Je Catalonia itajitenga na Uhispania ?

Zaidi ya watu milioni tano wamejiandikisha kupiga kura .
Maelezo ya picha, Zaidi ya watu milioni tano wamejiandikisha kupiga kura .
Iliyochapishwa

Watu wa eneo la Catalonia nchini Uhispania wameanza kupiga kura katika uchaguzi uunaotazamwa kuwa mtihani mkubwa wa kuunga mkono Uhuru wa eneo hilo tajiri.

Zaidi ya watu milioni tano wamejiandikisha kupiga kura .

Wanachama wa vyama vya Catalan, wanaotaka kujitenga na ambao wanaongoza katika kura ya maoni wanasema kuwa ushindi utavipa vyama vyao uwezo wa kutangaza

Je Catalonia itajitenga na Uhispania ?
Maelezo ya picha, Je Catalonia itajitenga na Uhispania ?

kwa kauli moja uhuru wao.

Serikali ya Uhispania ambayo inakataa kata kata kukubalia shughuli hizo za upigaji wa kura ya maoni kuhusiana na swala hilo imetaja kura hiyo ya maoni kama upuzi

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola akipiga kura
Maelezo ya picha, Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola akipiga kura

mtupu.

Uchaguzi huo unaonekana kama swala muhimu katika historia ya hivi punde ya Uhispania.