Cuba kuondolewa vikwazo na Marekani?

Rais wa Cuba, Raul Castro
Maelezo ya picha, Rais wa Cuba, Raul Castro
Iliyochapishwa

Rais wa Cuba, Raul Castro, amemhimiza rais Obama wa Marekani kutumia mamlaka yake ya urais kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo jambo linalopingwa na bunge la Congress lililo na wajumbe wengi wa chama pinzani cha Republicans.

Castro amesema, hatua ya Marekani ya kurudisha uhusiano wa kidplomasia na Cuba haikutakuwa na maana yoyote iwapo hatua hiyo haitaandamana na kuondolewa kabisa vikwazo hivyo vya kiuchumi dhidi ya nchi yake vilivyowekwa yapata miaka 50 iliyopita.Pia anataka kurudishwa kwa mamlaka ya Cuba eneo la Guatanamo bay linalotumiwa na Marekani kama gereza na kituo cha kijeshi.