Maelfu watarajiwa kujitokeza kumuaga Papa Wemba

Papa Wemba
Maelezo ya picha, Mwili wa Papa Wemba utazikwa Jumatano
Iliyochapishwa

Maelfu ya watu wanatarajiwa kujitokeza leo mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za rumba Papa Wemba.

Leo ndiyo ni siku ya kwanza ya kipindi cha siku tatu za maombolezo rasmi ya kumuenzi mwanamuziki huyo nchini humo.

Wemba, 66, aliyesifika kote duniani kama mmoja wa wanamuziki nguli wa nyimbo za rumba kutoka DR Congo, alifariki baada ya kuzirai <link type="page"><caption> akitumbuiza mjini Abidjan</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/04/160424_papa_wemba_is_dead" platform="highweb"/></link> wiki moja iliyopita.

  • <link type="page"><caption> Video: Wasifu wa Papa Wemba</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/04/160428_video_papa_wemba_history" platform="highweb"/></link>
  • <link type="page"><caption> Faly Ipupa na mashabiki waulaki mwili wa Papa Wemba</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/04/160428_faly_ipupa" platform="highweb"/></link>

Alipendwa sana na mashabiki kwa nyimbo zake na pia mtindo wake wa mavazi.

Wemba
Maelezo ya picha, Mwili wa Papa Wemba ulisafirishwa hadi Kinshasa Alhamisi

Mwanamuziki huyo, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, anatarajiwa kuzikwa Jumatano.

Rais Joseph Kabila ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ya wafu leo kwa heshima ya marehemu mjini Kinshasa.