarifa hii.
