Muogeleaji wa Marekani Anita Alvarez aokolewa na kocha wake baada ya kuzirai katika bwawa la kuogolea
Mwanamichezo muuogeleaji wa Marekani Anita Alvarez alilazimika kuokolewa na kocha wake baada ya kupoteza fahamu na kuzama kwenye bwawa (swimming pool) kwenye Mashindano ya Dunia ya Aquatics.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 25 hakuwa anapumua na alikuwa amezama baada ya kukamilisha mzunguko wake wa kwanza wa kuogelea katika fainali ya bila malipo akiwa peke yake mjini Budapest.
Kocha wake, Andrea Fuentes, aliijitupa kwenye maji na kumvuta Alvarez hadi juu kabla ya kuchukuliwa kwa machela kwa ajili ya matibanbu. Timu ya kuogelea ya Marekani baadaye ilitoa taarifa ikisema Alvarez "anajisikia vizuri sasa".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Alvarez aliwahi kuzimia pia hapo mwaka jana akifanya mazoezi ya kufuzu kwa Olimpiki mjini Barcelona, ambapo kocha wake Fuentes alimuokoa pia katika tukio hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images












