Takriban watu 1000 wauawa katika tetemeko la ardhi Afghanistan
Afisa wa serikali ya eneo hilo aliambia BBC kwamba idadi ya waliofariki zaidi ya 1000 huenda ikaongezeka, na kwamba wengine zaidi ya 600 wamejeruhiwa.
Moja kwa moja
Jina la kampuni ya Kijapani lilivyozua taharuki mitandaoni

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakenya wengi mtandaoni na wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kwingineko wanaelezea mshtuko wao na wakizua mjadala kuhusu jina la kampuni mpya ya Naomi Osaka iliyozinduliwa.
Jina la kampuni ya vyombo vya habari lenye maana ''hana sehemu za siri'' kwa kiswahili ambayo Osaka amezindua kwa ushirikiano na bingwa mara nne wa NBA LeBron James - imezua taharuki na imekuwa ikivuma kwenye mtandao waTwitter.
Neno hilo kwa kawaida si la staha kutamkwa hadharani kwa maana ya Kiswahili.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kituo cha runinga cha Kenya, Citizen, kimeandika kuhusu mada hiyo kikihoji kwa nini Wakenya wamekuwa wakijadili kwa kiasi kikubwa mtandaoni.
Kampuni ya utayarishaji imesema itakuwa ikitengeneza hadithi ambazo "ni maalum kitamaduni lakini za ulimwengu kwa watazamaji wote" na zinalenga "kushughulikia masuala muhimu ya jamii".
Jino la shujaa wa uhuru lawasili DR Congo

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Patrice Lumumba aliongoza Congo kupata uhuru Jino la kiongozi wa uhuru wa Congo aliyeuawa Patrice Lumumba limewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kufanyishwa ziara ya nchi yake.
Jino hilo ndio tu mabaki ya waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo, ambaye aliuawa mwaka 1961 na waasi kwa ushirikiano na mamluki wa Ubelgiji na mwili wake kuyeyushwa kwa tindikali.
Ziara ya kwanza ya jino hilo itakuwa ni katika mji aliozaliwa, uliopewa jina la Lumumbaville kwa heshima yake, kisha Kisangani, ambako alianzisha harakati zake za kisiasa, na kisha Lubumbashi, ambako aliuawa.
Jeneza lenye jino hilo hatimaye litazikwa katika mji mkuu Kinshasa, mkesha wa Siku ya Uhuru Alhamisi ijayo.
Watu wanne wafariki dunia na wengine 132 kujeruhiwa kwenye ajali ya treni Tanzania

Chanzo cha picha, Mtandao wa Twitter
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 132 kujeruhiwa kwenye ajali ya treni iliyotokea Tabora, Magharibi mwa Tanzania, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limethibitisha.
Taarifa kutoka TRC zinasema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 5 za asubuhi leo ambapo mabehewa nane yaliyokuwa na jumla ya abiria 930 yalianguka katika eneo la Malolo.
Katika taarifa hiyo, ilieleza kuwa majeruhi wamefikishwa katika hospitali ya Mkoa ya Kitete kwaaajili ya matibabu huku manusura wakitafutiwa utaratibu wa kumalizia safari zao.
Hata hivyo waliodhibitika ni watoto wawili, mmoja wa kiume na mmoja wa kike. Sambamba na hao wamefariki watu wazima wawili mmoja akiwa ni mwanamke.
Jeshi la Polisi wameeleza kuwa wanaendelea na uchunguzi wa chanzo cha ajili hiyo.
Matukio ya ajali za treni yametokea mara kadhaa ambapo mwanzoni mwa mwaka huu, treni iliyokuwa ikisafiri Arusha kwenda Dar es Salaam ilipata ajali katika eneo la Pangani, Tanga na kusababisha kifo cha mmoja na majeruhi watano.
Mwaka jana, ajali nyingine ilitokea Bahi- Dodoma ambapo watu watatu walipoteza maisha na wengine 66 kujeruhiwa.
Ikumbukwe mwaka 2002, abiria 280 walipoteza maisha kwenye ajali iliyokea Dodoma.
Sadio Mane: Bayern Munich yamsajili mshambuliaji wa kutoka Liverpool kwa £35m

Chanzo cha picha, Bayern munich
Sadio Mane amekamilisha uhamisho wa £35m kutoka Liverpool kwenda Bayern Munich kwa mkataba wa miaka mitatu.
The Reds watapokea euro 32m (£27.4m) na nyongeza ya euro 6m kulingana na mechi, pamoja na euro 3m kwa mafanikio ya kibinafsi na ya timu.
Liverpool walikataa ofa mbili kutoka kwa Bayern kabla ya kukubali ada ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Senegal, ambaye alikuwa kwenye kandarasi hadi msimu ujao wa joto.
"Huu ni wakati mwafaka kwa changamoto hii," alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
"Nilipendezwa na klabu hii kubwa tangu mwanzo hivyo hakukuwa na shaka akilini mwangu."
Mane alijiunga na Liverpool kwa pauni milioni 34 kutoka Southampton mnamo Juni 2016, na alifunga mabao 120 katika michezo 269, akimaliza msimu uliopita akiwa na mabao 23 katika mashindano yote.
"Sadio Mane ni nyota wa ulimwengu ambaye anaivutia FC Bayern na kuongeza mvuto wa Bundesliga nzima," rais wa Bayern Herbert Hainer alisema. "Ni kwa wanasoka wa kipekee kama huyu ambapo mashabiki huja kwenye viwanja."
Mane aliisaidia Liverpool kushinda Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu, na Februari alifunga penalti ya ushindi huku Senegal ikishinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza.
Unaweza kusoma zaidi
Tetemeko la ardhi la Afghanistan: Watu 1,000 wauawa na wengine 1,500 kujeruhiwa - afisa asema
Maelezo ya video, Tazama: Watu waliojeruhiwa katika tetemeko la ardhi wanakimbizwa kwenye helikopta ya uokoaji Tetemeko kubwa la ardhi limeua watu elfu moja na kuwaacha mamia ya wengine kujeruhiwa nchini Afghanistan, afisa wa Taliban ameambia BBC.
Picha zinaonyesha maporomoko ya ardhi na nyumba zilizoharibiwa zilizojengwa kwa udongo mashariki mwa mkoa wa Paktika, ambapo waokoaji wamekuwa wakihangaika kuwatibu majeruhi.
Kiongozi wa Taliban Hibatullah Akhundzada amesema mamia ya nyumba ziliharibiwa na huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.
Ni tetemeko baya zaidi kuwahi kutokea Afghanistan katika kipindi cha miongo miwili.
Mkuu wa habari wa jimbo la Paktika, Mohammad Amin Hazifi, aliambia BBC kuwa watu 1,000 wamefariki huku wengine 1,500 wakijeruhiwa.
Vikosi vya uokoaji bado vinawatafuta wengine waliozikwa chini ya ardhi, aliongeza.
Tetemeko la ardhi lilipiga takriban kilomita 44 kutoka mji wa kusini-mashariki wa Khost muda mfupi baada ya 01:30 saa za huko (21:00 Jumanne GMT), wakati watu wengi walikuwa wamelala nyumbani.
"Kila barabara unayopita, unasikia watu wakiomboleza vifo vya wapendwa wao. Nyumba zimeharibiwa," mwandishi wa habari wa eneo hilo katika jimbo lililoathirika vibaya la Paktika aliambia BBC.
Matetemeko ya ardhi yanaelekea kusababisha uharibifu mkubwa nchini Afghanistan, ambapo makazi katika maeneo mengi ya vijijini hayana utulivu au yamejengwa vibaya.
Mkulima wa eneo hilo Alem Wafa alilia alipoambia BBC kwamba timu rasmi za uokoaji bado hazijafika kijiji cha mbali cha Gyan - mojawapo ya walioathirika zaidi.
"Hakuna wafanyakazi rasmi wa kutoa misaada, lakini watu kutoka miji jirani na vijiji walikuja hapa kuokoa watu. Nilifika asubuhi ya leo, na mimi - mwenyewe - nimepata maiti 40."
Aliendelea: "Wengi wao ni watoto wadogo, wadogo sana. Kuna hospitali hapa. Lakini haiwezi kukabiliana na maafa haya. Haina uwezo."
Soma zaidi:
Mwana mfalme wa Saudia atembelea Uturuki kwa mara ya kwanza tangu mauaji ya Khashoggi

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Recep Tayyip Erdogan akimkumbatia Mwanamfalme Mohammed bin Salman wakati wa ziara yake nchini Saudi Arabia mwezi Aprili. Mwana mfalme wa Saudi Arabia anatarajiwa kuzuru Uturuki kwa mara ya kwanza tangu mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi mwaka 2018 katika ubalozi mdogo wa Istanbul.
Rais Recep Tayyip Erdogan atafanya mazungumzo ya ana kwa ana na Mohammed bin Salman yanayolenga kurekebisha uhusiano ulioharibika.
Bwana Erdogan aliwahi kumshutumu kwa njia isiyo ya moja kwa moja mwana wa mfalme kwa kuwaamuru maajenti wa Saudia kumuua Khashoggi.
Ziara hiyo inajiri huku Uturuki ikitafuta biashara, uwekezaji na usaidizi ili kuisaidia kukabiliana na mzozo wa kiuchumi unaozidi kuwa mbaya.
Pia imefanya kazi kuboresha uhusiano na Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri na Israel baada ya miaka mingi ya mvutano.
Mwana mfalme Mohammed wakati huo huo anataka kumaliza kutengwa kwake kimataifa.
Mpango wa kupeleka watafuta hifadhi Rwanda wapunguza kasi ya wahamiaji Uingereza – afisa

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Mpango wa wa kupeleka watafuta hifadhi Rwanda unakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa makundi ya kampeni Afisa mkuu katika Ofisi ya Mambo ya Ndani ya Uingereza anasema sera ya kuwapeleka wahamiaji Rwanda inaweza kuwa ilipunguza mtiririko wa wahamiaji kuelekea Uingereza.
Matthew Rycroft aliwaambia wabunge kuwa idadi ya wanaovuka ni ya juu ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu - lakini chini ya makadirio ya idara hiyo.
“Tayari kuna uwezekano kuwa matokeo yake yameanza kujitokeza,” Bw Rycroft aliiambia kamati teule ya mambo ya ndani.
Pia alifichua kuwa watu 47 walikuwa wameambiwa wangeondoka kwa ndege ambayo ilipangwa wiki iliyopita - na kisha ikafutwa, wakati changamoto za kisheria zilizuia waomba hifadhi kuondolewa.
Soma zaidi:
Wafanyakazi wa ushuru Kenya 'kuvaa kamera' katika vita dhidi ya rushwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Kamera zitatumiwa kwenye vituo vya mipakani Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) imesema itaanza kutumia kamera zitakazovaliwa na wafanyakazi wake ili kushughulikia wizi wa ushuru na rushwa, mkuu wa KRA amenukuliwa na gazeti la Business Daily la nchini humo.
Kamera hizo zitatumiwa hasa na wafanyikazi wa ndani katika idara ya kodi na wale wa udhibiti wa forodha na mipaka, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa KRA wameshutumiwa kwa kujilimbikizia mali ambazo haziendani na malipo yao.
"Hivi karibuni pia tutahakikisha maafisa wetu wana kamera zilizovaliwa kama hizi unazoziona huko Marekani, ili hatua yoyote watakayochukua irekodiwe na sisi tuione. Ukiizima, pia tutaelewa ni kwa nini unafanya hivyo," Kamishna Mkuu wa KRA Githii Mburu alinukuliwa akisema.
Mwaka jana, mamlaka ya ushuru ilitangaza kuwa inatazama wasifu wa mitandao ya kijamii wa watu waliolengwa ili kulinganisha mtindo wao wa maisha na ulipaji wao wa kodi.
Prince Charles na Camilla wako Rwanda kuhudhuiria mkutano wa Jumuiya ya Madola

Chanzo cha picha, PA Media
Mwanamfalme wa Wales na Duchess wa Cornwall wamewasili Rwanda kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa Jumuiya ya Madola.
Prince Charles anamuwakilisha Malkia, mkuu wa Jumuiya ya Madola, katika hafla hiyo, ambayo iliahirishwa mwaka 2021 na 2020 kwa sababu ya janga la corona.
Safari hiyo inaashiria ziara ya kwanza ya kifalme nchini Rwanda, ambayo ni moja ya mataifa machache ambayo Malkia hajatembelea.
Haya yanajiri baada ya kuripotiwa kuwa mwanamfalme huyo alikosoa kwa siri mpango wa Uingereza wa kutuma waomba hifadhi nchini Rwanda.
Kulingana na madai yaliyoripotiwa na gazeti la Times mapema mwezi huu, mrithi wa kiti cha ufalme alisemekana kuamini kuwa sera hiyo ilikuwa "ya kutisha".
Safari ya kwanza ya ndege iliyopaswa kuchukua waomba hifadhi kutoka Uingereza hadi Rwanda ilisitishwa wiki iliyopita, dakika chache kabla ya ndege kupaa, kufuatia maamuzi ya kisheria ya mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya.
Prince Charles na Camilla waliwasili katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Jumanne usiku na kulakiwa na kikundi kidogo cha watu mashuhuri.
Katika ziara hiyo, mrithi wa kiti cha ufalme atakutana na manusura na wahusika wa mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Mwanaume afungwa jela kwa kumuoa mke wa pili

Chanzo cha picha, Getty Images
Mahakama ya Pakistan imemuhukumu mwanaume kifungo cha miezi sita kwa kuoa mke wa pili bila ruhusa ya mke wa kwanza.
Mke wa mwanaume huyo kwa jina Saqib, Bi Ayesha Bibi, alishinda kesi hiyo, alipodai kuwa kitendo cha mume wake kuoa mke wa pili bila yeye kumpatia ruhusa ya maandishi , kilikuw ani ukiukaji wa sheria ya familia nchini Pakistan.
Jaji ali,muamuru mwanaume huyo kulipa faini ya dola 2,000.
Watetezi wa haki za wanawake wanasema uamuzi huo wa mahakama utawazuwia wanawake kuoa wake zaidi ya mmoja. Pia wanasema kuwa utawajengea uwezo na kuwawezesha wanawake kwernda mahakamani kudai haki yao.
"Inatia moyo kwamba mwanamke aliyenyanyaswa amelipeleka hili mahakamani," alisema Romana Bashir, kuu wa mradi wa amani na maendelea nchini humo. "Uamuazi huu unawapa uwezo wanawake," aliongeza.
Nchini Pakistan wanaume wanaweza kuoa wake wengine, lakini ni lazima waombe idhini kwa mke wa kwanza kabla ya kuoa mke mwingine.
Urusi na Ukraine: Mfumo wa makombora katika kisiwa cha nyoka ulipigwa na Urusi

Chanzo cha picha, Re
Maelezo ya picha, Picha ya setilati ya Kisiwa cha Nyoka Ripoti ya uongozi wa operesheni za vita wa Ukraine imeripoti kuhusu matokeo ya mashambulio ya " kusini" ambapo Kisiwa cha Nyoka kilichopo katika bahari nyeusi kilipigwa kwa makombora.
Kulingana na ripoti hiyo , "mfumo wa kukinga mashambulio ya anga aina ya Pantsir S1, kituo cha uongozaji wa safari za ndege (radar), na zana nyingine za kijeshi vilivyopo kwenye kisiwa hicho vilipigwa kwa kombora."
"Ukusanyaji wa taarifa kamili kuhusu shambulio hilo unaendelea," umesema ujumbe wa uongozi huo uliotumwa kwenye ukurasa wa Facebook.
Urusi ilithibitisha Jumanne kuwa eneo hilo la kisiwa cha nyoka au Zmeiny lilipigwa kwa makombora yake, lakini wizara yake ya ulinzi ilisema vikosi vya Urusi viliharibu silaha za adui vilipofyatua makombora yalke katika Kisiwa cha Nyoka na hakuna hata moja wao aliyelenga shabaha.
Februari 24, t jesh la Urusi lilishambulia eneo la Ukraine na udhibiti waKisiwa cha Zmeiny katika Bahari Nyeusi, kilomita 140 kutoka Odessa.
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Tetemeko la ardhi la Afghanistan: Takriban watu 920 wauawa na 600 kujeruhiwa, maafisa wanasema

Chanzo cha picha, AFGHANISTAN INFORMATION SERVICE
Tetemeko kubwa la ardhi limesababisha vifo vya takriban watu 920 na mamia ya wengine kujeruhiwa nchini Afghanistan, maafisa wa Taliban wamesema.
Picha zinaonyesha maporomoko ya ardhi na nyumba zilizoharibiwa zilizojengwa kwa udongo mashariki mwa mkoa wa Paktika, ambapo waokoaji wanahangaika kuwatibu majeruhi.
Katika maeneo ya mbali, helikopta zimekuwa zikisafirisha waathiriwa hadi hospitalini.
Kiongozi wa Taliban Hibatullah Akhundzada amesema mamia ya nyumba ziliharibiwa na huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.
Naibu waziri wake wa usimamizi wa majanga Sharafuddin Muslim aliambia mkutano wa wanahabari kuwa takriban watu 920 wameuawa na wengine 600 kujeruhiwa.
Tetemeko hilo lilipiga takriban kilomita 44 kutoka mji wa kusini-mashariki wa Khost muda mfupi baada ya 01:30 saa za huko (21:00 Jumanne GMT), wakati watu wengi walikuwa nyumbani, wamelala vitandani mwao.
Matetemeko ya ardhi yanaelekea kusababisha uharibifu mkubwa nchini Afghanistan, ambako kuna maeneo mengi ya vijijini ambako makao hayana utulivu au yamejengwa vibaya.
Maafisa wa Taliban walitoa wito kwa mashirika ya misaada kukimbilia katika maeneo yaliyoathiriwa mashariki mwa taifa hilo.
Miongo kadhaa ya migogoro imefanya kuwa vigumu kwa nchi hiyo masikini kuboresha ulinzi wake dhidi ya matetemeko ya ardhi na majanga mengine ya asili - licha ya jitihada za mashirika ya misaada ya kuimarisha baadhi ya majengo kwa miaka mingi.
Hata kabla ya Taliban kuchukua madaraka, huduma za dharura za Afghanistan ni adimu sana na haziwezi kukabiliana na majanga ya asilikikamilifu- na ndege chache na helikopta zinapatikana kwa waokoaji.
Zelensky: Hali ni ngumu katika jimbo la Luhansk

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Zelensky akiwa eneo la Mykolaiv, kusini mwa Ukraine tarehe 18 Juni , 2022 Mapigano katika jimbo la Ukraine Lugansk kwasasa ni mazito, amesema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, kupitia ujumbe wa video..
"Hali katika eneo la mapigano haijabadilika. Kwa usaidizi wa vikosi vya kimkakati, jeshi la Ukraine linaimarisha ulinzi katika jimbo laLuhansk – hali kusema ukweli ni ngumu pale kwa sasa. Wavamiziwanaweka shirikizo kubwa kuelekea Donetsk n," Zelensky alisema.
Kulingana na kiongozi huyo wa Ukraine, katika jimbo la Kharkiv, vikosi vya Warusi vinafyatua makombora mengi.
"Wamejitahidi kwa kila njia yoyote kuwazuwia wavamizi, lakini jeshi la Urusi halielewi chochote. Linafanya uharibifu tu - kwa njia hii inaonyesha makamanda wake hawana msimamo," alisem rais wa Ukraine.
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Rais wa Malawi amvua naibu mamlaka juu ya ufisadi

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amemvua makamu wake Saulos Chilima mamlaka yote aliyokabidhiwa baada ya kutajwa katika kashfa ya ufisadi ya $150m (£123m) iliyohusisha kandarasi za serikali.
Makamu wa rais bado hajajibu tuhuma hizo.
Ripoti ya Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (ACB) iliwataja maafisa 53 wa sasa na wa zamani kuwa walipokea pesa kutoka kwa mfanyabiashara kutoka Uingereza na Malawi Zuneth Sattar kati ya 2017 na 2021, rais alisema.
Hii ni kuhusiana na kandarasi 16 ambazo Huduma ya Polisi ya Malawi na Jeshi la Ulinzi la Malawi zilitoa kwa kampuni tano za Bw Sattar.
Maafisa waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na makamu wa rais na mkuu wa polisi - ambaye amefutwa kazi.
Lakini sheria ya Malawi hairuhusu rais kumfukuza kazi au kumsimamisha kazi makamu wake kwa vile rais huyo ni afisa aliyechaguliwa.
"Kila bora ninachoweza kufanya kwa sasa, ambacho nimeamua kufanya, ni kunyima afisi yake majukumu yoyote aliyokabidhiwa huku nikisubiri ofisi ithibitishe madai dhidi yake," rais alisema katika hotuba ya kitaifa Jumanne.
Bw Chakwera aliungana na Bw Chilima kumshinda Peter Mutharika katika uchaguzi wa urais wa 2020. Wawili hao walikuwa wameahidi kupambana na ufisadi serikalini.
Shaye Moss: 'Sitaki mtu yeyote ajue jina langu'

Chanzo cha picha, Getty Images
Mfanyikazi wa zamani wa uchaguzi wa Marekani ambaye alitajwa na washirika wa Trump katika madai yao ya udanganyifu katika uchaguzi ametoa ushahidi kwa wabunge wanaochunguza ghasia za jengo la bunge Capitol.
"Iligeuza maisha yangu juu chini," alisema Shaye Moss, na kuongeza kwamba amepokea vitisho vingi vya kuuawa tangu uchaguzi wa rais wa 2020.
Mwezi mmoja baada ya Trump kushindwa katika uchaguzi, mama na binti yake walitawala machoni pa watu baada ya wakili wa kampeni ya Trump kutoa video ya CCTV ikimuonyesha Bi Moss akionekana kukabidhiwa kitu na mamake.
Vyombo vya habari na wasaidizi wa Trump walianza kubishana kwamba video iliyohaririwa ilionyesha mpango haramu wa kuingiza kura 18,000 za uwongo zinazomuunga mkono Biden kwenye mashine za uchaguzi za kuhesabu kura.
Katika siku ya nne ya usikilizwaji wa kesi hiyo, jopo hilo lilisikiliza kutoka kwa Warepublican ambao Trump aliwashinikiza kubatilisha kura hiyo.
Yeye na mama yake, ambaye pia ni mfanyakazi wa zamani wa uchaguzi, walisema sasa wanaishi kwa hofu.
"Sifanyi chochote tena. Sitaki kwenda popote. Pili nadhani kila kitu ninachofanya. Kimeathiri maisha yangu kwa kiasi kikubwa katika kila nyanja. Yote kwa sababu ya uwongo," Moss aliendelea.
Yeye, pamoja na mama yake, Ruby Freeman, walifanya kazi siku ya uchaguzi kuhesabu kura huko Atlanta kwa Kaunti ya Fulton.
Burkina Faso: Kiongozi wa kijeshi akutana na rais aliyepinduliwa

Chanzo cha picha, Reuters
Katika hali ya kushangaza kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso amekutana na rais aliyempindua katika mapinduzi Januari iliyopita. Roch Marc Christian Kabore aliandamana na rais mwingine wa zamani Jean-Baptiste Ouedraogo.
Maafisa walisema mkutano huo ulionyesha hamu ya Luteni Kanali Paul-Henri Damiba ya kutaka maridhiano na kwamba hali ya usalama wa nchi ilijadiliwa.
Video ya mkutano huo inaonyesha wawili hao wakisaliamana na hata kutabasamu huku kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso akimkaribisha mtu aliyemtoa madarakani kwa matembezi kwenye zulia jekundu mahali anapopafahamu vyema - ikulu ya rais. Taarifa ilisema Roch Marc Christian Kabore alikuwepo kujadili masuala ya usalama na kujaribu kutuliza joto la kisiasa.
Mnano mwezi Januari Luteni Kanali Paul-Henri Damiba alisema alimuondoa madarakani rais Kabore kwa sababu alishindwa kuzuia mashambulizi ya wapiganaji wa kijihadi. Licha ya ahadi ya kuimarisha usalama, ghasia zimeendelea. Kiongozi huyo wa kijeshi pia ametangaza kwa utata kipindi cha mpito cha miaka mitatu kabla ya uchaguzi.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo Jumatano tarehe 22 Juni 2022
