Tetesi za soka Ulaya Jumapili 14.08.2022

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, wanaweza pia kuwa njiani kuelekea Stamford Bridge, huku Chelsea wakiongoza mbio za kuwasaka wachezaji wa Barcelona. (Express Online)
Lakini Barcelona wako tayari kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu kumnunua Aubameyang. (Metro)
Hata hivyo, De Jong amewaambia wachezaji wenzake wa Barcelona kwamba sasa kuna uwezekano wa kujiunga na Manchester United badala yake (Metro)
Chelsea wamekubali makubaliano ya kibinafsi na beki wa Ufaransa Wesley Fofana, 21, lakini ofa mbili zimekataliwa na Leicester City, ambao wanataka zaidi ya £80m. (Mail Online)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wamefanya mazungumzo na Atletico Madrid kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Uhispania mwenye umri wa miaka 29 Alvaro Morata kwa pauni milioni 30. (The Athletic, via Mail Online)
Na Manchester United wameisisitizia Paris St-Germain kwamba mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 24, hauzwi. (Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, BBC Sport
Hata hivyo, Paris St-Germain wanataka kumpa mkataba wa muda mrefu Marcus Rashford wa Manchester United ili kushirikiana na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23. (Sunday Times - subscription required)
Kiungo wa kati wa Tottenham Muargentina Giovani Lo Celso, 26, yuko Uhispania kukamilisha uhamisho wa mkopo wa msimu mzima kwenda Villarreal. (Fabrizio Romano)
Juventus wako kwenye mazungumzo ya kandarasi na mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 28, ambaye atakubali kusitisha mkataba wake na Barcelona mara tu mkataba utakapokamilika. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa kushoto wa Anderlecht, Sergio Gomez tayari amejiunga na Manchester City kabla ya kupendekezwa kwa mkataba wa pauni milioni 11 kwa ajili ya beki huyo wa Uhispania mwenye chini ya umri wa miaka 21. (Fabrizio Romano)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola huenda akamnyatia beki wa kushoto wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 25, ili kuimarisha zaidi safu yake ya ulinzi. (Mail on Sunday)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Ufaransa Tanguy Ndombele, 25, amekubali kuhamia Napoli kwa mkopo wa msimu mzima. (Fabrizio Romano, via Sun Online)
Udinese wamemuacha beki wa Itali Destiny Udogie, 19, nje ya kikosi chao akijiandaa kufanyiwa vipimo vya afya Tottenham siku ya Jumanne. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle United wako kwenye mazungumzo na Benfica ili kufikia makubaliano juu ya mshambuliaji wa Ureno mwenye thamani ya pauni milioni 35 Goncalo Ramos, 21. (Sunday Express)
Nottingham Forest imekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Brighton Mfaransa Neal Maupay, 25, kwa £15m.. (The Athletic - subscription required)































