Mwanariadha Omanyala: 'Kila changamoto hukufanya uwe na nguvu zaidi

Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Mkenya Ferdinand Omanyala amezungumzia atatizo yake ya hivi majuzi ya kufika kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia nchini Marekani na kushindwa katika nusu fainali ya mbio za mita 100.

Moja kwa moja

  1. Mwisho wa matangazo ya habari zetu za moja kwa moja leo, tukutane kesho tena majaliwa

  2. Ndege iliyokuwa na shehena za silaha yaanguka na kuua 8

    Greece plane crash:

    Ndege ya mizigo iliyoanguka kaskazini mwa Ugiriki ilikuwa imebeba tani 11 za silaha - ikiwa ni pamoja na mabomu ya ardhini - ikielekea Bangladesh, maafisa wanasema.

    Watu wanaoishi ndani ya kilomita mbili kutoka eneo ambalo Antonov-12 ilianguka wameonywa kusalia ndani ya nyumba.

    Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Serbia kuelekea Jordan ilipoanguka Jumamosi jioni karibu na mji wa Kavala, na kuua watu wote wanane waliokuwa ndani.

    Video ya mashuhuda ilionyesha ndege hiyo ikiwaka moto na moto mkubwa wakati ikianguka. Ndege zisizo na rubani zilitumika kuchunguza eneo la mabaki hayo kwa tahadhari, huku TV ya serikali ya Ugiriki ikiripoti jeshi, wataalam wa milipuko na wafanyakazi wa Tume ya Nishati ya Atomiki ya Ugiriki hawakukaribia eneo la tukio kwa hofu ya usalama.

    "Vipimo vya (hewa) kwa sasa havijaonyesha chochote ," Luteni Jenerali Marios Apostolidis, wa Kikosi cha Zimamoto cha Kaskazini mwa Ugiriki, aliwaambia waandishi wa habari.

    Rubani aliripotiwa kuomba kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Kavala nchini Ugiriki, kutokana na tatizo la injini muda mfupi baada ya kupaa, lakini hakuweza kufika kwenye njia ya ndege.

  3. Tetesi kubwa tano za soka jioni leo: Baada ya Martinez, Man Utd macho kwa Toney, Rooney kwa Jones

    Martinez

    Manchester United baada ya kumtangaza punde tu kumsajili mlinzi Lisandro Martinez kutoka Ajax kwa ada ya £57m sasa inaekeleza nguvu zake kwa Ivan Toney, huenda ikapeleka ofa kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Brentford (Sunday Mirror)

    Wayne Rooney anafikiria kumpa nafasi mlinzi wa kati wa Manchester United, Phil Jones ya kuungana nae pale DC United anakofundisha sasa kwenye ligi kuu ya Marekani, MLS. Rooney amejiunga na timu hiyo wiki hii (Sun on Sunday).

    Rooney
    Maelezo ya picha, Rooney (kushoto, na Jones (kulia), enzi wakiwa pamoja Manchester United

    Mlinzi Calving Bassey ametua Amsterdam tayarti kukamilisha uhamisho wake wa kutua Ajax akitokea Rangers ya Scotland (Fabrizio Romano).

    Rangers itapeleka ofa kwa Liverpool kwa ajili ya Ben Davies kurithi mikoba ya Calvin Bassey anayetimikia Ajax (theScottish Sun).

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Memphis Depay amefanya mazungumzo na bodi ya Barcelona kuhusu hatma yake klabuni hapo. Kijiti kaachiwa Dapay kuamua kuhusau hatma yake, licha ya kuungwa mkono na kocha wake Xavi. (Ronamo)

  4. Joto Mediterania: Maelfu waendelea kuokolewa, moto mkubwa ukiendelea

    HEATWAVES

    Ufaransa imewahamisha zaidi ya watu 14,000 waliokuwa kwenye hatari ya moto unawaka kwenye misitu kusini-magharibi, huku moto ukienea pia Hispania, Croatia na Ugiriki.

    Mamlaka huko Gironde, Ufaransa, eneo maarufu la watalii, wamefanikiwa kuwaondoa walinzi waliokuwa kwenye moja ya makambi - watalii wenyewe waliondoka mapema.

    Moto umeenea katika maeneo ya Teste-de-Buch na Landiras. Kusini mwa Hispania, zaidi ya watu 3,200 walikimbia moto katika milima ya Mijas, ingawa baadaye wengine waliweza kurejea.

    Moto huko Ureno umedhibitiwa kwa sasa. Hata hivyo, mamlaka ya Ureno inasema takriban watu 238 wamefariki kutokana na joto katika wiki iliyopita.

    Moto ya Mijas nchini Hispania haiko mbali na Malaga, eneo maarufu la watalii. Kwingineko nchini Hispania, moto mkubwa umezuka katika majimbo ya Castilla y León na Galicia.

  5. Jessie Duarte: Kifo cha mwanaharakati huyu wa Afrika Kusini 'ni pigo' kwa demokrasia' - ANC

    Duarte
    Maelezo ya picha, Jessie Duarte alijtolea maisha yake kupigania usawa, ANC kimesema
    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Mwanaharakati wa kisiasa wa Afrika Kusini Jessie Duarte amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68. Bi Duarte ambaye alikuwa mwanachama wa muda mrefu wa chama tawala cha African National Congress alifariki baada ya kuugua saratani, ANC imesema.

    Alikuwa naibu katibu mkuu wa chama na mwanasiasa mkongwe. Bi Duarte alihudumu kama msaidizi wa binafsi wa Nelson Mandela kutoka 1990-1994 baada ya kuachiliwa kutoka gerezani.

    "tumempoteza Komredi Jessie, ni pigo kubwa, sio tu kwa familia bali kwa vuguvugu la kidemokrasia na nchi kwa ujumla," Msemaji wa Kitaifa wa ANC, Pule Mabe, alisema katika taarifa.

    Wale waliomfahamu binafsi hapo awali walieleza mapenzi yake makubwa kwa ANC na viongozi wake. Hii ilimfanya kuwa mwaminifu sana, lakini alikosolewa kwa kumuunga mkono Jacob Zuma wakati wa urais wake, licha ya baadhi ya vitendo vya kutiliwa shaka alipokuwa madarakani. Atazikwa baadaye leo Jumapili kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu.

  6. Mwanariadha Omanyala: 'Kila changamoto hukufanya uwe na nguvu zaidi'

    Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika Mkenya Ferdinand Omanyala amejibu kifalsafa matatizo yake ya hivi majuzi ya kufika kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia nchini Marekani na kushindwa katika nusu fainali ya mbio za mita 100.

    Ukweli kwamba alifanikiwa kufika kwenye shindano hilo kimiujiza kwani kutokana na hati yake ya kusaifiria kuipata katika dakika za mwisho.

    Alifika nchini Marekani yakisalia masaa matatu kabla ya kuanza kwa mashindano siku ya Ijumaa ambapo aliibuka wa tatu. Lakini alifanikiwa kushika nafasi ya tano katika nusu fainali ya Jumamosi, hivyo kushindwa kutinga fainali. “Kila changamoto unayokabiliana nayo leo hukufanya uwe na nguvu zaidi kesho,” aliandika kwenye Twitter. "Haijalishi ni kiasi gani kitaanguka juu yetu, tunaendelea kusonga."

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Mwanariadha wa Marekani Fred Kerley alishinda medali ya dhahabu ya mita 100, akikimbia kwa sekunde 9.86 katika fainali iliyofanyika Jumamosi. Mnamo Septemba mwaka jana, Omanyala alikimbia kwa sekunde 9.77 jijini Nairobi na kuvunja rekodi ya Afrika.

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2