Ndege za Kenya zaanza safari za kila siku Tanzania
Kampuni ya ndege nchini Kenya, Kenya Airways (KQ) imeanza rasmi safari zake nchini Tanzania baada ya taifa hilo kuondoa marufuku ya safari za ndege za Kenya iliyokuwa imeiweka mwezi uliopita.
Moja kwa moja
Esther Namuhisa
Mwanamke mmoja akimbizwa bila nguo barabarani na 'askari' Msumbiji
Video inayowaonesha wanaume wanne wakiwa na sare za jeshi wanamkimiza huku wakimpiga mwanamke mmoja ambaye hakuwa amevaa nguo na kumtuhumu kuwa mfuasi wa kundi la waasi la IS.
Wakati ambapo rafiki wa mwanamke huyu alikua akirekodi tukio hilo kwa kutumia simu alipigwa risasi na kufariki papo hapo.
Video hii ilitumwa katika mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni huko Msumbiji.
Wataalam wa video za mitandaoni waliweza kufahamu baadhi ya majengo kwenye video hiyo pamoja na miti.Lakini pia wakaona kitu ambacho kipo kwenye mji wa Cabo Delgado Kaskazini mwa Msumbuji, eneo ambalo limekua na migogoro ya mara kwa mara..
David Matsinhe ni mtafiti kutoka Amnesty International ameeleza kuwa sare za wanaume wale pamoja na lafudhi yao inaonesha kuwa walikua wanajeshi wa serikali.
"Viatu vyeusi na sare ambazo zinaonyesha dhahiri ni serikali. Kila kitu kwenye video hii kinaonyesha kuwa ni vikosi vya serikali. Kwa hivyo ni jukumu lao kuruhusu uchunguzi huru na wazi ufanyike, ili wale waliohusika wahukumiwe kwa mujibu wa sheria", David ameeleza.
Video za kutisha na za manyanyaso zimekua zikitoka katika eneo hili ambalo linaonekana kutengwa mara kwa mara.
Baadhi ya video hizo zinatumiwa na waasi wa kundi la kiislamu kuogopesha raia, kundi hili linahusishwa na lile la wapiganaji wa IS.
'Damu ya mgonjwa aliyepona corona inaweza kutibu covid 19'
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Alli Mutasa
- Nafasi, BBC Swahili
Mpaka sasa hakuna tiba au chanjo ya covid-19 duniani, ugonjwa huu unaoathiri vibaya mfumo wa pumzi na huweza kupelekea kifo. Ingawa wanasayansi katika nchi mbalimbali wako mbioni kutafuta dawa au chanjo.
Kuna ushuhuda kwamba maji ya damu ya mgonjwa aliyepona covid-19, huweza kuleta afueni kwa mgonjwa mahututi wa covid-19.
Uganda, imezindua mradi wa kukusanya, kuchakatisha na kutunza 'plasma' ya ahueni ili kuponyesha Covid-19, vile idadi ya vifo na wagonjwa mahututi ikiongezeka nchini humo.
Mradi wa uchunguzi yakinifu wa kukusanya, kuchakatisha na kuhifadhi plazma ya ahueni, kwa lengo la kutibu Covid19 nchini Uganda.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mapafu Chuo kikuu Makarere na kiongozi mradi, Dk Bruce Kirenga anasema walichelewa kidogo kuanza kwa sababu wadhibiti walitaka lazima mfumo mzima wa vibali kupitiwa.
Shughuli za kuwapata watoaji damu, miongoni mwa wagonjwa wa zamani wa covid, ilianza Juni baada ya Baraza la Kitaifa la Sayansi na Teknolojia Uganda kutoa kibali. Jumla ya watu 190 waliendewa – wanawake 8, wanaume 184; 23 walikataa. Na baada ya kuchujwa kwa virusi mbalimbali, mkiwemo vya ukimwi, hepatitisi na kaswende, ni 162 walistahili. Baada ya yote, vizio 127 vya damu vilipatikana.
Lakini Je, idadi hiyo inatosha na watu watakuwa na utashi wa kushiriki?
Maelezo ya sauti, Maji maji ya damu ya aliyepona covid 19 yanaweza kutibu mgonjwa mahututi wa corona Waziri wa zamani wa ulinzi atangazwa kuwa rais wa mpito Mali

Chanzo cha picha, AFP
Waziri wa zamani wa ulinzi nchini Mali, Bah Ndaw ameteuliwa kuwa rais wa mpito wakati kanali Assimi Goita atakuwa makamu wake, televisheni ya taifa nchini humo imetangaza.
Jeshi la Mali limekuwa na mvutano mkubwa kutoka kwa viongozi wa Afrika Magharibi kurejesha utawala kwa raia baada ya rais Ibrahim Boubacar Keïta kuondolewa madarakani mwezi mmoja uliopita.
Bwana Ndaw ni mwanajeshi mstaafu ambaye alikuwa waziri wa ulinzi wakati bwana Keïta akiwa madarakani.
Viongozi wa Afrika Magharibi walisisitiza wiki iliyopita kwamba ateuliwe rais wa mpito ambaye ni raia wa kawaida, huku kukiwa na dalili kuwa askari atakuwa makamu wake, kwa kipindi cha mpito cha miezi 18-kabla ya uchaguzi.
Haijawekwa wazi kama bwana Ndaw atakubaliwa na Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika magharibi Ecowas, au vyama vya upinzani .
Ndege za Kenya zaanza safari za kila siku Tanzania

Kampuni ya ndege nchini Kenya, Kenya Airways (KQ) imeanza rasmi safari zake nchini Tanzania baada ya taifa hilo kuondoa marufuku ya safari za ndege za Kenya iliyokuwa imeiweka mwezi uliopita, kulingana na taarifa ya Mamlaka ya safari za anga nchini Tanzania TCAA.
Ndege hiyo ya Kenya imeanza rasmi safari mara mbili kutoka Dar es Salaam mpaka Nairobi na mara tatu kwa wiki kuelekea Zanzibar.
Hatua hii ya kufunguliwa kwa ndege za Kenya kwenda nchini Tanzania imekuja baada ya Kenya kuondoa sharti la kuwaweka karantini kwa muda wa siku 14 Watanzania wanaoingia nchini humo
Nini hatma ya muungano wenye utata DRC?

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi amekuwa na mikutano ya nadra na aliyekuwa rais wa taifa hilo Joseph Kabila wakati muungano wa vyama vyao ukiwa na mvutano.
Viongozi hao wawili walijadili kuhusu maendeleo ya muungano wao.
Licha ya kwamba bwana Tshisekedi alishinda urais, chama cha Kabila bado kina viti vingi vya wabunge .
Majadiliano kati ya vyama hivi yalichukua muda wa miezi saba kabla ya makubaliano kupatikana ili serikali kuundwa.
Mahusiano kati ya vyama viwili yamekuwa ya uhasama, wanasiasa wenye upinzani wamekuwa wakirushiana maneno ya kashfa na wakati mwingine kufanya ghasia.
Mikutano kati ya bwana Tshisekedi na Kabila imeweza kupunguza kwa kiwango kidogo mvutano ambao umekuwepo kwa miezi kadhaa, AFP imeripoti.
EU yaviwekea vikwazo silaha zinazopelekwa Libya

Chanzo cha picha, AFP
Umoja wa Ulaya (EU) umeziwekea vikwazo kampuni tatu kwa kukiuka zuio la Umoja wa mataifa kwa taifa la Libya.
Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje mjini Brussels umeamua kutatua changamoto hiyo kwa kuzifungia kampuni tatu zinazopeleka silaha Libya.
Vilevile watu wawili waliwekewa zuio kwa kukiuka haki za binadamu nchini Libya.
"Orodha mpya inaonyesha kuwa mikakati ya EU ni kuweka vikwazo ili kuunga mkono maendeleo ya harakati za kisiasa na kuzuia wahalifu wa zamani na sasa kufanya uhalifu zaidi," taarifa kutoka EU imeeleza.
Kampuni hizo tatu zilizofungiwa ni kutoka Uturuki, Kazakhstan na Jordan , wakala wa habari AFP imeripoti.
Ripoti ya Umoja wa mataifa mapema mwezi huu ilionekana ukiishutumu Urusi ,Uturuki na Nchi za Falme za kiarabu (UAE) na mataifa mengine ambayo yalikaidi waziwazi zuio la kimataifa na kupeleka silaha Libya.
Libya imekuwa katika ghasia kwa muda mrefu tangu kuuawa kwa kiongozi wao kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011 na jeshi la Nato.
Mataifa ya Falme za kiarabu yanamuunga mkono jenerali Khalifa Haftar, wakati Uturuki ikiwa inamuunga mkono mpinzani wake aliyepo Tripoli.
Je televisheni inaweza kuwa mbadala wa darasa au shule?
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yves Bucyana
- Nafasi, BBC Swahili

Rwanda imeanzisha njia mpya ya kufundishia kwa kutumia televisheni na redio wakati huu ambao shule zimefungwa kutokana na covid 19, lakini swali kwa wazazi na jamii ni Je njia hii mpya inaweza kutoa matokeo kama yale ya darasani.
Baadhi ya wazazi wanasema ni vigumu kwa wanafunzi kufuatilia masomo kwa njia hiyo.
Katika shule binafsi kutumia mfumo wa whatsapp kutuma masomo kwa wanafunzi wao wakati baadhi ya walimu walianza kufundisha kwa kutumia chaneli za youtube baada ya mishahara yao kusimamishwa.
Mpango wa masomo yanayotolewa kupitia redio na televisheni ya taifa kama njia mbadala inayotumiwa na taasisi ya elimu ya Rwanda (Rwanda Education Board) ni kusaidia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutosahau masomo wakati huu wa mlipukjo wa Covid19 ambapo shule zilifungwa.

Ni mpango ulioibua maswali mengi hasa baadhi ya wazazi wakiona kwamba una changamoto nyingi na matatizo kwa watoto:
‘’Mfumo huu una changamoto nyingi,kwanza mtoto akiangalia TV anashawishika kuangalia mambo mengine. Changamoto nyingine ni kwa sisi wazazi ,masomo hutolewa wakati wazazi wengi hawapo nyumbani ,aidha ni vigumu kwa wazazi ambao hawakusoma huwa hawawezi kuwasaidia watoto wao wanapohitaji usaidizi’’
Aidha kuna wananchi wengi nchini ambao wanasema hawana Redio na TV wala huduma ya umeme,
je wao watasaidikaje?

‘’Mimi najiuliza ,Watoto wangu watawezaje kufuatilia masomo hayo? sina simu,radio wala TV kwa hiyo siwezi hata kuwaza kwamba hayo masomo yapo’’.
Hata hivyo taasisi ya elimu ya Rwanda inasema imeanza kusambaza redio zisizohitaji umeme katika baadhi ya vijiji ili kusaidia wanafunzi kufuatilia masomo yanayotolewa.
Karibu katika matangazo mubashara
