Wanajeshi wanne wa Rwanda wauawa Msumbiji
Wanajeshi wanne wa Rwanda wameuawa katika operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wa nchini Msumbiji katika jimbo la Cabo Delgado , kwa mujibu wa Rwandan press.
Moja kwa moja
Wapinzani waondoka bungeni Uganda kutokana na kushikiliwa kwa wabunge
Wabunge wa upinzani nchini Uganda wametoka bungeni baada ya Waziri Mkuu na Mwanasheria kushindwa kutoa jibu la kuridhisha kuhusu ni wapi walipo wabunge wawili wawili wa upinzani.
Wabunge , Mohammed Ssegirinya na Allan Ssewanyana, woter kutoka chama cha Bobi Wine chana National Unity Platform , waliachiliwa hivi karibuni kwa dhamana baada ya kushitakiwa kwa mauaji yaliyohusiana na mashambulio yaliyotokea katika jimbo la kati nchini humo.
Lakini walikamatwa mara moja baada ya kuondoka gerezani. Jumatatu jioni, Bw Ssegirinya alivutwa kutoka ndani ya gari la wakili wake nje ya gereza la Kigo prison na maafisa wa usalama waliokuwa na silaha waliokuwa wamevaa mavazi meusi na kumuondosha ndani ya basi dogo aina Toyota Hiace ambalo halikuwa na nambari za usajiri.
Polisi wanasema sasa anakabiliwa na mashitaka mapya ya uhaini na uchochezi wa ghasia. Bw Ssewanyana walikamatwa katika mazingira kama hayo siku tano zilizopita.
Wote walitiwa nguvuni mapema mwezi Septemba. Spika wa Bunge la Uganda Jacob Oulanyah aliitaka ufafanuzi juu ya mazingira ambayo wabunge hao wawili wa upinzani walikamatwa tena.
Waziri Mkuu Robinah Nabbanja aliliambia bunge kwamba Bw Ssewanyana alikuwa tayari amekwishahojiwa akiwa pamoja nawakili wake huku Bw Ssegirinya akitarajiwa kuhojiwa akiwa pamoja na wake karibuni.
WHO yasikitishwa na madai ya unyanyasaji wa ngono wa wafanyakazi wake dhidi ya raia DRC

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la Afya Duniani limesema limesikitishwa na madai ya unyanyasaji wa ngono dhidi unaofanywa na wafanyakazi wake nchini DRC wakati wa mlipuko wa Ebola.
Madai hayo ambayo yalikuja , mwaka mmoja baada ya uchunguzi uliofanywa na shirika la habari za masuala ya kibinadamu na taasisi ya Thomson Reuters.
Wanawake wa eneo hilo walidai kunyweshwa pombe, kuviziwa na kulazimishwa kufanya ngono na wawili walipata ujauzito.
Mkurugenzi wa WHO barani Afrika , Matshidiso Moeti ameomba radhi kwa wanawake na wasichana waliopata masaibu hayo kwa mwaka 2018 na 2020 kwasababu hatua kali zitachukuliwa kwa wafanyakazi hao na watumishi wengine wa afya.
Wachunguzi huru wanasema kuwa mfumo umeshindwa na uzembe wa mtu mmoja katika ripoti yao.
Katibu mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema ripoti hiyo inafadhaisha kuisoma.
Aliomba radhi na kuongeza kuwa hataacha kuahidi kuwasaidia waathirika kwa ulinzi na kupata haki yao.
- WHO yataka uchunguzi dhidi ya wafanyakazi wake kuhusu madai ya ngono ufanyike
Wanajeshi wanne wa Rwanda wauawa Msumbiji

Chanzo cha picha, Reuters
Wanajeshi wanne wa Rwanda wameuawa katika operesheni ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wa nchini Msumbiji katika jimbo la Cabo Delgado , kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Rwanda.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rwanda kutangaza majeruhi katika kikosi chake cha wanajeshi 1,000 tangu waanze operesheni nchini Msumbiji.
Wanajeshi wanne wameuawa na 14 wengine wamejeruhiwa vibaya , kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Rwanda.
Haijawekwa wazi ni katika eneo gani haswa la jimbo la Cabo Delgado, ambako wanajeshi wa Rwanda waliuawa.
Jumamosi iliyopita Rais wa Msumbiji na Rais wa Rwanda walikuwa wanawapongeza wanajeshi ambao wamejitoa kupambana na magaidi.
- Mzozo wa Msumbiji: Wanajeshi wa Rwanda waongoza vita dhidi ya wapiganaji Msumbiji
Mshindi wa sumo mara 1000-Hakuho astaafu

Chanzo cha picha, Reuters
Hakuho, ni miongoni mwa nyota wa wacheza mieleka duniani , ameweza kuwa mshindi wa mieleka ya sumo kwa zaidi ya mara 1,000 , na sasa anastaafu.
Hakuho, mwenye umri wa miaka 36, alihamia Japan akiwa anatokea Mongolia akiwa na umri wa miaka 15. Baada ya hapo alikuwa anashinda mchezo wa sumo duniani.
Amekuwa akisumbuliwa na jeraha la goti kwa muda sasa.
Mwanzoni mwa mwaka huu, alikosa kuhudhuria mashindano kadhaa kutoka na hali yake ya jeraha kuwa mbaya.
Mwezi Januari, alilazwa hospitalini baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Hakuho ni mwana mieleka mwenye ushindi mkubwa katika historia ya mchezo wa sumo. Hatua ya yeye kustaafu kucheza mchezo huo , atabakia mchezaji mmoja tu wa ulimwengu wa Sumo katika viwango vya juu nchini Japan, 'Yokozuna'.Hakuho alianza kunga'ara kwa Yokozuna kwa mara ya kwanza ndani ya miaka sita baada ya michuano yake ya mwaka 2001.
Anajulikana kwa mbinu za mashambulizi kadhaa.
Anajulikana kwa kuhamasisha watu wengi kuwa mashabiki wa mchezo huo wa sumo.
Lakini ushindi ulikuwa ukija na gharama zake.
Hakuho alifanyiwa hata upasuaji katika goti lake la kulia mwanzoni mwa mwaka huu.
Mwezi Novemba mwaka jana, alipata angalizo kutoka baraza la Yokozuna kama ataendelea kukosa michuano katika siku zijazo , basi atalazimishwa kujihuzulu.
Mara tu baada ya kupata ushindi wa mashindano ya 45 mwezi Julai mwaka jana, Hakuho alisema katika mahojiano katika shirika la utangazaji la Japan- NHK kuwa hajisikii vizuri.
Na kuongeza kuwa anawaza sana kuhusu kazi anayoweza kufanya siku zijazo.
Hakuho alipata uraia wa Japan mwaka 2019.Hivyo kuruhusiwa kuwa na kutoa mafunzo ya sumo.Hakuho alisema amekuwa akiwafundisha vijana wadogo kupenda mchezo wa sumo.
Ujerumani yamchagua mbunge wa kwanza mwanamke mweusi

Chanzo cha picha, Youtube
Maelezo ya picha, Awet Tesfaiesus Awet Tesfaiesus ambaye ni mbunge wa chama cha Green atakuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika ,kuchaguliwa kuwa mbunge katika bunge la Ujerumani-Bundestag.
Wakili huyo mwenye miaka 47-aligombea Hessen ambalo linahusisha Frankfurt na Kassel ambako anaishi.
Tangu amehitimu chuo kikuu cha Frankfurt mwaka 2006, amekuwa mwanasheria, mara nyingi akiwakilisha kesi za wakimbizi na wanaotafuta makazi, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
Alizaliwa Eritrea, na kuhamia Ujerumani na familia yake akiwa ma umri wa miaka 6 na amekuwa katika mji wa Heidelberg.
Amekuwa mwanachama wa Greens tangu mwaka 2009, alijikita kwenye siasa kufuatia mapigano ya risasi ya Hanua nje tu ya Frankfurt, mwaka 2020 ambapo wanaofuata mrengo wa kulia waliuawa watu 11.
Jina lake, “Awet”, ambalo kwa asili ya lugha yake ya Eritre ina maanisha ushindi- “jina linateta nuru ya kuongoza njia katia methali za Eritrea.
Ataenda Berlin kuwa mbunge wa Bundestage.
Jinsi mchakato wa amani unavyorudishwa nyuma Sudani Kusini

Waangalizi wa mchakato wa kumaliza mapigano nchini Sudani Kusini wametoa angalizo juu ya mgogoro mpya katika eneo la Tambura kaskazini mwa jimbo la Equatoria ,ambapo anaweza kuwa na athari kubwa katika utekelezaji wa makubaliano ya amani.
Wiki iliyopita, Wataalamu wa Umoja wa Mataifa walisema , viongozi wa kisiasa wanawajibika katika mgogoro huu hatari unaoendelea eneo la Tambura , awali eneo hilo lililokuwa na amani zaidi katika nchi nzima.
Wataalamu wamesema hivi karibuni kuwa vurugu kati ya jamii ya Azande na Balanda katika eneo la Tambura zimesababisha watu zaidi ya 100 kufariki. Watu zaidi ya 80,000 wamelazimika kuhama makazi yao na mamia ya watoto wametenganishwa na wazazi wao.
Walisema pia kuwa jeshi la Sudan Kusini na jeshi la upinzani wanahusika katika kuwapa silaha Azande na jamii ya Balanda .
Jenerali Teshome Gemechu Aderie, ambaye ni mkuu wa kamati hiyo ya waangalizi wa machafuko, alisema kundi la Igad wasijihusishe katika kuwapa silaha bali kufanya kazi ya kumaliza mgogoro.
“Kiwango cha ghasia katika eneo la Tambura unasababisha mchakato wa amani kuwa na wasiwasi mkubwa," alisema.
- Mfahamu Dkt. Riek Machar, na imani zake za msituni kwenye mgogoro wa Sudan Kusini
- Miaka 10 ya Uhuru wa Sudani Kusini: Vita mbili kuu na harakati za miongo sita ya kutafuta kujitawala
Mwanaharakati wa mazingira Uganda: Viongozi wa dunia wamepoteza uelekeo
Mwanaharakati wa mazingira nchini Uganda, Vanessa Nakate ametoa hotuba yenye nguvu katika mkutano wa Youth4Climate uliofanyika mji wa Milan, nchini Italia.
Aliwaambia wajumbe wa mkutano kuwa viongozi wa dunia wamepoteza uelekeo na dunia imeharibika.
"Afrika inachagia sehemu ndogo katika uchafuzi wa mazingira lakini inaathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi," alisema.
Bi Nakate aliuliza pia ni nani ataenda kugharamia uharibifu wa mazingira:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mwanaharakati wa Sweeden, Greta Thunberg, alizungumzia na kuwashutumu viongozi wa dunia kwa maneno ambayo yanavutia lakini hayana utekelezaji.
Alimaliza hotuba yake kwa kuhoji "Tunahitaji nini ? Haki katika mabadiliko ya tabia nchi, Lini tunataka mabadiliko hayo? Sasa!"
Karibu vijana 400 wameshiriki mkutano huo na kutuma mawazo yao na mawaziri wa nishati watakutana pia Milan.
Mawazo mazuri yatapelekwa katika mkutano wa Cop26 huko Glasgow mwezi ujao.
Wanasayansi wanasema watu wenye umri wa chini ya miaka 40 wanakabiliana na changamoto ya joto kali, mafuriko na mazao kushindwa kuota.
Kenya yashindwa kutoa chanjo ya Pfizer kwa kukosa sindano inayohitajika

Chanjo ya Pfizer haiwezi kutolewa nchini Kenya kwa sasa ijapokuwa imewasili nchini.
Hii ni baada ya Wizara ya Kenya kuthibitisha kuwa haina sindano inayohitajika kuwezesha uchomaji wa chanjo hiyo.
"Tulikuwa tunatarajia Marekani itutumie sindano ambazo zinatakiwa kutumiwa kutoa kipimo tulichopokea, lakini hawakufanya hivyo, sasa tunasubiri, kama walivyoahidi kufanya hivyo," afisa wa ngazi ya juu katika Wizara ya afya alinukuliwa na vyombo vya habari akisema hilo.
Katika mahojiano ya simu, Dkt Andrew Mulwa, mkurugenzi wa Huduma za Matibabu katika wizara hiyo, alielezea kuwa maafisa wana matumaini kuwa Marekani itatoa sindano zinazohitajika hivi karibuni kabla ya muda wa matumizi wa chanjo hiyo kumalizika.
Sindano hiyo ni tofauti na sindano ya kawaida.
Kenya: Kwa nini wageni wenye asili ya Asia waliotua Nairobi wamezua gumzo mtandaoni?

Chanzo cha picha, BBC/Njoroge Kabakuri
Wakenya wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuhoji idadi kubwa ya wageni kutoka bara Asia walioonekana katika maeneo tofauti jijini Nairobi na viungani mwake.
Baadhi yao wanataka ufafanuzi kwa nini wageni hao wanaonekana kana kwamba wamekwama nchini na wengine wakitaka kujuu iwapo wanaweza kuwa tishio kwa usalama.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Hata hivyo Msemaji wa Serikali Cyrus Oguna amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema wageni hao waliofika kwa makundi makubwa ni watalii wa kimataifa ambao wana hati halali.
"Hao ni watalii nchini kihalali na wengine wanapendelea kusafiri na kukaa kama familia," alisema.

Chanzo cha picha, Peter Njoroge
Ijapokuwa wengine walipewa nafasi katika vituo anuwai jijini Nairobi na Machakos, wengine wanaaminika kuwa wafanyikazi wa kawaida waliokwama baada ya kushindwa kulipa ada ya malazi ambayo walidai kuwa ya gharama kubwa.
Wageni hao walitua nchini wiki chache zilizopita na walikuwa wakisafiri kwenda Saudi Arabia, ambayo imeweka nchi kadhaa za Asia kwenye orodha nyekundu ya COVID-19.
Jeshi nchini Guinea lazuia wanachama wake kushiriki uchaguzi mkuu ujao

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Wanajeshi walichukua madaraka nchini Guinea mnamo 5 Septemba Uongozi wa kijeshi nchini Guinea umewazuia wanachama wake kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao ambao hiyo itaashiria kurudi kwa utawala wa raia.
Hayo yanajiri wakati jeshi lilitangaza siku ya Jumatatu hati ya mpito ambayo ilimthibitisha kiongozi wa jeshi Kanali Mamady Doumbouya kama rais kufuatia mapinduzi ya mapema mwezi huu.
Hati hiyo pia inaangazia serikali inayoongozwa na waziri mkuu wa raia na baraza la kitaifa la mpito ambalo litatumika kama bunge kwa muda.
Baraza hilo litakuwa na wanachama 81 kutoka kwa jamii na itajumuisha viongozi wa biashara ,vyama vya kisiasa, mashirika ya kidini, wanadiplomasia na mashirika ya kitaalamu. Pia wanazuiwa kushiriki uchaguzi wa ngazi ya mikoa na kitaifa.
Karibu asilimia 30 ya wanachama wa baraza hilo lazima wawe wanawake, na itajumuisha rais na makamu wake wawili .
Baraza litaamua juu ya urefu wa kipindi ambacho kitatawala kabla ya uchaguzi kufanywa ili kuanzisha serikali ya kidemokrasia.
Korea Kusini inatathmini 'kupiga marufuku' ulaji mbwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Kitoweo cha nyama ya Mbwa Korea Kusini Rais wa Korea KusisiniMoon Jae-in amegusia uwezekano wa kupiga marufuku ulaji wa nyama mbwa.
Baadhi ya Wakorea hawajakula nyama ya mbwa na nahitaji yake umepungua katika miaka ya hivi karibuni.
Lakini inakadiriwa kuwa hadi mbwa milioni moja huliwa kama kitoweo kila mwaka nchini humo.
Akizungumza wakati alipokutana na waziri mkuu, Bw. Moon alihoji ikiwa muda umewadia 'kupiga' marufuku nyama ya mbwa.
Hii ni mara ya kwanza rais huyo anayejulikana kwa kupenda nyama ya mbwa, kugusia uwezekano wa kupiga marufuku kabisa ulaji mbwa.
Alitoa tamko hilo baada ya kufahamishwa kuhusu mbinu mpya ya kuwalinda wanyama waliotelekezwa nchini humo.
Tayari kuna sheria inayopiga marufuku uchinjaji wa kikatili wa mbwa na paka, lakini ulaji wenyewe haujapigwa marufuku.
Afghanistan: Watumiaji wa mitandao ya kijamii wafuta maelezo yao kwa kuhofia kushambuliwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Kabla ya Taliban kuchukua uongozi nchini Afghanistan mwezi uliopita, kulikuwa na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wenye ushawishi ambao walikuwa wakipinga vikali sera za kundi hilo.
Lakini tangu Agosti 15, Waafghanistan wamekuwa wakifuta picha na ujumbe wao wa zamani mitandaoni - na wengine wameamua kujiondoa kabisa katika mitandao ya kijamii kwa hofu ya kulengwa na vikosi vya Taliban.
Ijapokuwa Taliban ilitangaza msamaha wa jumla kwa Waafghanistan wote ambao hapo awali walipigana nao au walikuwa sehemu ya serikali iliyopita, baadhi ya wale waliokimbia nchi hiyo waliambia BBC kwamba hawaliamini kundi hili.
Kumekuwa na ripoti kutoka sehemu mbali mbali za nchi kwamba wapiganaji wa Taliban wamewaua raia baada ya kutekwa kwa mji mkuu wa Kabul, licha ya ahadi ya viongozi wao.
Wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Taliban Mohammad Yaqoob alitoa ujumbe wa sauti akikiri kwamba kumekuwa na visa kadhaa vya "mauaji ya kulipiza kisasi" dhidi ya raia yanayofanywa na wapiganaji wa kundi hilo. Hakutoa maelezo zaidi au kutaja matukio maalum.
Tamko hilo lilizua hofu ya athari inayoweza kutokana machapisho ya mitandao ya kijamii, licha ya Facebook kuanzisha huduma za ziada kwa watumiaji nchini Afghanistan - pamoja na kuwaruhusu kufunga profaili zao na kudhibiti ufikiaji wa yaliyomo.
BBC ilizungumza na watu wawili, mmoja mjini Kabul na wa pili katika mji mwingine mkubwa wa Afghanistan, ambao walikuwa na mamilioni ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii na ambao walionekana kuwa na ushawishi kabla ya Taliban kuingia madarakani.
Wote wawili wamefuta akaunti zao kwa hofu ya kulengwa. Kutokana na hali ilivyo nchini Afghanistan, majina ya watumiaji waliohojiwa yamebadilishwa katika ripoti yetu.
Korea Kaskazini imerusha kombora jingine, jeshi la korea Kusini limesema

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Matangazo ya runinga ya Korea Kusini wakati kurushwa kwa kombora la hivi punde. Picha ya maktaba Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa mafupi kuelekea pwani yake ya mashariki mapema Jumanne, linasema jeshi la Korea Kusini.
Jaribio hilo lilifanyika wakati balozi wa Korea Kaskazini aliposema katika Umoja wa Mataifa kwamba hakuna mtu anayeweza kuzuia haki ya Pyongyang kujilinda na kujaribu silaha zake.
Mapema mwezi huu Pyongyang ilifanyia majaribio makombora ya masafa marefu.
Lakini siku chache zilizopita Korea Kaskazini ilikuwa imeonyesha nia ya kushiriki mazungumzo na Kusini.
Jeshi la Marekani lilisema katika taarifasiku ya Jumanne kwamba ina taarifa ya kurushwa kwa kombora lakini haikuwa tishio la haraka kwa wafanyikazi wa Merika au washirika wake.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ameamuru Baraza la Kitaifa la Usalama mjini Seoul kuchunguza nia yoyote inayohusiana hatua ya hivi punde ya Pyongyang kujaribu kombora lake pamoja matamshi kutoka kwa dada yake Kim Jong-un, Kim Yo-jong.
Siku kadhaa zilizopita Bi Kim alisema kuwa wako tayari kutathmini pendekezo la Bwana Moon la kutangaza rasmi kumaliza Vita vya Korea, lakini akaongeza kuwa Kusini inahitajika kusitisha "sera zake za uhasama" kwanza.
- Kwanini jaribio la kombora la Korea Kaskazini linaweza kuyatia hofu mataifa mengine?
- Korea Kaskazini yajaribu kombora jipya la masafa marefu lenye uwezo wa kupiga Japan
- Kwa nini Korea Kaskazini inaendelea na jaribio makombora?
Hujambo na karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumanne 28.09.2021.
