FA kumuadhibu meneja wa Leicester City

Nigel Pearson
Maelezo ya picha, Nigel Pearson
Iliyochapishwa

Meneja wa Leicester City Nigel Pearson atapewa adhabu na chama cha soka cha uingereza FA. Pearson mwenye miaka 51amekutwa na hatia ya kutumia matusi kuelekea kwa watazamaji wakati timu yake ikipoteza mchezo dhidi ya Liverpool. Makundi ya mshabiki wa timu hiyo wamemtaka Pearson kuomba msamaha. Huku kipa wa timu hiyo Kasper Schmeichel anatarajiwa atafanyiwa upasuaji siku ya ijumaa baada ya kuwa amevunjika upasuaji huu utakao muweka nje ya uwanja kwa wiki nne mpaka sita. Nafasi yake itachukuliwa na kipa namba mbili Ben Hamer atakaecheza mchezo wa wikiendi ijayo dhidi ya Manchester City