Tunisia, Angola zafuzu nusu fainali CHAN
Iliyochapishwa
Tunisia na Angola zimefanikiwa kuingia hatua ya mtoano ya mashindano yanayoendelea ya Ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani (CHAN).

Wamefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kuwalaza Senegal na Rwanda.
Tunisia iliifunga Senegal 2-0 kufika hatua hiyo na kuongoza katika kundi D, wakati Angola ikiwa imelala bao moja, ilifanikiwa kujitutumua na kuizaba Rwanda 2-1.
Tunisia sasa watakabiliana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika hatua ya robo fainali siku ya Jumamosi, wakati Angola watapepetana na Cameroon siku hiyo hiyo.
Rwanda imefunganya virago na kurejea nyumbani bila ya pointi yoyote katika mashindano hayo.



























