Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi atafuta washirika katika safari yake ya Afrika
Bw Lavrov alifanya mazungumzo mjini Cairo na mwenzake wa Misri, Sameh Shoukry.
Moja kwa moja
Vita vya Ukraine: Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi atafuta washirika katika safari yake Afrika

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shokry (kulia) alikutana na Sergei Lavrov siku ya Jumapili Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov ameanza ziara katika nchi za Afrika nchini Misri, akitafuta kuungwa mkono huku kukiwa na hasira juu ya vita vya Ukraine.
Alizilaumu nchi za Magharibi kwa kuihimiza Ukraine kupigana na Urusi ‘’hadi mwisho mchungu’’.
Bw Lavrov alifanya mazungumzo mjini Cairo na mwenzake wa Misri, Sameh Shoukry.
Misri ina uhusiano mkubwa na Urusi, ambayo hutoa ngano, silaha na - hadi uvamizi wa Ukraine ulipoanza – ilikuwa na idadi kubwa ya watalii.
Baada ya mazungumzo yake na Bw Shoukry, Bw Lavrov aliambia mkutano wa pamoja wa wanahabari kwamba nchi za Magharibi zinaendeleza mzozo huo ingawa zinaelewa ‘’nini na mwisho wake utakuwa nini’’.
‘’Hatuna ubaguzi wowote dhidi ya kuanza tena mazungumzo juu ya maswala mapana zaidi, lakini hii haitegemei sisi, kwa sababu mamlaka ya Kiukrene - kuanzia rais hadi washauri wake wengi, wengi - wanasema mara kwa mara kwamba hakutakuwa na mazungumzo hadi Ukraine itashinda Urusi kwenye uwanja wa vita,’’ alisema.
Katika hili, Waukraine wanatiwa moyo kikamilifu na wa Magharibi, iwe London, Washington, Berlin au Umoja wowote wa Ulaya na mji mkuu wa Nato. Kwa hiyo chaguo ni lao".
Ni hatua ya kwanza kwa Bw Lavrov kufanya ziara fupi barani Afrika akichukua Ethiopia, Uganda na Congo-Brazzaville.
Katika makala iliyochapishwa na magazeti ya humu nchini katika maandalizi ya ziara yake, Bw Lavrov alisema nchi yake siku zote ‘’imekuwa ikiwaunga mkono Waafrika kwa dhati katika harakati zao za kupigania uhuru kutoka kwa nira ya ukoloni’’.
Aliongeza kuwa Urusi ilithamini ‘’msimamo’’ wa Waafrika kuhusu suala la Ukraine.
Mataifa mengi ya Afrika yameathiriwa vibaya na uhaba wa nafaka unaosababishwa na vita vya Urusi nchini Ukraine.
Ukraine na Urusi kwa kawaida hutoa zaidi ya 40% ya ngano ya Afrika, Benki ya Maendeleo ya Afrika inasema.
Misri kwa kawaida ni mlaji mkubwa wa ngano ya Ukraine.
Mnamo mwaka wa 2019, iliagiza tani milioni 3.62, zaidi ya nchi yoyote.
Lakini katika makala yake, Bw Lavrov alikanusha shutuma kwamba Urusi ilikuwa ‘’inasambaza njaa’’ na akailaumu kwa propaganda za Magharibi.
Aliongeza kuwa vikwazo vya Magharibi vilivyowekewa Urusi vimezidi ‘’tabia mbaya’’ katika soko la kimataifa la chakula ambalo lilitokana na janga la vorusi vya corona.
Soma zaidi:
Kenya yarejelea mauzo ya mirungi hadi Somalia

Maelezo ya picha, Uuzaji wa mirungi kutoka Kenya hadi Somalia waanza tena Ndege ya kwanza ya mizigo iliyosafirisha shehena ya mirungi hadi Mogadishu ilipaa mapema Jumapili baada ya kupigwa marufuku kwa miaka miwili.
Hii inafuatia kutiwa saini kwa mikataba kadhaa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ikiwa ni pamoja na kuanzisha biashara ya mirungi ambayo pia inajulikana kama miraa.
Katika makubaliano hayo, Somalia itasafirisha samaki na bidhaa nyingine nchini Kenya.
Habari hizi zitakuwa afueni kubwa kwa wafanyabiashara wa miraa nchini Kenya ambao wameathiriwa na kuzorota kwa biashara ya bidhaa hiyo.
‘’Ahadi yetu kama serikali kusaidia wakulima wa miraa na sekta nyingine zote katika kupata fursa za soko za ndani na kimataifa bado ni thabiti,’’ Peter Munya, Waziri wa Kilimo wa Kenya alisema.
Somalia ilipiga marufuku miraa mnamo mwezi Machi 2020 kufuatia uhusiano mbaya wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Marufuku hiyo ilisababisha hasara ya soko la kila siku la zaidi ya tani 50 za mirungi yenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni (dola 169,296.78) wakati huo.
Tangu Rais Hassan Sheikh Mohamud ambaye alichaguliwa tena mwezi Juni baada ya kupigiwa kura mwaka wa 2017
Vita vya Ukraine: Vikosi vya Kyiv vyasonga kuelekea Kherson – Zelensky

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mashambulio ya risasi yameruhusu vikosi vya Kyiv kusonga mbele kuelekea Kherson Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema majeshi yake yanasonga mbele ‘’hatua kwa hatua’’ katika eneo la kusini linalokaliwa la Kherson.
Mji wa Kherson ulitekwa na Urusi mapema katika vita na unakaa kwenye eneo la kimkakati magharibi mwa mto Dnipro.
Siku ya Jumamosi, maafisa wa ulinzi wa Uingereza waliripoti mapigano makali karibu na Kherson.
Hatua hiyo ya mapema ya Ukraine ilimaanisha kuwa njia za usambazaji bidhaa za Urusi magharibi mwa mto zilikuwa ‘’hatarini zaidi’’, kulingana na tathmini yao.
Mapema mwezi huu, Naibu Waziri Mkuu wa Ukrainia Iryna Vereshchuk aliwataka wakaazi wa Kherson kuhama mji huo haraka iwezekanavyo ili kuepuka kunaswa katika jiji hilo wakati wa makabiliano makali Ukraine kusini.
‘’Ni muhimu kufanya hivyo kwa vikosi vya wanajeshi vya Ukraine kutohatarisha raia wakati wa operesheni za kukera,’’ aliiambia TV ya serikali.
Soma zaidi:
Monkeypox: WHO yatangaza tahadhari ya juu zaidi juu ya kuzuka

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Zaidi ya visa 16,000 vya ugonjwa huo sasa zimeripotiwa kutoka nchi 75 Mlipuko wa ugonjwa wa monkeypox umetangazwa kuwa dharura ya kiafya duniani na Shirika la Afya Duniani.
Uainishaji huu ni tahadhari ya juu zaidi ambayo WHO inaweza kutoa kufuatia ongezeko la kimataifa katika visa vya ugonjwa huo.
Hatua hii inawadia mwishoni mwa mkutano wa pili wa kamati ya dharura ya WHO kuhusu virusi.
Zaidi ya visa 16,000 sasa zimeripotiwa kutoka nchi 75, alisema mkurugenzi mkuu wa WHO Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Kulikuwa na vifo vya watu watano hadi sasa kutokana na mlipuko huo, aliongeza.
Kuna dharura zingine mbili tu za kiafya kwa sasa - janga la virusi vya corona na juhudi zinazoendelea za kumaliza ugonjwa wa polio.
Soma zaidi:
Mwanamke wa China ashindwa katika kesi ya kutaka kugandisha mayai

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Bi Xu amesema atakata rufaa Mahakama ya China imetoa uamuzi dhidi ya mwanamke ambaye hajaolewa anayetafuta haki ya kugandisha mayai yake.
Teresa Xu alichukua hatua za kisheria mwaka wa 2019 baada ya Hospitali ya uzazi ya Beijing kukataa kutekeleza utaratibu huo, unaopatikana tu kwa wanawake walioolewa wenye matatizo ya uzazi.
Lakini mahakama iligundua kuwa hospitali hiyo haikukiuka haki zake.
Bibi Xu aliitaja hukumu hiyo kama ‘’kurudisha nyuma’’ haki za uzazi za wanawake, na akaahidi kukata rufaa.
Kulingana na hukumu hiyo hospitali ilisema ‘’lielewa’’ malalamiko lakini ilibidi kufuata sheria.
Wakati Bi Xu alifungua kesi hiyo kwa mara ya kwanza, Chao Wei, msemaji wa hospitali hiyo, alisema wafanyakazi walifuata kanuni za serikali kuhusu teknolojia ya usaidizi wa uzazi, iliripoti New York Times.
Kisha 30, Bi Xu alijaribu kugandisha mayai yake mnamo mwaka 2018 ili kuzingatia zaidi kazi yake kama mhariri wa kujitegemea.
Lakini alisema wafanyikazi wa hospitali walikuwa wamemtia moyo kuwa na mtoto wakati huo badala yah atua hiyo.
Baadaye aliambiwa matibabu hayo yalipatikana tu kwa wanawake ambao hawawezi kupata mimba bila kuingilia kati, shirika la habari la AFP linaripoti.
Hospitali pia ilisema mimba kwa wanawake wazee ni hatari zaidi, na ikabaini changamoto zinazowakabili akina mama wasio na waume.
Soma zaidi:
Je, Afrika inaweza kuwa mshirika wa Ukraine katika vita dhidi ya Urusi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Hatua ya kupinga uvamizi wa Urusi nchini Ukraine katika jiji la Durban, Afrika Kusini, Machi 6, 2022 Urusi kufunga bandari za Ukraine kumesababisha kupanda kwa bei ya nafaka na bidhaa nyingine kadhaa, jambo ambalo limeumiza nchi nyingi za Afrika, kwasababu Ukraine ilikuwa mojawapo ya wasambazaji wakuu wa bidhaa hizo.
Na ingawa maandamano na umasikini tayari kunaonekana kuongezeka barani Afrika kutokana na ongezeko la bei za bidhaa, karibu nusu ya nchi za Kiafrika hazijalaani hadharani uvamizi huo, zinajaribu kuendelea kushirikiana na Urusi, hakuna nchi hata moja iliyounga mkono vikwazo dhidi ya Urusi.
Ukraine inataka kubadili mtazamo huu na kuvutia nchi za Afrika upande wake.
Kwa kuongezea, wanajaribu kununua silaha muhimu kwa vikosi vya wanajeshi barani humo.
Urusi pia inataka kuvutia Afrika upande wake - Julai 24, Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov anaanza ziara ya nchi za bara hilo, na kampuni ya televisheni ya RT hivi karibuni inataka kufungua ofisi ya Afrika ili kuitangaza Urusi.
BBC News Ukraine ilichunguza kwa nini Ukraine iliunga mkono Afrika wakati wa vita, Waafrika wanafikiria nini kuihusu na kama mataifa ya Afrika yako tayari kuunga mkono Waukraine katika vita dhidi ya Urusi.
Kwa nini Ukraine inaunga mkono Afrika?
Mwitikio wa nchi nyingi za Magharibi ulikuwa kuweka vikwazo katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi.
Wakati huo huo, Afrika, Amerika ya Kusini, nchi nyingi za Asia hazikujiunga na vikwazo, ambayo iliruhusu wanasiasa wa Kirusi kusema kwamba wengi wenye ubinadamu wanakataa sera ya Magharibi dhidi ya Urusi.
Mwanzilishi mwenza wa Kituo cha Utafiti wa Afrika, mwalimu wa Taasisi ya Sayansi ya Tiba ya KNU iliyopewa jina la Shevchenko Oleksandr Mishin anasema kwamba kutoegemea upande wowote kwa nchi nyingi kumedhoofisha uwezo wa kumuadhibu haraka mchokozi, na Urusi inajaribu kuchukua nafasi ya Masoko ya Ulaya katika masoko ya ‘’ maeneo yasiyoegemea upande wowote’’, kujiwasilisha yenyewe kama mjenzi mpya wa ulimwengu wa pande nyingi.
‘’Kimsingi, Urusi inaelezea kwa nchi hizi zote hizo kwamba njia ya kupatatikana kwa msingi wa haki wa pande nyingi inategemea vile Ukraine itakavyodhoofishwa na kuuawa kwa Waukraine,’’ Mishin anabainisha.
Soma zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja
