EPL: Liverpool yabamizwa na Aston Villa kwa mabao 7 kwa 2
Iliyochapishwa
Mchezo wa mwisho kabisa kunako ligi kuu soka England jana jioni ulikua kati ya Aston Villa iliyoichezesha kindumbwendumbwe Liverpool kwa kuichapa mabao 7-2. Kocha wa Liverpool Jugen Kloop anasema kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wake kama Sadio Mane na mlinda mlango Allison Backer ilikua sababu ya kichapo hicho.
