Uhamiaji:Cameron kuishawishi Ujerumani

Chanzo cha picha, BBC World Service
Iliyochapishwa
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron yuko Berlin Ujerumani, kwa mazungumzo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel, kuhusiana na mageuzi katika jumuia ya muungano wa bara ulaya.
Bwana Cameron atajaribu kumshawishi Bi Merkel, kuunga mkono mapendekezo ya mabadiliko katika jumuia hiyo.

Chanzo cha picha, AFP
Tayari amekutana na Waziri mkuu wa Polland, Ewa Kopacz, ili kujaribu kumshawishi aunge mkono mipango ya sheria kali kwa wafanyikazi wahamiaji.

Chanzo cha picha, Getty
Polland imekuwa ikipinga, mpango wa kupunguza manufaa ya wahamiaji wa Ulaya.
Msemaji wa Downing Street, amesema kuwa viongozi hao wawili, walikubaliana kuwe na majadiliano zaidi kuhusiana na maswala hayo.



























