Al-Shabab walitumia $24m kununua silaha mwaka jana - ripoti
Kundi la al-Shabab nchini Somalia lilitumia dola milioni 24 (£18m) mwaka 2021 kununua silaha, kulingana ripoti ya taasisi ua Hiraal lenye makao yake mjini Mogadishu.
Moja kwa moja
Rais Samia azindua Chuo cha Uongozi Tanzania

Chanzo cha picha, Mwananchi
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amefungua ramsi Chuo cha Uongozi kitakachohudumia Tanzania na nchi zingine 6 ya Afrika.
Chuo hicho kipo Kibaha mkoani Pwani na ujenzi wake umegharimu dola za Kimarekani 45 milioni sawa na sh105.7 bilioni.
Akizindua chuo hicho rais Samia amesema ana amini kitakua sehemu muhimu katika kuwaandaa viongozi wenye uzalendo na weledi bila kujali ni wa chama gani. Rais Samia amesema chou hicho ni nguzo ya kimkakati kwa mataifa sita ya Rafiki ya jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa bara la Afrika.Chuo hicho kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Julius Nyerere kimejengwa kwa ufadhili wa chama cha kikomunisti cha China.Azimio la kujengwa kwa chuo hiki lilikuwa ni baina ya vyama rafiki vya ANC, CCM, FRELIMO, SWAPO, MPLA na ZANUPF na kitakuwa na uwezo wa kuhudumia watu zaidi ya 200 kwa wakati mmoja.
Kampeni ya mtandao kuzuia wamasai kuondolewa Ngorongoro Tanzania yafikisha watu milioni 3

Zaidi watu milioni 3 wamejitokeza kwenye Kampeni ya kupinga kuhamishwa kwa wamasai zaidi ya 70,000 kwenye eneo la Ngorongoro, Kaskazini mwa Tanzania.
Kampeni hiyo inayoongozwa na mtandao wa Avaaz, inahamasisha watu kuweka saini zao kupinga wanaanchi hao kuondolewa na walimuomba Rais wa Tanzania Samia Hassan Suluhu alipokuwa Ubelgiji kuhudhuria Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika uliomalizika hivi karibuni mjini Brussels.
''Kama raia kutoka kote ulimwenguni, tunatoa wito kwenu kupinga jaribio lolote la kuwafurusha Wamasai kutoka katika ardhi yao ya kitamaduni au kuwataka kuhama ili kutoa nafasi kwa wawindaji wa kigeni. Tunakutegemea wewe kuwa bingwa wa watu wako na kukomesha jaribio lolote la kubadilisha haki zao za ardhi kinyume na matakwa yao,'' Ujumbe wa wanaharakati hao kwa Rais Samia ulisema.
Mtandao huo unasema ulipokea ujumbe kutoka kwa viongozi wa wamasai wa eneo hilo, wakiomba msaada wa kutoondolewa.
Wananchi hao jamii ya wamasai wameonyesha wazi msimamo wao kwamba hawataki kuondoka katika eneo hilo ambalo serikali inataka kuboresha shughuli za utalii, sakata lililotua mpaka bungeni.
Baada ya kuibuka mvutano bungeni kuhusu hatua ya kuwaondoa wamasai katika eneo hilo la hifadhi la Ngorongoro, Waziri mkuu alikwenda kuzungumza na wananchi hao na kusema amepokea mawazo yao, na serikali itafanyia kazi ili kuja na mpango bora wa kuboresha eneo hilo, ikiwemo kutenga eneo kwa ajili ya uwindaji na utalii wa wasomi.
Viongozi wa Wamasai wamewasilisha rufaa katika mahakama ya mkoa, wakitaka kusitishwa kwa mipango yote ya eneo hilo na kuitaja jaribio hilo jipya kuwa ni ukiukaji wa wazi wa amri iliyoizuia serikali kuwafurusha watu wa jamii ya Wamasai katika kesi iliyohusisha kufurushwa kwa vurugu.
Hata hivyo Waziri mkuu amesisitiza kwamba serikali ina nia njema, akisema itahakikisha haki za binadamu zinalindwa ikiataka kuona shughuli za ufugaji zikiendelea na utalii ukiendelea kwa namna iliyo bora.
Wadukuzi wauteka tena wavuti wa serikali ya Msumbiji

Chanzo cha picha, Getty Images
Wadukuzi wanasema wamechukua tena udhibiti wa zaidi ya wavuti 30 nchini Msumbiji, baada ya seriklia kusema ilizuwia shambulio hilo Jumatatu.
Kikundi kinachoitwa “Yemeni Hackers” kilisema kuwa kilikuwa nyuma ya shambulio la hivi karibuni.
Wadukuzi walisema “waliingilia kabisa ‘’ wizara 34, ikiwemo wizara ya ulinzi.
Wavuti nyingine zilizolengwa ni pamoja na ule wa idara ya taifa ya udhibiti wa majanga, utawala wa barabara na mashirika ya maji, pamoja na wizara ya ulinzina taasisi ya taifa ya usafiri wa nchi kavu.
Wadukuzi walitishia kutoa data za siri iwapo madai yo ya kikombozi hayatatimizwa.
Erminio Jasse, mkuu wa taasisi ya taifa ya Msumbiji ya masuala ya kielekroniki, alisema Jumatatu kuwa hakuna taarifa zilizoibiwa.
Serikali inatarajiwa kutoa taarifa tena kuhusu tukio hilo Jumatano.
Rais Uhuru Kenyatta amuunga mkono rasmi Raila Odinga kumrithi Sagana

Chanzo cha picha, afp
Maelezo ya picha, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga Rais Uhuru Kenyatta amemunga mkono rasmi kinara wa chama cha ODM nchini Kenya Raila Odinga kuwania urais.
Akihutubia mkutano wa wajumbe katika eneo la mlima Kenya, Uhuru ameitaka jamii yake kumuunga mkono Odinga akisema kwamba anaheshimu maslahi ya taifa.
Kiongozi huyo bila kumtaja naibu wake William Ruto amesema kwamba hatakuwa na tatizo naye katika siku za usoni iwapo 'atabadilika'.
''Nawaomba mumuunge mkono Raila Odinga kwasababu anapigania maslahi ya taifa hili. 'Kijana wangu' atakapobadilika tutamfikiria pia naye'', alisema Uhuru.
Hii ni mara ya kwanza rais Uhuru Kenyatta ameiambia jamii yake hadharani kwamba kiongozi huyo wa chama cha ODM ndiye anayempigania kumrithi.
Rais Kenyatta amekuwa akiashiria kumuunga mkono kiongozi huyo wa ODM bila kumtaja moja kwa moja.
Katika Mkutano huo wa tatu wa Sagana, Uhuru alikuwa waziwazi akisema kwamba Raila ndiye bora sio tu kwa Mlima Kenya bali kwa Wakenya kwa jumla.
Rais amesema kwamba ameongeza uchumi wa taifa hili maradufu tangu alipochukua hatamu kutoka kwa rais Mwai Kibaki.
Alisema kwamba kiongozi huyo wa ODM anaelewa kule taifa linakoelekea hivyobasi atakuwa na amani kumpatia uongozi.
Maimuna Said- 'nilijua nitashinda Uspika'

Uthubutu na kupigania ndoto yake ndivyo vimekuwa vikimuongoza Maimuna Said, mwanadada mwenye umri wa miaka 26 kujitosa katika ushindani wa nafasi mbalimbali za uongozi nchini Tanzania.
Hivi karibuni jina lake liligonga vyombo vya habari alipojitokeza kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kijana zaidi miongoni mwa wagombea wengine.
Je nini kilimsukuma na kwanini anatamani kuwa kiongozi, mwandishi wa BBC Munira Hussein ameandaa taarifa hii.
Uefa huenda ikahamisha fainali ya Ligi ya Mabingwa kutoka St Petersburg Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Uefa inakaribia kubadili fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu kutoka St Petersburg kufuatia mzozo wa Ukraine na Urusi.
Urusi imepeleka wanajeshi wake katika majimbo miwili inayodhibitiwa na waasi nchi Ukraine na kuna hofu kwamba uvamizi unapangwa.
Nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Uingereza, zimeweka vikwazo dhidi ya Urusi kujibu hatua hiyo.
Uefa imesema "inafuatilia kwa karibu hali hiyo" na "uamuzi wowote utafanywa kwa wakati unaofaa hali ikiazimu".
Wadukuzi wanadai fidia ili kufungua tovuti za serikali Msumbiji

Chanzo cha picha, Getty Images
Wadukuzi wamepata tena udhibiti wa tovuti zaidi ya 30 za Msumbiji, saa chache baada ya serikali kusema kuwa imezima shambulio la Jumatatu.
Kundi linaloitwa "Yemen Hackers" limedai kuhusika na shambulio hilo la hivi punde.
Baadhi ya tovutizilizolengwa ni pamoja na mamlaka ya usimamizi wa majanga ya kitaifa, mamlaka ya barabara na mashirika ya maji, na wizara ya ulinzi na taasisi ya kitaifa ya usafiri wa nchi kavu.
Wadukuzi hao wameweka ujumbe katika moja ya tovuti wakitaka kikombozi ndani ya saa 24.
"Ikiwa jumla ya dola 20,000 haitahamishwa katika Bitcoin, data ya siri itavujishwa, ikiwa ni pamoja na ile ya Wizara ya Ulinzi na taarifa zote rasmi na barua pepe za siri," ujumbe huo ulisema.
Wadukuzi hao walisema "wamejipenyeza kabisa" katika wizara 34 na kwamba hakuna suluhisho la haraka.
Walisema kuwa serikali imepuuza ukubwa wa shambulio hilo.
Erminio Jasse, mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Serikali ya Kielektroniki ya Msumbiji, siku ya Jumatatu alihakikisha kwamba hakuna taarifa yoyote iliyoibiwa.
Serikali inatarajiwa kutoa sasisho tena Jumatano.
Mwandishi aliyekimbia Uganda awasili Ujerumani - ripoti

Chanzo cha picha, AFP
Mwandishi wa Uganda Kakwenza Rukirabashaija, ambaye alitoroka nchini wiki mbil zilizopita, amewasili Ujerumani, wakili wake ameambia shirik ala habari la AFP.
"Aliwasili Ujerumani asubuhi hii," wakili wake Eron Kiiza, alinukuliwa kusema Jumatano.
Mwanasheria hiyo alitaja hatua hiyo kuwa "unafuu mkubwa ".
Mwandishi huyo aliyeshinda tuzo alilikimbia taifa hilo la Afrika Mashariki baada ya kupewa dhamana na mahakama.
Alikuwa ameomba ruhusa ya kuondoka nchini kutafuta matibabu kutokana na majeraha ambayo anasema aliyapata akiwa kizuizini katika eneo lisilojulikana.
Lakini mahakama ilikataa kumpa mwandishi huyo paspoti yake.
Wakili huyo aliliambia shirika la habari la AFP kwamba mwandishi huyo alikimbia kwa kutembea kwa miguu hadi nchi jirani ya Rwanda na kisha akasafiri hadi nchi ya tatu, ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, lilifanikisha safari yake hadi Ujerumani.
Rukirabashaija alikamatwa mwezi Disemba na kushtakiwa kwa mawasiliano ya kuudhi kwa kutoa matamshi yasiyofurahisha kuhusu Rais Yoweri Museveni na mwanawe kwenye Twitter. Alikanusha mashtaka.
Kesi yake inatarajiwa kuanza Machi 23.
Iran yarudisha chanjo za Corona 'zilizotengenezwa Marekani'

Chanzo cha picha, Reuters
Iran imerudisha dozi 820,000 za chanjo ya virusi vya corona iliyotolewa kama msaada na Poland kwa sababu ilitengenezwa Marekani.
Televisheni ya taifa siku ya Jumatatu ilimnukuu Mohammad Hashemi, afisa wa wizara ya afya, akisema kwamba Poland ilitoa takriban dozi milioni moja za chanjo ya AstraZeneca ya Uingereza na Uswidi kwa Iran.
"Lakini chanjo zilipofika Iran, tuligundua kuwa dozi 820,000 kati ya hizo ambazo ziliagizwa kutoka Poland zilitoka Marekani," alisema.
Waziri wa afya wa Iran, Bahram Einollahi, aliandika katika barua kwa mkuu wa mamlaka ya forodha kwamba licha ya uhakikisho wa Poland,chanjo hizo zilitoka kutoka "chanzo kisichoidhinishwa".
Alisema watoa huduma wa Poland wameahidi "kubadilisha chanjo hizo na zile kutoka kwa chanzo kilichoidhinishwa" na kurudisha chanjo zilizorejeshwa.
Mnamo 2020, Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Hosseini Khamenei, ambaye ndiye mwenye usemi wa mwisho juu ya maswala yote ya serikali, alikataa uwezekano wowote wa chanjo za Marekani au Uingereza kuingia nchini, na kuziita "haramu".
Iran sasa inaagiza tu chanjo za Magharibi ambazo hazijazalishwa Marekani au Uingereza.
Ufadhili wa IMF Somalia mashakani kutokana na kucheleweshwa kwa uchaguzi

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Mpango wa ufadhili wa kijeshi unaweza kuathiriwa na kucheleweshwa wa uchaguzi Shirika la Fedha Duniani (IMF) huenda likasitisha mpango wake wa kuisaidia Somalia katika muda wa miezi mitatu ijayo iwapo uchaguzi uliopangwa utacheleweshawa zaidi.
Mpango muhimu wa ufadhili wa mishahara ya kijeshi pia unaweza kathiriwa.
Mpango wa msamaha wa deni unahitaji kutathminiwa upya ifikapo tarehe 17 Mei na serikali mpya, kulingana na mkuu IMF nchini Somalia, Laura Jaramillo Meya.
Mkataba huo utafanya deni la Somalia kushuka hadi dola milioni 560 (£400m) kutoka dola bilioni 5.2 mwaka 2018.
Awamu ya kwanza ya mpango huo wa mwaka 2020, deni lilipunguzwa hadi dola bilioni 3.7.
Kupunguzwa kwa deni kunatarajiwa kuruhusu nchi kuvutia ufadhili zaidi na misaada kutoka kwa washirika wa kimataifa ili kukuza sekta yake ya kibinafsi.
Uchaguzi nchini Somalia umecheleweshwa kwa muda mrefu - ulikuwa umepangwa kufanyika Novemba 2020, lakini umeahirishwa mara mbili kutokana na kutokubaliana kuhusu namna ya upigaji kura.
Watu 18 wauawa katika shambulio la wanamgambo wa Niger

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Jeshi la Niger limekuwa likipambana na wanamgambo kwa miaka mingi Raia 18 nchini Niger wameuawa katika shambulio la wanamgambo magharibi mwa nchi hiyo, serikali inasema.
Majambazi waliokuwa na pikipiki walivamia lori lililokuwa likisafirisha watu kati ya vijiji viwili vya mkoa wa Tillaberi.
Magharibi mwa Niger - kama vile nchi jirani za Mali na Burkina Faso - kwa miaka mingi imekuwa ikikabiliwa na mashambulio ya wanamgambo, licha ya juhudi za vikosi vya kimataifa vilivyotumwa katika eneo la Sahel kupambana na wanamgambo wa kijihadi.
Majirani wote wawili wa Niger sasa wana serikali za kijeshi baada ya wakuu wa jeshi kuwatimua tawala za kiraia, wakisema wameshindwa kukabiliana na uasi.
Al-Shabab walitumia $24m kununua silaha mwaka jana - ripoti

Chanzo cha picha, Getty Images
Kundi la al-Shabab nchini Somalia lilitumia dola milioni 24(£18m) mwaka 2021 kununua silaha, kulingana ripoti ya taasisi ua Hiraal lenye makao yake mjini Mogadishu.
Ripoti hiyo pia inadai kuwa al-Shabab, ambao wana ufungamano na al-Qaeda, ina kusanya mapato ya karibu dola milioni 180 kila mwaka.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la Al-Shabab’s Arsenal - From Taxes to Terror, inasema kundi hilo linatumia mbinu mbalimbali kupata silaha, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa moja kwa moja kutoka soko la ndani, na kutoka kwa wafanyabiashara wa silaha walio na kandarasi ya kununua na kusambaza silaha kutoka nje ya nchi, hasa Yemen.
Taasisi ya Hiraal pia inasema kwamba waasi wanadhibiti sehemu kubwa ya Somalia na kudumisha kiwango cha ushawishi kwa raia kupitia mchanganyiko wa ushawishi, utawala na kulazimisha.
Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatano 23.02.2022
