Marcus Rashford: Mshambuliaji wa Manchester arejea katika mazoezi kamili

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford ameshiriki katika mazoezi kamiliIjumaa kwa mara ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji wa bega.
Rashford mwenye umri wa miaka 23, ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa England hajacheza mechi yoyote tangu alipokuwa mchezaji wa akiba katika fainali za Euro 2020.
Amekuwa akisumbuliwa na tatizo la bega kwa miezi kadhaa na alifanyiwa upasuaji mwanzoni mwa mwezi Agosti.
"Marcus alifanya mazoezi kamli leo kwa mara ya kwanza na wenzake," amesema meneja Ole Gunnar Solskjaer.
"Kulikuwa na wasiwasi kidogo, lakini alionekana yuko SAWA, jambo lililokuwa zuri ."
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi ya Primia Ligi ya Jumamosi dhidi ya Everton katika Old Trafford , Solskjaer alikosoampangilio wa mechi.
United iliicharaza Villarreal katika Championi Ligi JUmatano usiku lakini itacheza chini ya saa 72 baadaye, huku Manchester City na Liverpool, ambazo zilicheza mechi ya Ulaya Jumanne, zikikutana katika mechi ya Championi Ligi siku ya Jumapili.















