Afisa jela kuhatarisha usalama wa ndege

Chanzo cha picha, Reuters
Mahakama nchini Korea Kusini imemtia hatiani afisa mtendaji wa zamani wa shirika la ndege la taifa, "Korean Airline" kwa kosa la kuvunja sheria ya usalama katika ndege, ikijulikana kama "kesi ya njugu".
Heather Cho, ambaye pia anajulikana kama Hyun-ah, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela akipona kifungo cha miaka 10 ambayo ni adhabu ya juu kabisa kwa kosa hilo.
Cho aliilazimisha ndege iliyokuwa ikielekea Seoul kurudi katika lango na kumshusha mhudumu wa ndege hiyo kwa sababu hakupenda namna alivyokuwa akigawa njugu.
Kesi hiyo ilimpata mvuto mkubwa duniani na kusababisha kupewa uzito mkubwa nchini Korea Kusini.
Cho, ambaye alikuwa makamu wa rais katika shirika la ndege, alipatikana na hatia ya kuvuruga usalama wa ndege
Ndege yake ilikuwa katika eneo la kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFK mjini New York, tarehe tano Desemba wakati watu walioshuhudia wanasema Cho alichukia baada ya kugawiwa njugu aina ya macadamia ambazo hakuomba kupatiwa na ambazo akizigawa zilikuwa ndani ya mfuko badala ya kuweka kwenye bakuli.

Chanzo cha picha, AFP
Aliamuru ndege hiyo kurudi katika lango la kupandia na kumshusha mhudumu mkuu.
"Hii ni kesi ambayo utu wa binadamu umechezewa" amesema Jaji Oh Sung-woo siku ya Alhamisi.
Cho ni mtoto wa kike wa mwenyekiti wa shirika la ndege la Korean Air, na kufanya kuwepo madai kwamba biashara hiyo ya ndege imekuwa ya kifamilia.
Cho alifanya anachotaka katika ndege hiyo"kana kwamba ilikuwa ndege yake binafsi", amesema Jaji Oh. "Inatia mashaka kwamba namna njugu zilivyogawiwa zilitolewa kimakosa."
Jaji amesema Cho ameshindwa kujutia kosa lake hata baada ya kuwasilisha barua mahakamani akiomba msamaha kutokana na tukio hilo.
Waendesha mashitaka waliomba mahakama itoe adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja sheria za usalama wa ndege, shambulio na kuingilia uchunguzi wa kesi hiyo.
Watu walioshuhudia tukio hilo wametoa ushahidi wakati wa kesi hiyo kwamba Cho alimpiga mfanayakazi wa ndege hiyo na kitabu cha maelezo ya huduma za ndege.
Cho, ambaye ni binti wa mwenyekiti wa shirika la ndege la Korean Air, ameomba radhi hadharani kwa kitendo alichofanya na kujiuzulu mwezi Desemba nyadhifa zote alizokuwa nazo katika shirika hilo la ndege.































