Putin hana haja na mazungumzo ya amani,anayatumia kujipanga-Waziri mkuu wa zamani wa Russia
"Nadhani ataendelea kukandamiza na kuongeza uvamizi," alisema Kasyanov, akiongeza kuwa "alikuwa na wasiwasi sana ... kwamba kitu cha kutisha kinaweza kutokea katika uwanja wa vita".
Moja kwa moja
Ripoti za majeruhi wengi kutokana shambulizi la kombora huko Mykolaiv

Chanzo cha picha, Reuters
Tunasikia ripoti za vifo vya watu wengi kufuatia shambulio la kombora kwenye kambi ya jeshi la Ukraine katika mji wa kusini wa Mykolaiv.
Ripoti moja inasema takriban watu 45 wamefariki.
Mwandishi wetu Andrew Harding, huko Odesa, anasema angalau makombora mawili yanaripotiwa kugonga kambi ya jeshi katika viunga vya kaskazini mwa jiji hilo.
Juhudi za uokoaji zinaendelea.
Harding anasema kambi hizo zilikuwa zikitumiwa kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa eneo hilo katika jiji hilo ambalo limekuwa likizuia mashambulizi makubwa ya Urusi kwenye ufuo wa Bahari Nyeusi.
"Mykolaiv imepata wiki za mashambulizi makali ya mabomu, baada ya wanajeshi wa Urusi kusukumwa kutoka mjini," anasema.
"Vikosi vya Urusi basi vilijaribu kupita mji huo kuelekea kaskazini lakini walizuiwa tena na Waukraine.
"Raia wengi tayari wamekimbilia magharibi."
Putin hajatilia maanani mazungumzo ya amani, asema Waziri Mkuu wa zamani wa Urusi

Chanzo cha picha, Reuters
Waziri Mkuu wa zamani wa Urusi, Mikhail Kasyanov, haamini kwamba Rais Vladimir Putin ametilia uzito kuhusu mazungumzo ya amani, na hakuna uwezekano wa kutoa suluhu la mzozo "ambalo litakuwa starehe kwa watu wa Ukraine".
Zaidi ya ahadi ya kutoegemea upande wowote - ambayo ina maana kwamba Ukraine haitoomba kuwa sehemu ya Nato au EU - Kasyanov anaamini Putin atasisitiza "kutambuliwa rasmi" kwamba Crimea ni sehemu ya Urusi.
"Hilo ni muhimu kabisa, Bw Putin ana wazimu kuhusu Crimea," aliambia BBC World News.
Kasyanov - ambaye alikuwa waziri mkuu kati ya 2000-2004 - alisema ana shaka kuwa makubaliano yoyote yatakwama kutokana na mazungumzo ya sasa kati ya pande hizo mbili, akipendekeza ilikuwa tu kuwapa Warusi "muda wa kujipanga upya".
Alisema Putin na washirika wake wa karibu wa kisiasa walikuwa na "wasiwasi" kuhusu kiwango cha vikwazo "vibaya" vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za Magharibi, akipendekeza kiongozi huyo wa Urusi "hakutarajia vikwazo hivyo vingekuwa vikali."
Lakini alisema uamuzi wowote wa kusitisha operesheni za kijeshi nchini Ukraine "utakuwa mwanzo wa mwisho wa [Putin]".
"Nadhani ataendelea kukandamiza na kuongeza uvamizi," alisema Kasyanov, akiongeza kuwa "alikuwa na wasiwasi sana ... kwamba kitu cha kutisha kinaweza kutokea katika uwanja wa vita".
Unaweza pia kusoma:
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
‘Nikirudi Tanzania maisha yangu yatakuwa mikononi mwa rais’-Tundu Lissu
Maelezo ya sauti, ‘Nikirudi Tanzania maisha yangu yatakuwa mikononi mwa rais’-Tundu Lissu Kiongozi wa upinzani wa Tanzania aliye uhamishoni nchini ubelgiji Tundu Lissu amesisitiza kwamba anahitaji kuhakikishiwa usalama wake na rais wa Tanzania Samia Suluhu kabla ya kurejea nyumbani .
Akijibu kauli ya rais Samia aliyoitoa katika mahojiano na BBC kwamba Tundu yuko huru kurejea nyumbani na kuishi kama watanzania wengine ,kiongozi huyo wa upinzani amesema sio jambo la busara kumlinganisha na watanzania wengine kwa sababu hakuna aliyejaribu kuuawa kwa kupigwa risasi 16 au kutishiwa maisha yake kama yeye .
Akizungumza na BBC Swahili ,Lissu amesemahaitakuwa salama kwake kurejea hasa kwa sababu waliojaribu kumuua hawajachukuliwa hatua .
Unaweza kusoma:
MSF yataka majibu kuhusu taarifa za mauaji ya wafanyikazi wake watatu Ethiopia

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la kutoa misaada ya kimatibabu MSF limeitaka serikali ya Ethiopia kujibu taarifa za habari kwamba jeshi lake lilihusika na mauaji ya wafanyakazi wao watatu wa kutoa misaada mwezi Juni mwaka jana.
Ripoti ya uchunguzi ya gazeti la New York Times inadai wafanyakazi wa MSF walipigwa risasi na wanajeshi wa Ethiopia katika eneo la Tigray ambako vita vimekuwa vikiendelea tangu Novemba 2020.
Miili ya María Hernández, Tedros Gebremariam, na Yohannes Halefom iliyokuwa na risasi ilipatikana kando ya barabara katika eneo la Kaskazini la Tigray siku moja tu baada yao kutoweka. Gari lao lililoteketezwa lilikuwa karibu.
Gazeti la New York Times linasema liliwahoji wachunguzi, maafisa wakuu wa Mashirika ya misaada na wanajeshi wa Ethiopia ambao wote walisema watatu hao walipigwa risasi na wanajeshi wa serikali ya Ethiopia kwa amri ya kamanda ambaye alikasirishwa kuwakuta katika eneo la mapigano.
MSF, ambayo imeeleza mauaji hayo kuwa ya makusudi, sasa inaitaka serikali kujibu ripoti ya New York Times. Shirika hilo la kutoa misaada linasema linataka kuelewa mazingira kamili ya mauaji hayo na kuwajibika kikamilifu kwa waliohusika. Serikali ya Ethiopia bado haijajibu madai hayo yaliyochapishwa siku ya Alhamisi.
Fahamu hali ilivyo hadi sasa huko Ukraine kwa muhtasari tu, Hali ilivyo hadi sasa Ukraine
Kiwanda cha ndege chaharibiwa: Urusi imerusha makombora kadhaa karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lviv magharibi mwa Ukraine, na kuharibu mtambo wa karibu wa kutengeneza ndege, kulingana na maafisa wa eneo hilo. Lviv iko karibu na mpaka wa Poland na imekuwa ikichukuliwa kama kimbilio salama kwa maelfu ya wakimbizi.
Miji mingine iliyopigwa makombora: Miji mingi mikubwa pia imekabiliwa na mashambulizi mapya ya angani. Katika mji wa mashariki wa Kharkiv, jengo la chuo kikuu na majengo mawili ya ghorofa yalipigwa makombora, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine 11. Kusini zaidi, huko Kramatorsk, watu wawili waliuawa na sita kujeruhiwa katika shambulio la kombora. Na katika mji mkuu wa Kyiv, mtu mmoja aliuawa baada ya kombora lililorushwa kulipuka katika mtaa wa makazi.
Walionaswa Mariupol wazingirwa: Urusi yasema wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine, kwa usaidizi wa vikosi vyake vyenye silaha, wamezingira na kuzunguka mji wa Mariupol, Ukraine, kusini mwa Ukraine. Makumi ya maelfu ya raia wanasadikiwa kuwa wamenaswa kwenye eneo la maonyesho.
Nusura katika eneo la maonyesho waokolewa: Mkuu wa haki za binadamu wa Ukraine asema kuwa raia wa kwanza waliokuwa wamejihifadhi katika jumba la maonyesho huko Mariupol wamenusurika na kutoka kupitia kwenye vifusi. Kufikia sasa watu 130 wameokolewa, anasema, baada ya shambulio ambalo Ukraine inalaumu Urusi.
Wau milioni mbili wavuka Poland: Mlinzi wa mpaka wa Poland asema zaidi ya wakimbizi milioni mbili kutoka Ukraine wamevuka na kuingia nchini, wengi wao wakiwa wanawake na watoto
Uingereza yazuia RT: Mdhibiti wa utangazaji wa Uingereza Ofcom amefutilia mbali leseni ya chaneli ya TV inayofadhiliwa na serikali ya Urusi RT.
Soma zaidi:
Katika picha: Makombora zaidi huko Kyiv
Hizi ni baadhi ya picha kutoka eneo la mlipuko mpya wa kombora katika mji mkuu wa Kyiv wa Ukraine asubuhi ya leo.
Mtu mmoja aliuawa na wengine 19 kujeruhiwa wakati sehemu za kombora lililoanguka la Urusi lilipotua katika eneo la makazi kaskazini mwa mji huo, mamlaka za mitaa zilisema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Unaweza pia kusoma:
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Vita vya Ukraine: $ 1bn zatolewa kuzuia uhaba wa chakula barani Afrika

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Sudan inaagiza sehemu kubwa ya ngano yake kutoka Urusi na Ukraine Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inapanga kuchangisha $1bn (£759m) katika muda wa wiki moja kusaidia uzalishaji wa kilimo barani Afrika na kulinda bara la Afrika kutokana na uhaba wa chakula unaotokana na uvamizi unaoendelea wa Urusi nchini Ukraine.
Nchi nyingi za Kiafrika zinategemea mataifa hayo mawili yanayopigana kwa usambazaji wao wa nafaka.
Somalia, Benin, Misri na Sudan zinaongoza kwenye orodha ya nchi ambazo zinategemea pakubwa Urusi na Ukraine, huku zaidi ya 70% ya ngano yao ikitoka katika mataifa hayo mawili.
“AfDB inaona ongezeko hili la bei ya ngano, mahindi na maharagwe ya soya kama uwezekano wa kuzidisha uhaba wa chakula na kuongeza mfumuko wa bei,” Rais wa AfDB Akinwumi Adesina alisema.
Mkopeshaji huyo wa kimataifa anasema ataitisha mkutano wa mawaziri wa fedha na kilimo barani Afrika ili kutekeleza mpango huo.
Kupitia mfuko huo, AfDB inalenga kuongeza uzalishaji wa mpunga wa ngano, mahindi na soya kwa kutumia teknolojia zinazostahimili hali ya hewa, zikiwemo aina za mazao zinazostahimili joto na ukame.
Aina ya ngano inayostahimili joto tayari imejaribiwa nchini Sudan na Ethiopia.
Kulingana na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD), angalau mataifa 25 ya Afŕika yanaagiza zaidi ya thuluthi moja ya ngano yao kutoka Russia na Ukrainia.
Kwa hakika, kwa 15 kati yao, sehemu hiyo ni zaidi ya nusu ya matumizi yao ya kila mwaka ya ngano ambayo yanatoka katika mataifa hayo mawili yanayopigana.
Soma zaidi:
Wanajeshi 14,200 wa Urusi wameuawa tangu kuanza kwa vita, Ukraine inasema

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Urusi waendelea kuawa tangu kuanza kwa vita, Ukraine inasema Wanajeshi 14,200 wa Urusi wameuawa tangu kuanza kwa vita, Ukraine inasema
Tunapoingia siku ya 23 ya uvamizi wa Urusi, wizara ya ulinzi ya Ukraine inasema katika taarifa yake ya kila siku kwenye Facebook kwamba takriban wanajeshi 14,200 wa Urusi wameuawa tangu mzozo huo uanze.
Kupata idadi kamili ya majeruhi kwa kila upande kumeonekana kuwa changamoto, huku Urusi na Ukraine zikidai idadi tofauti sana.
Katika taarifa za hivi karibuni mnamo Machi 3, Urusi ilidai kuwa wanajeshi wake 498 waliuawa katika mapigano, lakini imekaa kimya juu ya kuachilia takwimu zaidi tangu wakati huo.
Wakati huo huo, maafisa wa Marekani walisema mnamo Alhamisi idadi ya waathiriwa wa Urusi inaweza kuwa zaidi ya 7,000, hadi 14,000 kujeruhiwa.
Miongoni mwa uharibifu mwingine uliosababishwa dhidi ya silaha na magari ya Urusi ni pamoja na Ukraine kudai kuwa vikosi vyake pia vimeharibu:
- Mizinga 450
- 93 ndege
- helikopta 112
- Na kuharibu mifumo 43 ya kupambana na ndege
Hata hivyo, BBC imeshindwa kuthibitisha madai hayo.
Soma zaidi:
Duterte asema nchi yake haitatuma wanajeshi ikiwa Marekani itajihusisha na vita

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Urusi Vladimir Putin (kulia) akipeana mkono na mwenzake wa Ufilipino Rodrigo Duterte katika mkutano mwaka 2017 Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema hatapeleka wanajeshi wake kupigana nchini Ukraine iwapo Marekani itahusika katika mzozo huo.
Marekani na Ufilipino zina mkataba wa ulinzi wa pande zote mbili ambao unaahidi mataifa yote mawili kusaidiana ikiwa nchi yoyote ingeshambuliwa na mtu wa nje.
"Sitafanya hivyo. Ikiwa Wamarekani watashiriki vita na wako hapa, kwa nini nitume wanajeshi wangu? Sio vita vyetu kupigana,”alisema Duterte katika hotuba yake siku ya Alhamisi.
"Ikiwa vurugu zitaenea na vita kwa namna fulani vifike hapa, hiyo itakuwa ngumu sana. Almuradi imi ndio Rais, sitamtuma hata mwanajeshi wangu mmoja kwenda vitani,” aliongeza.
Baada ya kuingia madarakani katikati ya mwaka 2016, Duterte amechukua hatua za kuimarisha uhusiano na Moscow, huku akikosoa sera za usalama wa Marekani.
Duterte amekutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mara mbili mjini Moscow.
Katika hotuba ya Alhamisi alimtaja Bw Putin kama “rafiki wa kibinafsi” na siku za nyuma aliripotiwa kumwita kiongozi huyo wa Urusi kama “sanamu” lake.
Hata hivyo, pia alilinganisha mzozo wa Ukraine na Vita vyake dhidi ya Madawa ya Kulevya, ambayo imeshuhudia maelfu ya washukiwa wa dawa za kulevya wakiuawa wakati wa operesheni za polisi tangu kuanza mwaka wa 2016.
"Putin anaua raia huko,"Duterte alisema, "Niliua tu wahalifu kwa sababu ya dawa za kulevya."
Soma:
Ukraine 'imeifedhehesha' Urusi kwenye uwanja wa vita,inawaua wanajeshi wake wengi na kuharibu zana zao

Chanzo cha picha, Getty Images
Ukraine "inaidhalilisha" Urusi kwenye uwanja wa vita anasema mtaalam wa kijeshi wa Uingereza.
Prof Michael Clarke, mkurugenzi wa zamani wa Taasisi ya Huduma ya Kifalme ya Muungano (RUSI) anasema: "Warusi wanafanya karibu kila makosa vitani ambayo yanawezekana kufanyika."
Akiongea kwenye kipindi cha Leo cha Radio 4 cha BBC, anaeleza: "Wao [wanajeshi wa Urusi] wanaonekana kama vikosi ambavyo havikuwa tayari kabisa, ambavyo havikuwa vimefikiria jinsi kampeni kuu inavyoweza kuwa.
"Waukraine wanazuia hatua za Urusi katika maeneo yote na hata wanaendesha mashambulizi ya kukabiliana kwa sasa yenye ufanisi. Warusi wanapoteza vifaa na wanajeshi wengi."
Prof Clarke anasema Ukraine ina mfumo wa amri na udhibiti wa uwanja wa vita kama wa "Nato’uliojengwa kwa usaidizi kutoka nchi za Nato tangu 2014.
Shambulio la kiwanda cha kutengeneza ndege huko Lviv asubuhi ya leo linaweka wazi "Warusi wanaenda kutafuta miundombinu ambayo inaweka ndege za Kiukreni angani", anasema.
Kushambulia mji wa magharibi kilomita 70 tu kutoka mpaka wa Poland pia ni "jaribio la kuzitia hofu nchi za Magharibi kutokana na kuwasaidia Waukraine kama vile wamekuwa," anaongeza.
Unaweza pia kusoma:
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Mataifa ya Afrika hayawezi kuendelea kutounga mkono upande wowote katika vita vya Ukraine

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Takriban watu milioni tatu wamekimbia makazi yao kutokana na vita hivyo, kulingana na Umoja wa Mataifa Takriban watu milioni tatu wamekimbia makazi yao kutokana na vita hivyo, kulingana na Umoja wa Mataifa
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema mataifa ya Afrika hayawezi kubaki kutounga mkono upande wowote katika vita vya Ukraine.
Akizungumza na BBC, Linda Thomas-Greenfield alibainisha kuwa katika kura iliyopigwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu wiki mbili zilizopita kuonesha kuchukia uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, nchi 17 za Afrika - nusu ya dunia nzima - zilijizuia na nyingine nane hazikupiga kura kabisa.
Balozi huyo alisema hakuwezi kuwa na msingi kwenye kutoegemea upande wowote, na kwamba mgogoro huu haukuwa tu mashindano ya Vita Baridi kati ya nchi za Magharibi na Urusi.
Bi Thomas-Greenfield alisema Marekani ilikuwa ikisaidia kutafuta vyanzo mbadala vya bidhaa ambazo nchi huagiza kutoka Urusi.
Mwanadiplomasia huyo pia alisema Marekani itaunga mkono pendekezo la Afrika Kusini la kupatanisha Urusi na Ukraine.
Angalia zaidi:
Mkimbizi wa zamani atoa mchango wa mahindi kwa Waukraine

Chanzo cha picha, Adrien Nimpagaritse
Maelezo ya picha, Adrien Nimpagaritse alikua na kwenda shule katika kambi ya wakimbizi nchini Tanzania Mkulima mdogo nchini Burundi, ambaye zamani alikuwa mkimbizi, anatoa 100kg (220lb) za zao la mahindi kama mchango kwa wale wanaokimbia ghasia nchini Ukraine.
“Mimi mwenyewe nikiwa mkimbizi hapo awali, nilifikiria kutoa msaada.
Mimi ni mkulima mdogo, sina mengi ya kutoa lakini nina moyo wa upendo,” Adrien Nimpagaritse aliambia BBC.
“Kuzitazama picha hizo, niliona wanawake na watoto wakifariki dunia.
Sina sauti ya kuchangia katika kuleta suluhu la mzozo huo, lakini naweza kuchangia baadhi ya kile nilicholima kama ishara ya upendo.”
Bw. Nimpagaritse alikuwa yatima mwenye umri wa miaka minne alipokimbilia Tanzania wakati wa wimbi la ghasia za kikabila mwaka wa 1996.
Alilelewa katika kambi ya wakimbizi ya Mutenderi, ambako alisoma shuleni, na alirejea nyumbani Burundi baada ya miaka 11 mwaka 2007, akiwa na umri wa miaka karibu miaka 15.
“Niliona jinsi kuwa mkimbizi kulivyo - hatukuweza kupata chakula,” alisema.
“Iwapo mtu, jirani, angekupa jani la muhogo tu na maji ungeshukuru sana.”

Chanzo cha picha, Adrien Nimpagaritse
Maelezo ya picha, Adrien Nimpagaritse sasa amerejea Burundi, ambako ameoa na ana watoto watatu Bw Nimpagaritse sasa anaishi katika jimbo la Ruyigi mashariki mwa Burundi, ambako ameoa na ana watoto watatu.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 alimtaka mtu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kuja kuchukua mchango wake wa mahindi kwa ajili ya Ukraine.
“Ningehimiza pia mtu yeyote aliye na moyo kama huo kusaidia vivyo hivyo - inaweza kusaidia karibu familia 20.
“Binafsi ninaweza kumudu kutoa kilo 100 za mahindi, haitoshi, kwa hivyo, ikiwa mtu mwingine ataongeza zaidi, itasaidia."
Soma zaidi:
Mzozo wa Ukraine: Afisa wa China akutana na balozi wa Urusi nchini China

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais wa China na yule wa Urusi Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya China alikutana na balozi wa Urusi nchini China siku ya Alhamisi ili kubadilishana mawazo kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili, kilisema chombo cha habari cha Reuters kikinukuu wizara ya mambo ya nje ya China.
Cheng Guoping, Kamishna wa Mambo ya Nje na Masuala ya Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, alikutana na Andrey Denisov wa Urusi na kubadilishana mawazo kuhusu ushirikiano wa pande hizo mbili dhidi ya ugaidi na usalama, ilisema ripoti hiyo.
Mkutano huo unakuja huku kukiwa na hofu kwamba Beijing itakubali ombi la Urusi kutoa msaada wa kijeshi katika uvamizi wake nchini Ukraine.
Marekani imeonya kuwa "haitasita kuitoza gharama kubwa " China ikiwa itaisaidia Urusi moja kwa moja na zana za kijeshi.
Wanajeshi wa Urusi hawana 'vitu muhimu kama vile chakula na mafuta' - Uingereza

Chanzo cha picha, PA
Maelezo ya picha, MOD Vikosi vya Urusi vinajitahidi kudumisha mashambulizi yao nchini Ukraine, kulingana na tathmini ya hivi punde ya kijasusi kutoka Wizara ya Ulinzi ya Uingereza.
"Matatizo ya kimkakati yanaendelea kukumba uvamizi unaodorora wa Urusi nchini Ukraine," ripoti hiyo inasema.
Wanajeshi hawajaweza kuwapa wanajeshi wao walio mstari wa mbele "vitu muhimu kama vile chakula na mafuta," kwa sababu ya kushindwa kupiga hatua za kijeshi na ukosefu wa ubora wa anga.
"Mashambulizi ya Ukraine yasiyoisha yanailazimisha Urusi kugeuza idadi kubwa ya wanajeshi ili kulinda njia zao za usambazaji bidhaa. Hii inapunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kushambulia wa Urusi."
Ripoti hiyo inaangazia tathmini ya Marekani mapema siku ya Alhamisi, ambayo ilisema kwamba wanajeshi wa Urusi "wamehifadhiwa kote nchini".
Habari za hivi punde, Jengo karibu na uwanja wa ndege wa Lviv lashambuliwa: Meya
Meya wa mji wa Lviv amesema kwenye Telegram yake kwamba uwanja wa ndege haukupigwa, lakini jengo karibu na uwanja huo lilishambuliwa
"Kwa hakika sio uwanja wa ndege," aliandika.
Ikiwa imethibitishwa kama shambulio la kombora la Urusi, litakuwa shambulio la karibu zaidi ambalo wametekeleza katika jiji la kihistoria la Lviv tangu vita vilipoanza wiki tatu zilizopita.
Habari za hivi punde, Mzozo wa Ukraine: Wanajeshi wa Urusi wakabiliwa na 'mashambulizi yasioisha'
- Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa wito wa kuporomoka kwa Ukuta wa Berlin huku akiwataka wabunge wa Ujerumani "kubomoa" aina mpya ya ukuta unaogawanya Ulaya kati ya uhuru na ukandamizaji.
- Mwenzake wa Urusi Vladimir Putin alitoa matakwa yake ya makubaliano ya amani na Ukraine katika mazungumzo ya simu na kiongozi wa Uturuki
- Urusi ilisema haitatoa azimio la kibinadamu kwa ajili ya kura ya Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa kama ilivyopanga, na kuishutumu Marekani kwa kuyashinikiza mataifa kutoiunga mkono.
- Maafisa wa ulinzi nchini Marekani na Uingereza wanasema vikosi vya Urusi havijapiga hatua yoyote ya hivi karibuni katika eneo hilo, na huenda vinapambana na matatizo ya motisha na vifaa.
- Makombora yalirushwa Kharkiv, jiji la pili kwa ukubwa nchini Ukraine, lakini vikosi vya eneo hilo viliyakabili mashambulizi hayo
- Mamlaka za eneo hilo zimesema kuwa mji wa kusini-mashariki wa Mariupol bado unakabiliwa na mashambulizi makali ya vikosi vya Urusi, na karibu watu 30,000 wameutoroka.
- Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kumuonya mwenzake wa China Xi Jinping kuhusu wito baadaye Ijumaa kwamba China itakabiliwa na "gharama kubwa" ikiwa itaiokoa Urusi kutoka kwa vikwazo vya Magharibi.
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja
