Mahakama Kuu Tanzania yatupilia mbali kesi ya Mdee na wenzake

Mdee
Iliyochapishwa

Mahakama Kuu nchini Tanzania imetupilia mbali kesi ya msingi iliyokuwa imefunguliwa na wabunge 19 wa viti maalumu wa CHADEMA ambao walivuliwa uanachama wa chama hicho.

Chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, kupitia kamati kuu yake kiliwavua uanachama wanachama wake hao 19 walioapishwa kuwa Wabunge wa viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya uchaguzi wa mwaka 2020. 

Baada ya kuvuliwa ubunge walikata rufaa Baraza kuu la chama hicho ambacho ni ngazi ya juu ya maamuzi ya ndani ya chama.

Hata hivyo maamuzi ya mwezi Mei, 2022 Baraza Kuu la Chama likaunga mkono maamuzi ya kamati kuu ya chama hicho ya kuwafukuza uanachama wabunge hao 19, miongoni mwao ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake BAWACHA Halima Mdee. 

Baadae walienda Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Baraza Kuu, na kuomba zuio la muda la ubunge iliyotolewa maamuzi yake leo.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, mbunge anapaswa kutokana na chama cha siasa, hivyo wabunge hao huenda wakapoteza ubunge wao, iwapo Spika wa bunge atapata taarifa rasmi na kutekeleza maamuzi ya mahakahama.

Mzozo wa nafasi za kibunge kwa wabunge hao zilianza mara tu baada ya uchaguzi wa mkuu wa mwaka 2020, ambapo Chadema ilipinga matokeo na ‘kususa’ kupeleka majina ya wabunge wa viti maalumu kwa kile ilichoeleza kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi, uliompa ushindi hayati John Magufuli.

Hata hivyo, wabunge hao, walitangazwa na aliyekuwa spika wa bunge, Job Ndugai kama wabunge wa viti maalumu wa Chadema, lakini chadema ilikana kuwatambua, ikisema haikuwasilisha jina lolote kwa nafasi za wabunge hao.

Baada ya uamuzi wa leo, Chadema kupitia katibu wake mkuu, John Mnyima imesema 'haki imeshinda dhulma na usaliti' na sasa wanasubiri bunge lifanye uamuzi wa kuwaondoa bungeni wabunge hao.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala, kwa upande wake anasema, kwa sasa hakuna kinachoweza kuzuia sheria kufuatwa katika kuwaondoa wabunge hao 19.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2

Tangu kuapishwa kwao Novemba 24, mwaka 2020 wabunge hao waliendelea kuhudhuria bungeni, huku kukiibua mjadala juu ya uwepo wao bungeni na kulipwa na fedha za umma, wakati chama kiliwafukuza.