Nguvu ya mikono ya kushilia kitu inasema nini kuhusu afya yako uzeeni?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Rafael Abuchaibe
- Nafasi, BBC World
- Iliyochapishwa
Nguvu za mikono yetu inaweza kuashiria kile kinachotokea ndani ya mwili wetu. Tafiti kadhaa za kisayansi zimehusisha upotezaji wa nguvu ya kushikilia - uwezo wa kushikilia kitu kwa mkono wako mmoja, kama vile mpira wa mafadhaiko, kwa mfano - na kuongeza kasi ya kuzeeka kwa mwili.
Utafiti wa 2020 uliochapishwa katika Jarida la European Journal of Clinical Nutrition ulichambua uwezo wa juu wa kukamata wa wagonjwa zaidi ya miaka 75 na kupata uhusiano wa moja kwa moja kati ya udhaifu wa nguvu hizo na uwepo wa sarcopenia, ambayo ni aina ya atrophy ya misuli ambayo hutokea umri.
Uchunguzi mwingine unaonyesha kuwaa kupoteza nguvu za kushikilia sio tu kuakisi matatizo yanayowezekana katika uzee, lakini katika umri wowote na kwamba watu ambao hawafikii mipaka ya chini ya nguvu mikononi mwao wanaweza kukabiliwa na matatizo ya kiafya kila aina, ikiwa ni pamoja na moyo na kupumua.
“Tuna tafiti kadhaa ambazo zinaashiria nguvu ya mshiko wa mkono huchukuliwa kama dalil za magonjwa sugu na hata vifo,” Profesa Mark Peterson, kutoka mpango wa tiba ya kimwili na urekebishaji wa Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani.
"Ni kiashiria cha jumla cha jinsi mwili ulivyo na nguvu : ikiwa mtu ana nguvu mwilini kuna uwezekano mkubwa ana nguvu katika miguu, mikono na hata sehemu ya tumbo," anasema mtaalam.
Nguvu ya kishikilia
Ili kujua uwezo wa juu zaidi wa mtu ya kushikilia kitu kwa nguvu , madaktari hutumia dynamometer, chombo ambacho mgonjwa lazima afinye kwa nguvu iwezekanavyo katika matukio matatu tofauti. Kisha matokeo matatu yanakadiriwa.
Kulingana na utafiti wa 2022 wa watafiti katika Chuo Kikuu cha Vienna huko Austria, watu ambao walikuwa na nguvu ya chini ya kushikilia kuliko wastani kwa kikundi chao cha umri, jinsia na urefu wanaweza kuwa na hatari kubwa ya vifo.
"Matokeo yanaonyesha kwamba nguvu ya juu ya kukamata chini ya wastani wa idadi ya watu kulinganishwa ni dalili ya hali za afya zinazosababisha kifo cha mapema," chasema Taasisi ya Kimataifa ya Uchambuzi wa Mifumo Inayotumika, kituo kilichoko Austria, ikirejelea matokeo ya kusoma.
Moja ya sababu zinazohusiana na kupoteza nguvu katika mikono ni sarcopenia, syndrome ambayo ina sifa ya upotevu unaoendelea na wa jumla wa misuli ya misuli na kazi ya misuli inayohusiana na mchakato wa kuzeeka.
Ingawa ni jambo la kawaida kupoteza misuli kadri umri unavyoongezeka, tafiti kadhaa, ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Southampton, nchini Uingereza, zimehusisha mtindo wa maisha kama vile maisha ya kukaa chini na uzani mkubwa kama viashiria vya kuishiwa na nguvu ya kushilikilia kitu uzeeni.
“Ndiyo maana uwezo wa kushikilia kitu ni chombo kizuri sana,” Profesa Peterson aeleza, “kwa sababu tunapompata mtu ambaye uwezo wa mikono yake kushikilia kitu ni mdogo, moja kwa moja tunajua u mwili na tunaweza kuingilia kati kwa kubadili tabia.”

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanasayansi wamefanikiwa kumegundua uhusiano uliopo kati ya nguvu ya mikono ya wazee na nguvu ya miguu yao na misuli ya tumbo.
"Unapozeeka, misuli ya sehemu ya chini ya mwili inakuwa na nguvu zaidi," Dk. Christopher Hurst, mtafiti mshiriki wa masuala ya mtindo wa maisha na ustawi katika Chuo Kikuu cha Newcastle nchini Uingereza, aliambia BBC Mundo.
"Ni misuli unayotumia kuinuka kutoka kwenye kiti, kutembea, na kupanda na kushuka ngazi."
Na kutokana na uhusiano huu wa moja kwa moja kati ya mikono na misuli mingine ya mwili, ni rahisi kwa wataalamu kutambua hatari zinazohusiana na kupoteza nguvu za misuli.
Watafiti katika Taasisi ya Geriatrics katika Chuo Kikuu cha Monash mjini Melbourne, Australia, waligundua katika utafiti wa muda mrefu kwamba nguvu dhaifu ya kushikilia kitu ilikuwa kiashiria kikubwa cha kuanguka kwa wanaume wazee na wanawake wanene.































