Chupi inayobana yamtoa m'bunge bungeni

Suruali ya ndani iliobana yamtoa mbunge ndani ya bunge Canada
Maelezo ya picha, Suruali ya ndani iliobana yamtoa mbunge ndani ya bunge Canada
Iliyochapishwa

Mbunge mmoja wa Canada alitoa sababu ambayo haijawahi kusikika iliomlazimu kutoka bungeni kwa haraka.

Amesema kuwa suruali yake ya ndani ndio iliomlazimu kuondoka mapema kwa kuwa ilikuwa ikim'bana.

Mbunge huyo wa upinzani Pat Martin alimwambia Spika kwamba vazi hilo lilimbana sana na kumzuia kuweza kuendelea na kikao cha kupiga kura.

Hatahivyo alifanikiwa kurudi kwa wakati na kupiga kura yake.

Bunge la Canada
Maelezo ya picha, Bunge la Canada

Baadaye mtandao wa twitter ulijaa ujumbe wa kisa hicho.

Mbunge huyo alizua ucheshi miongoni mwa wabunge wenzake liposema kwamba alinunua suruali hiyo kwa bei ya chini bila kujua kwamba ilikuwa ndogo.

Spika wa bunge hilo alisema kwamba alimuagiza mbunge huyo kuketi chini wakati alipotaka kutoka.