Tanzania yaondoa marufuku dhidi ya ndege za Kenya
Tanzania imeondoa marufuku ya safari za ndege za Kenya iliyokuwa imeiweka mwezi uliopita
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Taji alilovaa Notorious B.I.G lauzwa maelfu ya dola

Chanzo cha picha, G
Taji alilovaa msanii maarufu wa mtindo wa Hip hop, marehemu Notorious B.I.G alilovaa katika picha aliyopigwa muda mfupi kabla ya kuuawa kwake,limenunuliwa dola 594,750, kwa mujibu wa kampuni ya biashara Sotheby iliyoliuza.
Mauzo ya taji hilo yamefanyika katika mnada uliofanyika usiku wa Jumanne mjini New York ambapo pia barua za mapenzi za Tupac Shakur alipokuwa kijana mdogo ziliuzwa.
Mwezi uliopita , kampuni ya Sotheby's ilikuwa imesema taji hilo litagharimu kati ya dola 200,000 na dola 300,000, za Marekani na sasa limeuzwa kwa karibu mara mbili ya thamani iliyokadiriwa awali.
Notorious B.I.G au Biggie alivaa taji hili siku tatu tu kabla ya kupigwa risasi hadi kufa tarehe 09/03/1997, akiwa na umri wa miaka 24.
Barua za Tupac Shakur alizomuandikia mpenzi wake waliyekuwa wakisoma pamoja katika shule ya Baltimore, ziliuzwa dola 75,600.
Je kuna chembechembe za uhai katika sayari ya Venus?
Wazo kwamba viumbe wanaoishi wanaelea katika mawingu ya sayari ya venus ni uwezekano uliopo.
Lakini hilo ni kwa mujibu wa wataalamu wa angani baada ya kugundua kitu kilichopo angani ambacho hakiwezi kuelezeka.
Ni gesi kwa jina Phosphane PH3, molekyuli ilioundwa kutokana na atomu moja ya Phosphorous na tatu za Hydrogen... Soma zaidi taarifa hii
Kuna matumaini madogo ya ukuaji wa uchumi wa Kenya

Chanzo cha picha, AFP
Shirika linaloongoza kwa utoaji wa viwango linasema uchumi wa Kenya utakua kwa asilimia moja mwaka 2020, kikiwa ni kiwango cha chini cha matarajio ya ukuaji kilichotolewa awali.
Awali Shirika hilo Moody lilibashiri kuwa kiwango cha uchumi wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki kingefika asilimia sita kabla ya kuwasili kwa virusi vya corona.
Sekta ya utalii imeathiriwa kwa kiwango kikubwa na janga la corona, na huenda isiweze kurejea katika hali yake ya awali kwa miaka mitatu.
Hatahivyo Moody linasema kutakuwa na ukuaji wa uchumi wa takriban asilimia tano katika mwaka 2021.
Limeonya, hatahivyo, juu ya kuongezeka kwa hasara kwasababu ya kushuka kwa kiwango cha kodi ya mapato na kubanwa kwa matumizi ya serikali.
Shirika la fedha duniani IMF limebashiri kuwa chumi za mataifa yote ya bara la Afrika zitapungua kwa asilimia moja nukta tano katika mwaka 2020.
Marekani yamuwekea vikwazo mke wa rais zamani wa Gambia

Chanzo cha picha, Getty Images
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zineb Jammeh, mke wa rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh.
Zineb anaaminiwa kusaidia au kuruhusu shughuli za ufisadi wakati wa utawala wa mume wake wa miaka 22 katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.
"Zineb Jammeh alitumia nafasi yake kusaidia kwa mali, kudhamini, au kutoa usaidizi kwa mume wake. Alitumia wakfu na misaada kama chambo kusaidia usafirishaji haramu wa pesa kwa mume wake," taarifa ilisema.
Rais huyo wa wa zamani aliiongoza Gambia kwa miaka 20. Alitoroka nchi baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2017 na sasa anaishi Equatorial Guinea.
Ecowas inatumai utawala wa kiraia utarejea Mali ' ndani ya siku kadhaa'

Chanzo cha picha, EPA
Rais wa Ghana, Nana Akufo- Addo, amesema viongozi wa magharibi mwa Afrika wana matumaini ya kuiona serikali inayoongozwa na raia ikiwekwa nchini Mali katika kipindi cha siku kadhaa.
Alizungumza baada ya mazungumzo baina ya viongozi wa kikanda na wanamgambo wa Junta ambao walichukua mamlaka nchini Mali mwezi uliopita.
Bwana Akufo- Addo alisema kuwa jumuiya ya kiuchumi ya nchi zilizoko magharibi mwa Afrika Ecowas, wataondoa vikwazo " mara moja " pale raia watakapochukua mamlaka nchini Mali.
Viongozi wa Ecowas walikutana katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kwa mazungumzo juu ya mzozo wa kisiasa wa Mali.
Viongozi wa jeshi la Mali junta, Kanali Assimi Goita, pamoja na wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika pia walihudhuria.
Viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi wanahofia kwamba hali ya usalama nchini Mali inaweza kuharibiwa zaidi na kudhoofishwa kwa juhudi zilizofanyika kuyashinda makundi ya wapiganaji wa kiislamu.
Jumamosi, upinzani unaofahamika kama M5-RFP ulipinga pendekezo la jeshi la mchakato wa kipindi cha mpito cha miezi 18.
Kituo cha habari cha Tanzania chapata watazamaji bilioni moja katika YouTube
Chombo cha habari za mtandaoni nchini Tanzania Millard Ayo kimekuwa cha kwanza barani Afrika kupata watazamaji bilioni moja katika mtandao wa YouTube.
Mmiliki wake-ambaye ana jina hilo hilo- Millard Ayo amewashukuru wale wanaokitazama kituo chake kwa ajili ya kupata habari.
Ali Tweet picha yake ya kusherehekea mafanikio yake:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mwezi Juni, Msanii wa Muziki wa Tanzania Diamond Platnumz alikuwa mwanamuziki wa kwanza wa Afrika mashariki kuwa na ufuasi wa watu bilioni moja
Ndege za Kenya kupaa katika anga za Tanzania tena

Maelezo ya picha, Ndege za Kenya Airways, ni mojawapo ya ndege zilizokuwa zimezuia kuingia Tanzania Tanzania imeondoa marufuku ya safari za ndege za Kenya iliyokuwa imeiweka mwezi uliopita, kulingana na taarifa ya Mamlaka ya safari za anga nchini Tanzania TCAA.
Hatua hii ya Tanzania inakuja baada ya Kenya kuondoa sharti la kuwaweka karantini kwa muda wa siku 14 Watanzania wanoaingia nchini humo...https://www.bbc.com/swahili/habari-54172659
Tanzania ilikuwa imeziwekea marufuku ndege za Kenya Airways, Fly 540, Safarilink na AirKenya express kama hatua ya kujibu hatua ya karantini iliyowekwa awali na Kenya. Hata hivyo ndege hizo sasa zitaruhusiwa kufanya safari zake nchini Tanzania.
Kenya ilisema ilichukua hatua ya kuwaweka baadhi ya wasafiri karantini baada ya kuwasili nchini humo wakiwemo wale wanaotoka nchini Tanzania, kama njia mojawapo ya upunguza kusambaa kwa virusi vya corona.
Hatua zilizochukuliwa na nchi hizi mbili juu zilizouwia usafiri wa anga baina yake zilitia dosari mahusiano yake ya kidiplomasia.
Watuhumiwa 32 washitakiwa kuwa wapiganaji wa kikundi cha uhalifu
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yves Bucyana
- Nafasi, BBC Swahili

Maelezo ya picha, Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yao Kundi la watu 32 wako mahakamani nchini Rwanda kwa tuhuma za kuwa wapiganaji wa kundi la Rwanda National Congress RNC linaloendesha harakati zake mashariki mwa DRC.
Baadhi yao wanaongozwa na Meja mstaafu wa jeshi la Rwanda, Habib Mudathiru ,wengine wakiwa ni askari watoro kutoka jeshi la Rwanda.
Wanashitakiwa kujiunga na wapiganaji wa kundi la RNC ambalo linaongozwa na Jenerali Kayumba Nyamwasa mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda anayeishi uhamishoni nchini Afrika kusini.

Kuna pia wengine waliojiunga na wapiganaji wa vuguvugu la P5 ambalo pia linaendesha harakati zake mashariki mwa DRC.
Wote walikamatwa katika mapigano mashariki mwa Congo mwaka 2019 na baadae kukabidhiwa Rwanda.
Watuhumiwa wengi wanakiri mashitaka dhidi yao na kusema kwamba waliingizwa katika makundi hayo kwa nguvu. Kesi inaendelea.
Polisi Uganda kupima DNA za familia inayodai mtoto aliyekatwa kichwa ni wao

Chanzo cha picha, Rebecca Kadaga/ Twitter
Maelezo ya picha, Manaume aliyekamatwa na kichwa alisema alitaka kuwasilisha mzigo kwa Spika Rebecca Kadaga Polisi nchini Uganda wametibitisha kuwa kichwa cha mtoto kilichokatwa, kilichopatikana katika kikapu cha mwanaume aliyekamatwa kwenye lango la bunge nchini Uganda Jumatatu,kilikuwa ni sehemu ya mwili uliopatikana katika wilaya ya masaka, kusini- magharibi mwa mji mkuu Kampala.
Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai nchini humo anasema wachunguzi watafanya kipimo cha vinasaba DNA kwa wajumbe wa familia moja ya Masaka ambao waliripoti kupotea kwa mtoto wao, kubaini iwapo kweli mtoto huyo aliyekatwa kichwa ni wao.
Familia iliyompoteza mtoto iliviambia vyombo vya habari nchini humo Jumanne, kwamba walikuwa wamemuajiri Joseph Nuwashaba, mwenye umri wa miaka 22, ambaye alipatikana na kichwacha mtoto, kama mfanyakazi wa shamba leo.
Uchunguzi bado unaendelea kubaini ni yapi yalikuwa malengo ya Bwana Nuwashaba, na polisi wamesema watafanya uchunguzi juu wa akili yake.
Alipokamatwa Bwana Nuwashaba aliwaambia maafisa katika bunge kwamba alitaka kuwasilisha mzigo uliokuwa na kichwa kwa Spika wa Bunge Bi Rebecca Kadaga.
Spika hajatoa kauli yoyote juu yatukio hilo, na aliwaambia wabunge kuwa anasubiri matokeo ya uchunguzi wa polisi.
‘Shujaa' wa filamu ya Hoteli Rwanda atapewa haki kisheria, yasema Rwanda

Chanzo cha picha, Reuters
Msemaji wa uendeshaji mashitaka wa umma nchini Rwanda ameihakikishia familia kuwa ‘‘shujaa’’ wa filamu ya Hoteli Rwanda na mpinzani wa nchini hiyo Paul Rusesabagina atapata haki ya kisheria katika kesi dhidi yake inayoendelea.
‘’Hata alipokamatwa ilitangazwa wazi...alipouguwa alipata huduma ya matibabu, alipewa jopo la mawakili tena bure… Kesi itakuwa wazi kwa umma.’’ Amesema msemaji wa ofisi yauendeshaji mashitaka ya umma nchini Rwanda Paul Nkusi katika mahojiano na kipindi cha BBC Newsday
Bwana Nkusi amesema, la muhimu ni kwamba alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Rwanda na sasa yuko mikononi mwa polisi ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili.

Chanzo cha picha, RIB
Bwana Rusesabagina anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya raia, kuwajeruhi raia, kupora na kuharibu mali za raia, kuunda kundi lenye silaha hususan ni FNL ambalo linawatumikisha watoto vitani, na kuhusika katika shuguli za ugaidi, amesema Bwana Nkusi.
Nkusi amesema Rusesabagina binafsi alithibitisha mwenyewe kuhusika katika baadhi ya vitendo hivi.
‘’Ninaweza kutaja baadhi ya ushahidi aliousema mwenyewe…alisema alituma pesa kwa njia ya Western Union na kukusanya pesa za kuunga mkono kikundi cha FNL’’, Alisema Bwana Nkusi.
Familia ya Rusesababigina ambaye alipata umaarufu baada ya kucheza filamu ya Hoteli Rwanda juu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, inasema kuwa alitekwa nyara alipokuwa safarini Dubai katika Muungano wa nchi za kiarabu.
Msemaji huyo wa Ofisi ya mwendesha mashitaka ya umma amesema kuwa kwasasa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Remera na mawakili wake wanamtembelea.
Hujambo na karibu kwa matangazo mubashara leo Jumatano tarehe 16.09.2020
