Kwa nini serikali ya Kenya haina fedha?

Chanzo cha picha, Reuters
Iliyochapishwa
Wabunge nchini Kenya wanakutana katika kikao cha dharura ili kubaini kwa nini serikali haina fedha.
Malipo muhimu hayajafanywa na hivyobasi kuathiri wizara nyingi na huduma kwa uma pamoja na bunge lenyewe ambalo umeme umekatwa kwa siku kadhaa.
Hatua hiyo imesababisha huduma za maji na usafi kuzorota na wabunge wanasema kuwa hali hiyo haikubaliki.
Baadhi yao wanashtumu wizara ya fedha kwa kuzuia fedha, huku wengine wakiwalaumu wasimamizi wa bunge kwa kutotoa habari mapema kuhusu madeni ambayo hayajalipwa.
Kushuka kwa thamani ya shilingi pia kumeathiri mipango ya serikali kuchukua mkopo ili kusaidia bajeti ya mwaka huu.



























