Soko la hisa Uchina laathiri bara Afrika

Soko la hisa la china laporomoka na kuathiri sarafu za Afrika
Maelezo ya picha, Soko la hisa la china laporomoka na kuathiri sarafu za Afrika
Iliyochapishwa

Kuporomoka kwa soko la hisa nchini Uchina kunaendelea kuathiri sarafu na uchumi wa mataifa ya bara la Afrika.

Soko la hisa la Nigeria lilirekodi biashara ya chini katika kipindi cha miezi sita mapema siku ya jumanne huku wasiwasi kuhusu kushuka kwa bei ya mafuta pamoja na matukio ya Uchina yakiwashinikiza raia kuuza hisa zao.

Sarafu nyingine pia zimekuwa chini ya shinikizo ukilinganisha na sarafu ya dola.

Soko la hisa la Uchina
Maelezo ya picha, Soko la hisa la Uchina

Sarafu ya Kwacha nchini Zambia ,ile ya Uganda, shilingi ya Kenya na Cedi ya Ghana zimeporomoka thamani yake.

Nchini Nigeria,banki kuu inajaribu kudhibiti kiwango cha Naira kuwa 200 kwa dola.