Simba auawa baada ya kutoka mbugani Nairobi

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Simba mmoja aliyetoroka mbuga ya taifa ya wanyamapori ya Nairobi nchini Kenya amepigwa risasi na kuuawa na maafisa wa kutunza wanyamapori baada ya kumshambulia na kumjeruhi mtu mmoja.

Simba huyo alikuwa ameingia maeneo ya makazi karibu na kituo cha kibiashara cha Isinya.

Msemaji wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori Kenya (KWS) Paul Gathitu ameambia kituo cha redio cha Capital FM kwamba maafisa walilazimika kumpiga risasi mnyama huyo kwa sababu alikuwa anatishia usalama wa watu.

Visa
Maelezo ya picha, Visa vya simba kutoka mbuga ya Nairobi vimeongezeka

Alisema maafisa hao walikuwa wametumwa wakiwa na nia ya kumdhibiti lakini akawa mkali zaidi.

Kisa hicho kimetokea siku chache tu baada ya simba mwingine kutoka mbugani na <link type="page"><caption> kumjeruhi mzee wa umri wa miaka 63</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/03/160318_lion_injure_man" platform="highweb"/></link> katika eneo la Cabanas, karibu na uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Mwezi uliopita, <link type="page"><caption> simba wengine wanne</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/02/160219_lioness_nairobi_national_park" platform="highweb"/></link> walitoka mbugani na kuingia eneo la makazi Lang’ata.