Porton Down: Je, maabara hii inaweza kusaidia kuzuia janga lijalo?

Maabara
Iliyochapishwa

Moja ya vituo vya siri vya Uingereza vya utafiti wa kisayansi - Porton Down - kinakusudia kuzuia ama kukomesha janga linalofuata.

Nimepitia ulinzi mkali sana katika kituo hiki kilichoko mbali ili kuwafikia wanasayansi wake anbao ni nadra kuwafikia.

Wanapatikana katika Kituo kipya cha Kukuza na Kutathmini Chanjo.

Jukumu lao linajengwa na muitikio wa janga la Covid-19, na kinalenga kuokoa maisha na kupunguza suala la watu kujifungia ama kuzuiwa kutoka nje (lockdown) wakati wimbi jipya litakapoibuka.

"Covid, bila shaka, si ya mara moja," anasema Prof Dame Jenny Harries, mtendaji mkuu wa Shirika la Usalama la Afya la Uingereza (UKHSA), ambalo linaendesha maabara hizi.

"Tunasema [Covid] lilikuwa tukio kubwa zaidi la afya ya umma kwa karne moja, lakini sidhani kama yeyote kati yetu anadhani ita chukua karne moja nyingine kabla ya ugonjwa huo kuibuka tena," anaongeza.

Mchanganyiko wa mabadiliko ya hali ya hewa, ukuaji wa miji na watu wanaoishi karibu na wanyama - chanzo cha magonjwa mengi mapya ambayo hutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu - na hii inamaanisha tunakabiliwa na "wimbi la hatari linaloongezeka", anasema.

 Dame Jenny Harries ni wazi Covid haikuwa "tukio la mara moja" la afya ya umma

Porton Down - iliyoko katika maeneo tulivu ya mashambani ya Wiltshire, karibu na Salisbury - ni mojawapo ya maeneo machache duniani yaliyo na vifaa vya kutafiti baadhi ya virusi na bakteria wabaya zaidi. Kuna majokofu hapa yamehifadhi virusi vya Ebola.

Majengo ya jirani ni pamoja na Maabara ya Sayansi na Teknolojia ya Ulinzi (sehemu ya Wizara ya Ulinzi), ambapo ilithibitishwa kuwa na sumu hatari ya Novichok inayoathiri nerve.

Maabara za chanjo - zilizoko katika majengo ya kijani kibichi - zilijengwa haraka kama njia ya haraka ya dharura ya kukabiliana Covid.

Lakini, kwa kuwa mahitaji makubwa ya janga hilo yamepungua, mwelekeo umebadilika.

Kituo hiki kipya cha utafiti wa chanjo kinazingatia aina tatu za tishio:

  • Maambukizo yanayojulikana ambayo yanazidi kuwa magumu kukabiliana nayo
  • Vitisho vinavyoweza kusababisha tatizo, ikiwa ni pamoja na mafua ya ndege na aina mpya za Covid
  • Na "Ugonjwa X" - kitu kisichotarajiwa, kama Covid, ambao unaivamia ulimwengu bila kujiandaa na kwa mshangao
n

Lengo ni kufanya kazi na tasnia ya dawa, wanasayansi na madaktari kusaidia hatua zote za utengenezaji wa chanjo.

Wanasayansi wa Porton Down wanafanyia kazi chanjo ya kwanza dhidi ya homa inayofahamika kama Crimean-Congo Haemorrhagic Fever, ambayo huenezwa na kupe na kuua karibu theluthi moja ya wale walioambukizwa.

Ugonjwa huo unapatikana Afrika, Balkan, Mashariki ya Kati na Asia - na unaweza kuenea zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika mwisho mwingine wa mchakato, ufanisi wa chanjo hutathminiwa. Ilikuwa ni wanasayansi hapa ambao waliona kwamba wimbi la Omicron linaweza kukwepa baadhi ya ulinzi unaotolewa na chanjo za Covid.

Na bado wanafuatilia wimbi jipya la Covid kwa kuzikuza kwenye maabara, kuendelea na utafiti kwenye maabara kupitia kingamwili zilizochukuliwa kutoka kwa sampuli za damu na kuona kama wimbi jipya bado linaweza kuambukiza.

th

Tofauti ni kwamba, kabla ya janga hilo timu za hapa ziliweza kujaribu sampuli 100 tu kwa wiki - sasa kwa vifaa bora walivyo navyo wanaweza kufanya majaribio zaidi ya 3,000.

Chanjo za haraka zaidi

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili WhatsApp bofya kutufuatilia
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Jukumu hapa wameliweka kwenye mipango au kwenye "Misheni ya Siku 100" - maono yenye matarajio makubwa ya kutengeneza chanjo dhidi ya tishio jipya la virusi katika siku 100.

Kihistoria, imechukua muongo mmoja kubuni na kujaribu chanjo mpya. Hali ya kipekee ya janga hili ilimaanisha kuwa chanjo ya kwanza ya Covid ilitolewa ndani ya mwaka mmoja, na kutolewa kwa chanjo hiyo iliyoanza kutumika Disemba 2020.

Makadirio yanaonyesha kuwa chanjo za Covid ziliokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 14 katika miezi 12 tu ya kwanza zilipotumiwa.

"Fikiria kama chanjo hizo zingepatikana mapema," Prof Isabel Oliver, afisa mkuu wa kisayansi wa UKHSA alisema.

"Zilipatikana kwa haraka zaidi kuliko hapo awali katika historia, [lakini] tungeweza kuokoa maisha ya watu wengi zaidi na tungeweza kurudi kwenye hali ya kawaida haraka zaidi."

Matumaini hapa ni funzo kuhusu janga la Covid ikimaanisha kuwa tumejiandaa vyema kwa janga lijalo.

Prof Harries anasema siku za nyuma tumekuwa tukishughulika na matukio, lakini katika siku zijazo tunahitaji kuwa mbele na "kujaribu kuzuia au kukomesha" janga lolote kabla hata halijaanza.

Na kama ugonjwa mpya utatokea, anaongeza, tunahitaji "kuuzuia katika njia zake" katika hatua yake ya awali.