Mkataba wa amani wa Sudan-K watarajiwa

Chanzo cha picha, bbc
Iliyochapishwa
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini yuko Ethiopia kwa mazungumzo yanayokusudiwa kumaliza vita vya zaidi ya mwaka mmoja na nusu katika nchi hiyo.
Viongozi wa serikali na wapiganaji wanakabili vikwazo vya kimataifa iwapo watashindwa kutia saini mkataba wa amani ifikapo Jumatatu.
Pande zote mbili zinasema zinahitaji muda zaidi kutatua maswala kama kugawana madaraka baina yao katika serikali ya mpito.
Marais wa Uganda, Kenya na Ethiopia piya wanashiriki katika mkutano huo.
Juhudi zilizofanywa awali kumaliza vita vya mwaka mmoja na nusu, hazikufanikiwa.
Lakini redio na televisheni ya taifa ya Ethiopia imesema makubaliano yanatarajiwa kutiwa saini



























