Odinga atahadharisha kuhusu uchaguzi Kenya

Raila Odinga
Maelezo ya picha, Raila Odinga
Iliyochapishwa

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amesema kuwa uchaguzi wa mwaka ujao hautofanyika ikiwa makimishna wa tume ya uchaguzi hawataondolewa ofisini.

Waziri huyo mkuu wa zamani amekuwa akiongoza maandamano kila Jumatatu katika mji mkuu Nairobi kushinikiza kujiuzulu kwa makimishna wa tume ya uchaguzi.

Maandamano yamekuwa yenye ghasia.
Maelezo ya picha, Maandamano yamekuwa yenye ghasia.

Makimishna hao wamekataa kung'atuka na badala yake kuutaka upinzani kutumia bunge kuwaondoa ofisini.

Baadhi ya maandamano yamekumbwa na ghasia ikiwemo uporaji na ukatili wa polisi ulionaswa na kamera.