Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 13.07.2023

Chanzo cha picha, Getty Images
Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson anafikiria kuondoka katika klabu hiyo na kwenda kwenye klabu ya Al-Ettifaq inayofundishwa na Steven Gerrard ya nchini Saudi Arabia. Bado hawajawasilisha ofa rasmi kwa kiungo huyo wa kati wa England, 33, lakini wanataka kumsajili. (Telegraph)
Paris St-Germain itafanya kila linalowezekana kumpata mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29, kwenye klabu hiyo - ingawa chaguo lake la kwanza linabaki kuwa Bayern Munich. (RMC Sport)
Barcelona wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 28, lakini mpango wao mbadala ni kumnasa mchezaji wa Tottenham na Argentina Giovani lo Celso, 27. (Mundo Deportivo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Nottingham Forest wameendeleza nia yao ya muda mrefu ya kumnunua kiungo wa kati wa PSV Eindhoven na Ivory Coast Ibrahim Sangare, 25, kwa kuweka ofa mezani. (Athletic)
Liverpool wako tayari kutoa ofa kwa beki wa kati wa Chelsea Muingereza Levi Colwill, 20. (90min).
Manchester United, Newcastle United na Aston Villa zote zinawania saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 23. (ABC, via Metro).
West Ham iko njia panda kwa kuchelewa kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 24, kwa pauni milioni 105, jambo ambalo linasababishwa na kucheleweshwa kwa kutayarishwa kwa nyaraka na mawakili wa Arsenal. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton wanavutiwa na mshambuliaji Mfaransa Moussa Dembele, 27, na mshambuliaji wa Leicester Muingereza Jamie Vardy, 36. (FootballTransfers)
Newcastle bado wako kwenye mazungumzo na Leicester kuhusu winga wao Muingereza Harvey Barnes, 25, huku The Magpies wakifikiria kutoa ofa ya awali ya takriban £30m. (Mail)
Kiungo wa kati wa Nice na Wales Aaron Ramsey, 32, ana ofa ya pesa nyingi mezani kuhamia Saudi Arabia. (Sun)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 27, yuko kwenye orodha ndefu ya wanaosakwa na Atletico Madrid. (Marca)
Chelsea wako tayari kumuuza beki wa kati wa Uingereza Trevoh Chalobah, 24, msimu huu wa joto iwapo ofa sahihi itapatikana. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wamekataa ofa za pauni milioni 30 kumuuza kiungo wao wa kati wa England chini ya miaka 21 James McAtee, 20. (Sun)
Bristol City wamekataa ofa ya pauni milioni 15 kutoka kwa Bournemouth kwa ajili ya kiungo wa kati wa Uingereza Alex Scott, 19. (Bristol Live)
Beki wa Manchester United Muingereza Will Fish, 20, amekubali kucheza tena na Hibernian kwa mkopo wa msimu mmoja. (Manchester Evening News)
Wolves wako tayari kutoa ofa kwa Mhispania Jonny Castro Otto, 29, huku kukiwa na mazungumzo ya kutaka kumsajili tena beki wa pembeni wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 31. (Express & Star)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 24, atavaa jezi namba 11 atakapokamilisha uhamisho wa kwenda AC Milan. (Goal)

































