Mwanaume anayedaiwa kushukiwa kumuua Shinzo Abe azungumza
Mtengenezaji maarufu wa michezo ya sauti na video ametishia kuwashtaki wanaoeneza uvumi wa uongo kuwa yeye ndiye muuaji wa Shinzo Abe.
Moja kwa moja
Bunge la Marekani laitaka Rwanda kumuachilia Paul Rusesabagina

Chanzo cha picha, Getty Images
Bunge la Marekani limeidhinisha azimio linaloitaka Rwanda imuachilie mara moja Paul Rusesabagina kwa ‘sababu za kiutu’.
Mwaka jana, Bw Rusesabagina alihukumiwa kifungo cha miaka miaka 25 na mahakama ya Rwanda baada ya kumpata na hatia ya Rwanda ahamijwe ibyaha birimo iterabwoba.
Februari, 2022, wabunge wawili wa bunge la Marekani; Young Kim wa California na Joaquin Castro wa Texas, waliwasilisha pendekezo la kutaka Bw Rusesabagina aachiliwe bungeni ili liidhinishwe.
Hata hivyo mahakama ya Kigali ilimpata na hatia ikiwa ni pamoja na ya ugaidi kutokana na mashambulio ya mwaka 2018 na 2019 yaliyowauwa watu nchini Rwanda, yaliyotekelezwa na kikundi cha alichokiongozacha uasi cha MRCD/FLN.
Unaweza pia kusoma:
- Rwanda- Paul Rusesabagina akamatwe
- Human Rights Watch: 'Rusesabagina apewe haki ya kujitafutia wakili wake
- Utata juu kukamatwa kwa 'shujaa' wa filamu ya mauaji ya Rwanda.
Mzozo wa Sri Lanka: Waziri mkuu wa Sri Lanka aapishwa kama kaimu Rais

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Watu walijitolea kuwapatia chakula kwa wanajeshi mjini Colombo kusherehekea kuondoka kwa Bw Rajapaksa Waziri Mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe ameapishwa kama kaimu rais huku nchi ikikabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na ghasia.
Anachukua nafasi yaGotabaya Rajapaksa ambaye alikimbilia nchini Singapore baada ya maandamano makubwa ya upinzani ambayo hayakutarajiwa ambapo waandamanaji waliivamia kasri ya rais.
Waandamanaji walikaidi amri ya kutotoka njekuadhimisha kujiuzulu kwake wakati wa usiku.
Sri Lanka inakabiliwa na vurugu ya kiuchumi huku ikikabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula, mafuta na huduma nyingine za kimsingi.
Mchakato wa bunge wa kumchagua rais mpya utaanza Jumamosi, huku wabunge wakiwa na uwezekano mkubwa wa kusongesha kura uchaguzi huo hadi wiki ijayo.
Ikizingatiwa kuwa chama tawala kina wabunge wengi, inadhaniwa kuwa wabunge wanaweza kumuunga mkono Bw Wickremesinghe, ambaye ana uhusiano wa karibu za familia ya Rajapaksa.
Unaweza pia kusoma:
- Sri Lanka: Rais Gotabaya Rajapaksa akimbia nchi kwa ndege ya kijeshi
- Sri Lanka: Waziri Mkuu alitaka jeshi kufanya chochote kurejesha utulivu
- Sri Lanka: Waandamanaji ‘’watakaa ikulu mpaka viongozi waondoke
- Baada ya Rais Rajapaksa kukimbia, Ikulu ya Sri Lanka yageuka kivutio kisicho na mwenyewe cha utalii wa bure kwa Wasrilanka
Pigo kwa Mike Sonko baada ya mahakama ya juu zaidi Kenya kuamua alitolewa ofisini kwa njia ya haki

Chanzo cha picha, MIKE SONKO/FACEBOOK
Mahakama ya Juu nchini Kenya imeamua kwamba aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko aliondolewa afisini kwa haki mnamo Desemba 2020.
Mojawapo ya sifa kuu za mtu kutafuta kiti cha kuchaguliwa ni kwamba mgombeaji lazima awe hajapatikana na hatia ya kutumia vibaya ofisi ya Serikali au ya umma au kukiuka Sura ya Sita ya Katiba.
Hata hivyo, mgombeaji anaweza kuruhusiwa kugombea ikiwa hajamaliza njia zote za kukata rufaa.
Katika kesi ya Sonko, amemaliza njia zote za rufaa, ikizingatiwa kesi yake ya kuondolewa mashtaka iliamuliwa na Mahakama ya Juu zaidi, mnamo Ijumaa, Julai 15.
Sasa ni jukumu la Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutoa uamuziwa iwapo Sonko, ambaye alikuwa wameidhinishwa kugombea kiti cha ugavana katika kaunti ya Mombasa Alhamisi, Julai 14, atagombea au la .
Iwapo tume ya uchaguzi itakubali kugombea kwa Sonko, mwanya huo unaweza kupingwa mahakamani, ikizingatiwa kuwa Sonko sasa amemaliza chaguzi zake zote za rufaa.
Gavana huyo wa zamani wa Nairobi alikuwa ameidhinishwa na Mahakama Kuu ya Mombasa kuwania wadhifa huo.
Sonko anatafuta kumrithi Ali Hassan Joho kama gavana wa pili wa Mombasa.
Marais wa Somalia na Kenya kujadili uhusiano uliozorota baina ya nchi zao

Chanzo cha picha, VILLA SOMALIA
Rais Hassan Sheik Mohamud na mwenyeji wake, Uhuru Kenyatta watajadili jinsi ya kuimarisha mahusiano ya kihistoria na ushirikiano baina ya nchi mbili. Msemaji wa Rais wa Somalia ameiambia BBC kuwa suala la biashara ya miraa (milungi) baina ya nchi hizo litajadiliwa kando.
Ziara hii ya kiongozi wa Somalia inakuja huku kukiwa na ripoti kuwa nchi mbili zinapanga kusaini mkataba wa kufufua mauzo ya miraa nchini Somalia. Somalia ilisitisha ununuzi wa zao hilo mwaka 2020 wakati wa janga la Covid -19 .
Uhusiano baina ya Kenya na Somalia ulizorota sana wakati wa utawala wa rais wa zamani Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Somalia ilipokata uhusiano na Kenya “kuingilia ” masuala yake ya ndani ya nchi. Kenya ilikanusha madai hayo.
Zaidi ya hayo, nchi mbili zimekuwa katika malumbanoya muda mrefu kuhusu umilikiwa eneo la majini lenye utajiri wa mafuta katika eneo la mpaka baina yao. Mwezi Oktoba mwaka jana Mahakama ya kimataifa ya haki ilitoa uamuzi dhidi ya Kenya.
Kadhalika mwezi uliopita, balozi wa Somalia nchini Kenya aliondoka nje ya mkutano katika mji mkuu Nairobi baada ya wanadiploamasia kutoka jimbo lililojitangazi uhuru wake la Somaliland kualikwa . Haijawa wazi iwapo masuala haya yatajadiliwa katika sizara ya siku moja ya rais Hassan Sheik.
Unaweza pia kusoma:
- Kenya yajiondoa katika kusikilizwa kwa mzozo wake wa majini na Somalia
- Je mzozo wa mpaka wa majini baina ya Kenya na Somalia unaelekea kumalizika?
- ICJ yakataa kesi ya Kenya katika mzozo wa mpaka wa baharini na Somalia
Urusi na Ukraine: Muingereza aliyetekwa na wanaotaka kujitenga na Ukraine afariki

Chanzo cha picha, HANDOUT
Muingereza Paul Urey, ambaye alitekwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga wa Ukraine wanaoungwa mkono na Urusi, amefariki katika mahabusu, taarifa zinasema.
Familia ya Urey mwenye umri wa miaka 45 iliwasiliana na Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza kuhusu kifo chake, kulingana naPresidium Network, kikundi cha misaada cha kimekuwa kikiwasaidia ndugu zake.
Mama yake "amefadhaika na bado ana mshituko", kinasema kikundi hicho.
Uingereza inasema inataka ufafanuzi wa haraka kutoka Ukraine na serikali ya Urusi kuhusu taarifa za kifo cha mfanyakazi huyo wa misaada wa Uingereza.
Bw Urey, kutoka Warrington, Cheshirealikamatwa katika jimbo lililojitangazia uhuru wake la Donetsk People's Republic (DPR) mwezi Aprili na anashutumiwa kwa kuwa mamluki.
Alipelekwa jela pamoja na mwanaume mwingine , Dylan Healy, wwakati aliporipotiwa kujaribu kufanya kazi ya uokozi wa kibinadamu tarehe 25 Aprili.
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Jeshi la Togo lajuta kuwauwa vijana wadogo saba bila hatia

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Jeshi la Togo limekuwa katika hali ya tahadhari ya juu kufuatia shambulio la kwanza kabisa la wanamgambo lililosababisha mauaji Jeshi nchini Togo limeelezea kujuta kwa kuwauwa vijana saba wadogo siku ya Jumamosi usiku ambao liliwauwa kimakosa kwa kudhani kuwa walikuwa ni wapiganaji wa jihadi.
Katika taarifa, mkuu wa majeshi wa nchi hiyo, Dadja Maganawe, alisema kuwa kikundi hicho cha vijana kiliuliwa wakati waliposhambuliwa na ndege ua kijeshi wakat iwa ulinzi wa doria wa usiku.
Wahanga wote walikuwa na umri wa kati ya miaka 14 na 18.
Vyombo vya habari katika jimbo la kusini la Savanes viliripoti kuwa vijana hao walikuwa njiani kuelekea nyumbani baada ya kuhudhuria sherehe ya Kiislamu yaEid al-Adha.
Jeshi la Togo limekuw akatika tahadhari ya juu kufuatia shambulio la mauaji la wanamgambo wa jihadi la mwezi Mei, wakati wanajeshi wanane walipouawa karibu na mpaka wa nchi hiyo na Burkina Faso.
Matumaini ya Kenya kuandaa mashindano ya riadha ya dunia 2025 yatoweka

Chanzo cha picha, 2020 Olympic Games (© Getty Images)
Maelezo ya picha, Jasmine Camacho-Quinn alishinda medali ya dhahabu mita 100 na kumshinda Kendra Harrison katika Tokyo Matumaini ya Kenya kupokea mashindano ya raidha ya dunia kwa mara ya kwanza yamefifia baada ya Shirikisho la riadha dunaini kutkangaza kuwa Tokyo itaandaa mashindano hayo mwaka 2025.
Kenya ilikuwa imetangaza nia yake ya kuwa mwenyeji wa mashindano yam waka 2025, lakini Mkuu wa mashindano ya dunian ya riadha-World Athletics, Sebastian Coe katika tangazo lake alitangaza kuwa Tokyo imepata haki za kuwa mwenyeji.
Mji wa Poland wa Silesia na Singapore pia zilikuwa zimewasilisha maombi yake ya kupokea mashindano ya mwaka 2025, lakini mji mkuu wa Japan ambao uliandaa michezo ya Olyimpiki ya mwaka jana ndio ulioibuka na ushindi wa azma hiyo.
Mwanaume aliyeachiliwa kwa mauaji ya Malcolm X aishtaki New York kwa $40m

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Muhammad Aziz alikaa gerezani kwa miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kiongozi wa haki za kiraia Malcolm X. Mwanamume aliyepatikana na hatia kimakosa ya kumuua kiongozi wa haki za kiraia Malcolm X amewasilisha kesi mahakamani kutaka fidia ya dola milioni 40 (pauni milioni 33).
Muhammad Aziz alikaa gerezani kwa miaka 20 kwa mauaji hayo kabla ya kuachiliwa kwa kifungo cha nje mwaka 1985.
Lakini mwaka 2021, waendesha mashitaka waliamua kuachana na hatia yake, wakitaja ‘’ushahidi mpya uliogunduliwa’’.
Bw Aziz, 84, anashtaki kwa mashtaka yenye nia mbaya, kunyimwa haki za mchakato unaostahili na utovu wa nidhamu wa serikali.
Mwanajeshi mkongwe wa jeshi la wanamaji la Marekani, Bw Aziz alikuwa baba wa watoto sita mwenye umri wa miaka 26 alipokamatwa kwa mauaji ya Malcolm X mwaka wa 1965 katika ukumbi wa Audubon Ballroom huko New York.
Kiongozi huyo wa haki za kiraia alipigwa risasi na watu watatu wenye silaha wakati akijiandaa kuhutubia umati wa watu.
Bw Aziz alikamatwa pamoja na Khalil Islam, ambaye aliaga dunia mwaka wa 2009. Bw Islam alitumikia kifungo cha miaka 22 jela kabla ya kuachiliwa kwake.
Soma zaidi:
Vita Ukraine: Eneo la Nikolaev lapigwa makombora
Mkuu wa utawala wa kikanda wa eneo la Nikolaev, Vitaly Kim ameonyesha kupitia video jinsi shambulizi hilo lilivyofanyika.
Kulingana na yeye, roketi karibu 10 zilirushwa katika jiji hilo.
Vyuo vikuu viwili vikubwa jijini pia viliharibiwa.
Meya wa Nikolaev Alexander Senkevich pia aliripoti juu ya shambulio hilo kubwa.
‘’Waokoaji na timu za dharura tayari wapo kwenye maeneo ya tukio. Sasa tunajua kuhusu majeruhi wawili,’’ Senkevich alisema.
Pia unaweza kusoma:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mwanaume anayedaiwa kushukiwa kumuua Shinzo Abe azungumza

Chanzo cha picha, AFP/REUTERS
Mtengenezaji maarufu wa michezo ya sauti na video ametishia kuwashtaki wanaoeneza uvumi wa uongo kuwa yeye ndiye muuaji wa Shinzo Abe.
Hideo Kojima, mvumbuzi na mbunifu wa mchezo wa ‘’Metal Gear’’ amehusishwa na kupigwa risasi kwa waziri mkuu wa zamani wa Japan, na picha zake zimewekwa kwenye tovuti ya 4chan.
Picha hizo zilifuatiwa na mwanasiasa wa Ufaransa, na pia ziliripotiwa na vyombo vya habari nchini Ugiriki na Iran.
Kampuni hiyo inayomilikiwa na fundi huyo, Kojima Productions, ilisema analaani vikali kuchapishwa kwa habari hizo za uongo.
Tovuti ya 4chan ilitumia picha ya Kojima na kwa uwongo ilidai kuwa ‘’mrengo wa kushoto mwenye msimamo mkali’’ na aliwahi kufanya uhalifu hapo awali.
Vyombo vya habari pia viliripoti picha nyingine inayoonyesha kofia ya chuma iliyovaliwa na wanajeshi wa Urusi na nyingine iliyosimama karibu na picha ya Che Guevara, mwanaharakati mwenye itikadi kali.
Soma zaidi:
Alex Murdaugh: Wakili mashuhuri aliyeshtakiwa kwa mauaji ya mke na mwana

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Alex Murdaugh ni sehemu ya familia ya muda mrefu na yenye ushawishi huko South Carolina Wakili mashuhuri wa Marekani ameshtakiwa kwa mauaji ya mkewe na mwanawe, jambo la hivi punde zaidi katika sakata ambayo tayari imemshuhudia Alex Murdaugh akishutumiwa kwa kughushi kifo chake mwenyewe pamoja na makosa kadhaa ya uhalifu.
Maggie Murdaugh, 52, na mwanawe Paul, 22, walipigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yao zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Wakili huyo aliyefedheheka sasa aliripoti kupata miili yao kwenye shamba kubwa la familia huko Carolina Kusini.
‘’Nimeishughulikia sasa,’’ mamlaka inasema Bw Murdaugh aliwaambia wasafirishaji wa polisi katika simu ya 911.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 54 - ambaye tayari yuko jela na anakabiliwa na msururu wa mashtaka ya uhalifu - anakanusha kuhusika na vifo hivyo.
Kulingana na shtaka lililotolewa na baraza kuu la mahakama katika Kaunti ya Colleton ya South Carolina - ambako mauaji yalifanyika - Bw Murdaugh anatuhumiwa kuwaua wawili hao kwa bastola na bunduki.
Pia alishtakiwa kwa makosa mawili ya kupatikana na silaha hatari.
Iwapo atapatikana na hatia, anakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela bila uwezekano wa kuachiliwa huru.
Chini ya sheria za serikali anaweza pia kukabiliwa na adhabu ya kifo.
Soma zaidi:
Muigizaji Nigeria ahukumiwa kwa unyanyasaji kingono dhidi ya watoto

Chanzo cha picha, @OLOFOFOMUSIC
Maelezo ya picha, Olarenwaju James A.K.A Baba Ijesha Muigizaji maarufu nchini Nigeria siku ya Alhamisi amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumdhalilisha kingono mtoto mdogo kati ya 2013 na 2014.
Kesi hiyo imechukua mwaka huku upande wa mashtaka na utetezi wakiwasilisha ushahidi wao kwa nyakati tofauti mwaka jana.
Kulingana na mawandishi wa BBC Rhoda Odhiambo ambaye alikuwa katika mahakama ya Lagos, akiwa amevalia fulana ya manjano na suruali ya jeans nyeusi, Bw Olarenwaju Ominyika almaarufu ‘baba Ijesha’ alisimama kizimbani huku hakimu akimhukumu kifungo gerezani.
Sio tena mtu huru, lakini mfungwa hakimu aliamua kwamba anafaa kutumikia kifungo cha miaka kumi na sita kwa jumla kwa mashtaka manne ambayo alipatikana na hatia.
Lakini kwa vile angetumikia vifungo vyote kwa wakati mmoja, ikawa miaka mitano.
Makosa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia yalitupiliwa mbali kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.
Mwaka jana, Bw Ominyika alikiri kumdhulumu mwathiriwa.
Alisema mama wa mwathiriwa alimpigia simu na kumtaka awe sehemu ya utayarishaji wa filamu, ambapo ataonekana kuwa mwanaharakati wa kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.
Lakini hakimu alisema akiwa mtu mzima mwenye akili timamu, hakupaswa kumdhulumu mtoto, hata kama ni kwa ajili ya kuigiza.
Mwathiriwa na mamake hawakuwa mahakamani wakati uamuzi huo unasomwa.
Wanaharakati wa haki za wanawake na watoto wanasema uamuzi huo utakuwa mfano kwa yeyote anayenuia kumdhulumu mtoto.
Hata hivyo, mawakili wake wanapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Pia unaweza kusoma:
UN inasisitiza kuwa inakabiliana na ubaguzi wa kijinsia huku kukiwa na madai mapya

Maelezo ya picha, Sinead Andrews anasema alitengwa baada ya malalamiko yake Umoja wa Mataifa umesema kuwa unakabiliana na unyanyasaji wa kijinsia, ubaguzi wa kijinsia na utamaduni unaotawaliwa na wanaume ndani ya safu zake za uongozi.
‘’Sote tunajaribu wakati wote kuboresha mfumo,’’ msemaji wa katibu mkuu, Stephane Dujarric, aliambia kipindi cha Newsnight cha BBC.
Zaidi ya wafanyakazi kumi na wawili wa zamani na wa sasa wa Umoja wa Mataifa wameiambia BBC kuhusu chuki dhidi ya wanawake na ‘’hali ya hofu’’ dhidi yao.
Ripoti ya BBC mwezi uliopita ilifichua kufutwa kazi kwa wafanyikazi kadhaa ambao walijaribu kufichua madai ya makosa yanayofanyika.
Filamu hiyo iliyopewa jina la ‘The Whistleblowers: Inside the UN’, ina madai ya kina ya unyanyasaji wa kijinsia, rushwa, chuki dhidi ya wanawake na usimamizi kufumbia macho maovu.
Mshauri Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Sinead Andrews, amejitokeza kuzungumza kwa mara ya kwanza kuhusu hali hiyo.
Anasema ‘alitengwa’ baada ya kutoa malalamiko akiwa katika shirika hilo - madai ambayo Umoja wa Mataifa inakanusha.
Rekodi yake ya utendaji daima imekuwa ‘’yenye nguvu sana’’, aliiambia Newsnight, lakini baada ya ‘’kuzungumza’’ kwa mara ya kwanza, ‘’alianza kusikia maoni’’ kwamba utendakazi wake ‘’pengine ulikuwa unatatizwa’’.
‘’Kile ambacho sikutarajia ni kwamba mfumo ambao ulikusudiwa kunilinda, kama nilivyoripoti, haukuwepo kwa ajili yangu,’’ Bi Andrews alisema.
‘’Na hiyo ndiyo sehemu ya kukatisha tamaa zaidi’’.
Baada ya kuondoka Umoja wa Mataifa, alitoa malalamiko rasmi kuhusu bosi wake wa zamani, Fabrizio Hochschild, ambaye alikuwa chini ya katibu mkuu mjini New York mwaka wa 2019.
Katika barua pepe azilizoonekana na Newsnight, alisema ‘’alikuwa akiwakaripia wenzake mara kwa mara wakati wa mikutano ya timu jambo ambalo lilikuwa likiwadhalilisha na kumfedhehesha yeyote yule aliyelengwa siku hiyo.’’
‘’Pia alizungumza na washirika wengine wakuu wa kike kwa njia ya kuwadhalilisha,’’ aliandika.
Bw Hochschild ‘’alitengwa’’ na Umoja wa Mataifa mwaka jana baada ya uchunguzi wa ndani.
Mara kwa mara amekanusha makosa yoyote na ametaja madai ya Bi Andrews kuwa ya ‘’uongo’’.
Soma zaidi:
Ivana Trump, mke wa kwanza wa Donald Trump afariki dunia

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Donald na Ivan Trump mnamo mwaka 1985 Ivana Trump, mke wa kwanza wa Donald Trump na mama wa watoto watatu, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73.
‘’Alikuwa mwanamke mzuri, mrembo, na wa ajabu, aliyeishi maisha mazuri na ya kutia moyo,’’ Bw Trump alichapisha kwenye mtandao wake wa kijami wa ‘’Truth Social.’’
Bi Trump, ambaye alizaliwa katika nchi ambayo sasa inaitwa Jamhuri ya Czech, aliolewa na rais huyo wa zamani mwaka wa 1977. Walitalikiana miaka 15 baadaye mwaka wa 1992. Walipata watoto watatu pamoja - Donald Jr, Ivanka na Eric Trump.
Polisi wanaamini kuwa sababu ya kifo inaweza kuwa ajali, kulingana na Associated Press.
Vyanzo vya habari vililiambia shirika la habari kwamba Bi Trump alipatikana amepoteza fahamu karibu na ngazi katika nyumba yake ya New York City, na inaaminika kuwa huenda alianguka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ivana Trump, mke wa kwanza wa Donald Trump, afariki dunia Donald na Ivana Trump walikuwa watu mashuhuri kwa umma huko New York katika miaka ya 1980 na 1990, na mgawanyiko wao ulikuwa mada ya maslahi makubwa ya umma.
Baada ya kutengana, Bi Trump aliendelea kuzindua bidhaa za urembo, nguo na vito.
Alichukua sifa kwa kulea watoto wao katika maandishi ya kumbukumbu yake ya 2017 ‘Raising Trump’, akisema ‘’alifanya maamuzi kuhusu elimu yao, shughuli, usafiri, malezi ya watoto na posho yao’’ hadi chuo kikuu.
Katika kitabu hicho, aliongeza kuwa uhusiano wake na Bw Trump umeimarika tangu talaka yao, na akasema alizungumza naye mara moja kwa wiki.
Soma zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja
