Wataka miraa irejee sokoni tena Uingereza
Wafanyabiashara wa mirungi au miraa nchini Kenya wanaitaka serikali yao kufanya mazungumzo upya na serikali ya Uingereza kwa lengo la kurejesha tena biashara ya mmea huo Uingereza
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Wanamibia watahadharishwa juu ya matumizi ya kinyesi cha ndovu kama 'tiba' ya corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Matumizi ya kinyesi cha ndovu hayajafanyiwa majaribio ya kisayansi Waziri wa afya wa Namibia Kalumbi Shangula amewaonya watu dhidi ya kutumia kinyeshi cha ndovu "kutibu" Covid-19.
Baadhi ya waganga wa kienyeji wanasema kinyesi cha ndovu kinaweza kuchemshwa na hewa ya mvuke wake kuvutwa kama tiba ya mafua, maumivu ya kichwa na kutokwa damu puani lakini hilo halijathibitishwa kisayansi.
"Nina wasiwasi kuhusu watu ambao sio wa kuaminika wanaoweza kuwafanya watu wengine watumie pesa kwa dawa zisizo za kwa matumaini kwamba watatibiwa," BwanaShangula alinukuliwa akisema na shirika la habari la AFP.
Namibia imethibitisha kuwa watu 4,464 walipatwa na virusi vya corona nchini humo na wengine 37 wamefariki kwa virusi hivyo.
Wafungiwa kazini kwa kuhofia corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wajenzi hawajaruhusiwa kuziona familia zao tangu mwezi Machi Kampuni ya Kichina inayotengeneza kiwandacha saruji katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo imewafungia wafanyakazi wapatao 60, raia wa nchi hiyo katika eneo la ujenzi tangu mwezi Machi.
Wawakilishi wa kampuni hiyo wanasema uamuzi huo ulichukuliwa ili kuzuwia uwezekano wa wafanyakazi hao kumuambukiza virusi vya corona muajiri wao.
Kiwanda cha saruji cha Salamanga kinajengwa katika wilaya ya Matutuone katika jimbo la Maputo.
Uamuzi huo umewafanya wafanyakazi wawe mbali na familia zao.
Wakili Paulino Cossa anasema hatua hiyo inakiuka sharia za kazi
Muwakilishi wa kampuni hiyo anameahidi kuwaachilia wafanyakazi hao wiki ijayo.
Wataka miraa ya irudi sokoni Uingereza
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Peter Mwangangi
- Nafasi, BBC Swahili

Wafanyabiashara wa mirungi au miraa nchini Kenya wanaitaka serikali yao kufanya mazungumzo upya na serikali ya Uingereza kwa lengo la kurejesha tena biashara ya mmea huo Uingereza.
Wanaitaka serikali ya Kenya itatue mzozo wa kibiashara kati yake na Somalia ili ndege zinazobeba bidhaa hiyo ziruhusiwe nchini humo kwani Kenya imefunguliwa tena safari za ndege za nje ya nchi hiyo.
Mwenyekiti wa chama cha wauza miraa -Nyambene Miraa Traders' Association, Kimathi Munjuri anasema Uingereza ilifungia miraa kutokana na shinikizo kutoka kwa Muungano wa bara ulaya EU, lakini sasa kuna nafasi ya mazungumzo mengine.
‘‘Tunaomba serikali yetu iweke swala la miraa mezani wakati wa mazungumzo kati yake na Uingereza kuhusu mikataba maalum ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili,’’ anasema Kimathi.
Ni zaidi ya miaka sita sasa tangu Uingereza kupiga marufuku miraa au mirungi – mmea unaotumiwa kama kisisimuzi au kichocheo cha ulevi.
Madada wanaowakilisha soka ya Malawi kimataifa

Maelezo ya picha, Tabitha na Temwa Chawinga. Wakati Ligi Kuu ya China ya wanawake itakapong’oa nanga wiki hii, kutakua na sura za madada wa Malawi Tabitha na Temwa Chawinga.
Msimu huu utakuwa ni mara ya kwanza kwa madada hawa kucheza mechi wakikabiliana katika timu tofauti kwa mashindano kwani wamekua wakicheza pamoja katika timu ya taifa, klabu ya DD Sunshine ya Malawi na Timu ya Ligi ya Uswisi ya Kvarnsveden.
Temwa, mwenye umri wa miaka 21, atakuwa akichezea timu ya Wuhan FC na anatarajia kufuata nyayo za dada yake baada ya Tabitha kuchaguliwa kama Mchezaji wa mwaka wa Ligi kwa mwaka wa pili.
Tabitha, mwenye umri wa miaka 24, alipata tuzo baada ya kuwa mchezaji aliyefunga magoli zaidi na kuisaidia klabu yake ya Jiangsu Suning na kuifanya kuwa mshindi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Tabitha Chawinga amepata mafanikio makubwa ya Soka China akichezea timu ya Jiangsu Suninh Wapenzi wanaolipwa kuharibu mapenzi
Nchini Japan unaweza kulipa kundi binafsi linalojulikana kama 'wakaresaseya' kumtongoza mpenzi wako.
Mwaka 2010, Takeshi Kuwabara alifungwa jela kwa makosa ya kumuua mpenzi wake, Rie Isohata. Lakini kile kilichozua gumzo sio mkasa wenyewe, ni ukweli kwamba....Bofya hapa kusoma taarifa hii zaidi...
Waziri na Mkuu wa polisi Kenya wahojiwa na Seneti

Maelezo ya picha, Waziri Fred Matiang'i anajieleza mbele ya Seneti juu ya kukamatwa na polisi kwa maseneta Vyombo vya habari nchini Kenya vimezuiwa kufuatilia kikao cha kamati ya seneti ambapo Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang’i na Inspekta Mkuu wa polisi Hillary Mutyambai wanahojiwa juu ya kukamatwa kwa maseneta watatu.
Jumatatu Spika wa Seneti alimtaka waziri Matiang’i kuja bungeni Jumatano kujibu juu ya kukamatwa kwa maseneta Cleophas Malala wa Kakamega, Dkt Steve Lelegwe wa Samburu na Dkt Andrew Langat wa Bomet.
Maseneta walidai kuwa wenzao hao watatu walikamatwa ili kuwazuia wasipige kura ya muswada muhimu wa mgao mapato al maarufu "Shilingi moja,mwanaume mmoja Kura moja ".Awali Maseneta waliapa kutoendelea na vikao hadi wenzao waachiliwe.
Maseneta wote baadae waliachiliwa
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Polisi aliyeonekana akimnyonga mwanaume achunguzwa

Afisa wa polisi katika eneo la West Yoekshire nchini Uingereza anachunguzwa baada ya kupatikana kwa video inayoonesha akimsukuma chini mwanaumehuku akisema "tulia au nikuue".
Video hiyo inaonesha afisa huyo wa polisi alimpiga mweleka mwanaume huyo na kumkamiza chini ardhini na silaha shingoni.
Mwanaume huyo alionekana akigaragazwa sakafuni huku akisema "Basi nimeacha " kabla ya kuambia wan a polisi"geuka sasa " wakati polisi mwingine akisaidia kumshikilia.
Picha hizo kutoka Halifax ilisambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Polisiya West Yorkshire imesema afisa huyo amesimamishwa kazi na tukio hilo limeripotiwa kwenye taasisi inayochunguza minendo ya polisi.
Kiumbe mdogo wa jamii ya tembo agundulika baada ya miaka 50

Chanzo cha picha, Steven Heritage
Maelezo ya picha, Myama huyu ni mdogo kiasi cha kutoshea kwenye kijanja chako Mnyama mwenye asili ya ndovu lakini mwenye umbo dogo sawa na panya amegunduliwa nchini Afrika Kusini baada ya miaka 50 tangu alipotoweka.
Rekodi ya mwisho ya kisayansi juu ya " kutoweka kwa viumbe " hao wa jamii ya ndovu ilitolewa miaka ya 1970, licha ya kuonekana miongoni.
Kiumbe hicho cha jamii ya mamalia kilipatikana kikiwa hai na salama katika taifa la Djibouti, lililoko katika upembe wa Afrika, wakati wa safari ya uvumbuzi wa kisayansi.
Wanyama hao wa jamii ya ndovu, au sengis, sio ndovu wala panya, lakini wana uhusiano na wanayama wanaoitwa aardvarks, ndovu au tembo na viumbe wengine wa baharini wanaofahamika kama manatee.
Wana pua zilizochongoka ambazo wanazitumia kuwawinda na kuwala wadudu.
‘Burundi haiwezi kuondolewa katika Jumuiya ya Afrika Mshariki’

Chanzo cha picha, Ezechiel Nibigira/Twitter
Maelezo ya picha, Ezechiel Nibigira, Waziri wa Burundi wa masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Waziri wa Burundi wa masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) Ezechiel Nibigira, amesemakuwa taarifa kwamba Burundi itaondolewa uanachama wa jumuiya hiyo kwasababu haijalipa ada yake ya ni jambo lisilowezekana
Bwana Ezechiel Nibigira amesema kuwa taifa hilo kwa sasa linalipa deni lake.
Amesema kuwa Burundi inatarajia kulipa hivi karibuni dola milioni 2.6 kati ya dola milioni 6 inazopaswa kulipa.
WaziriNibigira ameiambia BBC kuwa ni kweli Burundi ilichelewa kulipa ada yake. Lakini akasema nchi wanachama zinafahamu kuwa imepitia vipindi vigumu.
Kikao cha mawaziri cha Jumuiya ya Afrika Mshariki kilichokaa tarehe 4 Agosti kilisema kuwa jumuiya hiyo inakabiliwa na matatizo ya kifedha kwasababu mataifa ya Burundi na Sudan Kusini hazilipi mchango wake ipasavyo na kuyataka kulipa ada zake kabla ya tarehe 15 Septemba.
Sudan Kusini inadaiwa deni la dola milioni 24 za ada ya Jumuiya hiyo.
Jeshi la Mali latangaza kuandaa serikali ya mpito

Chanzo cha picha, EPA
Vikosi nchini Mali vimemuondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keïta na kutangaza azma yao ya kuunda serikali ya mpito kabla ya uchaguzi mpya.
Hii inakuja baada ya rais Keïta kuonekana kwenye televisheni akisema kuwa amejiuzulu.
Yeye na Waziri mkuu walisindikizwa kwa mtutu wa bunduki kutoka mji mkuu Bamako hadi kwenye kambi ya jeshi.
Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika wamepinga kuchukuliwa kwa uongozi wa nchi na jeshi la Mali.
Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za magharibi, Ecowas, lilitangaza kufunga mipaka na nchi hiyo na imesitisha uhusiano wa kifedha na nchi hiyo.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana baadae Jumatano.
Hujambo na karibu kwa matangazo mubashara ya leo Jumatano tarehe 19.08.2020
