Mkuu wa Majeshi aapa kutokomeza Boko Haram

Chanzo cha picha, Nigeria Govt
Iliyochapishwa
Mkuu wa majeshi nchini Nigeria, ameapa kuwa atawashinda wapiganaji wa Kiislamu waBoko Haram, kufikia mwisho wa mwaka huu.
Katika mohojiano na BBC, Luteni Generali Tukur Yusuf Buratai, amesema kuwa wanamgambo hao wa wamesambaratishwa kwa kiasi kikubwa.
Buratai hata hivyo amekanusha madai kuwa watu mia saba wameuawa na Boko Haram, tangu rais Muhammadu Buhari, achukue uongozi wa taifa hilo Mei mwaka huu.
Mkuu huyo wa majeshi ameelezea matumaini yake kuwa Marekani itakubali ombi la serikali ya Nigeria, ka kuipa silaha ili kusaidia harakati ya kupambana na wanamgambo hao wa Kiislamu.




























