Israel yawaua Wapalestina wanne baharini

Iliyochapishwa
Jeshi la wanamaji la Israel limewafyatulia risasi mabaharia katika boti la Wapalestina na kuwaua watu wanne.
Israel imesema kuwa watu hao walikuwa wapiganaji waliovalia mavazi ya kupiga mbizi wakiwa na lengo la kushambulia Israel. Kundi la Hamas nchini Palestina limesema kuwa miili ya watu wanne imeopolewa kutoka baharini.

Hii imetokea wakati rais wa Palestina Mahmoud Abbas anahudhuria mkutano wa dharura wa kikanda nchini Uturuki baada ya shutuma nyingi kutolewa na jamii ya kimataifa juu ya shambulio lililotekelezwa na Israel dhidi ya meli za msaada za Palestina wiki iliyopita.



























