Kijana aliyepotea Japan apatikana

Watu waliokuwa wakimtafuta kijana huyo washangilia habari za kupatikana kwake akiwa hai
Maelezo ya picha, Watu waliokuwa wakimtafuta kijana huyo washangilia habari za kupatikana kwake akiwa hai
Iliyochapishwa

Mvulana mwenye umri wa miaka saba,Yamato Tanooka aliyepotea nchini Japan Jumamosi iliyopita sasa amepatikana akiwa hai.

Maafisa wa utawala katika kisiwa cha Hokkaido wanasema alipatikana na mwanajeshi mmoja katika kituo cha kufanyia mazoezi nje ya mji wa Shikabe mnamo Ijumaa.

Yamato Tanooka 7,aliyekuwa amepotea nchini Japan
Maelezo ya picha, Yamato Tanooka 7,aliyekuwa amepotea nchini Japan

Kijana huyo huyo ambaye aliachwa na babake mwituni kama adhabu alitembea kwa zaidi ya kilomita 4 hadi ukingoni wa msitu huo alipotulia.

Anasemekana kuwa katika hali nzuri ya kiafya ingawa amepelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Maafisa wa utawala katika kisiwa cha Hokkaido wanasema alipatikana na mwanajeshi mmoja katika kituo cha kufanyia mazoezi nje ya mji wa Shikabe mnamo Ijumaa.
Maelezo ya picha, Maafisa wa utawala katika kisiwa cha Hokkaido wanasema alipatikana na mwanajeshi mmoja katika kituo cha kufanyia mazoezi nje ya mji wa Shikabe mnamo Ijumaa.

Inasemekana kuwa alipopatikana alikuwa na njaa na baridi lakini katika hali nzuri.

Babake mtoto huyo aliwambia waandishi wa habari kuwa alimwomba msamaha na kuwa alifurahi kuwa mwanawe alipatikana akiwa hai.