Mpenzi wa Jinsia moja ashtaki ubaguzi wa kitabu China

Chanzo cha picha, AFP
Mahakama ya Beijing imekubali kesi moja ya mwanamke dhidi ya wizara ya elimu nchini humo kuhusu kitabu kimoja kinachoelezea kuwa usagaji ni ugonjwa wa kiakili.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoka eneo la Guangdong ambaye ni msagaji na hujulikana kwa jina Qui Bai amekuwa akifanya kampeni ya mabadiliko.
Maoni ya Wachina kuhusu usagaji yamepungua makali katika siku za hivi karibuni na kitendo hicho kilifanywa kutokuwa cha uhalifu mwaka 1997.
Hatahivyo ubaguzi wa wapenzi wa jinsia moja bado unaendelea.

Chanzo cha picha, AFP
Mapema wiki hii,vyombo vya habari vya Uchina viliripoti kuhusu mpenzi mmoja wa jinsia moja aliyeishtaki hospitali moja kwa kumshambulia baada ya mkewe na familia yake kumpeleka ii afanyiwe matibabu.
Mwaka wa 2014 bi Qui alikuwa akitafuta ufahamu kuhusu wanaume wanaojamiana kwa lengo fulani.
Sipendelei ubaguzi katika shule zetu na vifaa ninavyotumia kila siku.
Aliishtaki wizara ya elimu mwaka 2015 lakini akaraiwa kuiondoa kesi hiyo mnamo mwezi 2015 ambapo alitakiwa kufanya mazungumzo badala ya kuanzisha mashtaka.

Lakini baada ya barua zake kutozingatiwa alianzisha mashtaka mengine mnamo mwezi Aprili 2016 ambapo yalikataliwa na mahakama kwa madai kwamba ukosefu wa jibu kutoka kwa mahakama haukukandamiza haki zake.































