Tetesi kubwa tano za soka Ulaya jioni hii

ggg
Iliyochapishwa

Leeds Utd imekuwa kipaumbele cha uhamisho kwa Juan Mata huku nyota wa zamani wa Man Utd akikataa ofa nyinginezo muhimu. 

Mata alicheza mechi 285 katika kipindi cha miaka minane na nusu akiwa Manchester United, akifunga mabao 51 na kuchangia 47. Kiungo huyo mshambuliaji sasa ni mchezaji huru kufuatia kumalizika kwa mkataba wake Man Utd mwanzoni mwa majira ya kiangazi. 

Mnamo Julai, kampuni ya Uhispania AS ilifichua Leeds kuwa katika mazungumzo na Mata mwenye miaka 34. 

ggg

Kiungo wa Manchester City Bernardo Silva anayewaniwa kwa ukaribu na vigogo wa Uhispania Barcelona amesema anasubiria kuona mustakabali wake katika soka ndani ya siku chache zijazo.

Amesema “Nimekuwa wazi na Man City na wanajua ninachotaka. Nikibaki, nina furaha sana na nitaheshimu klabu hii kila wakati na kujitoa kwa kadri niwezavyo. Ikiwa sivyo, ni mpira wa miguu na tutaona kitakachotokea. Nitakuwa mwenye heshima daima." 

ggg

Andreas Christensen na Franck Kessie wanaweza kuondoka Barcelona kama wachezaji huru ikiwa hawatasajiliwa kabla ya Jumamosi. Wachezaji wote wamesajiliwa majira ya joto. Franck Kessié rai awa Ivory Coast ameingia klabuni hapo akitokea AC Milan huku Andreas Christensen raia wa Denmark akitokea Chelsea. 

Mshambuliaji mfaransa Arnaud Kalimuendo anatarajiwa kujiunga na Rennes muda wowote kutoka hivi sasa kwa ada ya €25m. Kalimuendo amesaini mkataba wa miaka 5 akitokea PSG. 

ggg

Thomas Tuchel na Todd Boehly wanashinikiza Chelsea kumsajili mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang. 

Aubameyang ,33, alijiunga na Barcelona mwaka 2022, ambapo amefunga magoli 11 katika michezo 17. 

Chelsea wanamuona kama mshambuliaji sahihi kwao baada ya kuondoka kwa Romelu Lukaku na Timo Werner hivi karibuni.