Mgombea wa Urais Waihiga Mwaure asalimu amri

Mgombea wa chama cha Agano Waihiga Mwaure amesalimu amri na kuitaka tume ya Uchaguzi IEBC kumtangaza William Ruto mshindi

Moja kwa moja

  1. Matokeo ya uchaguzi kenya 2022: William Ruto aomba utulivu na amani Kenya

    William Ruto
    Maelezo ya picha, William Ruto

    Kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi mkuu nchini Kenya, mgombea urais William Ruto amehutubia umma siku ya Jumapili.

    Ruto aliwashukuru Wakenya kwa kupiga kura katika uchaguzi huo wakati wa ibada ya kanisa nyumbani kwake Karen iliyohudhuriwa na washirika wake wa kisiasa.

    "Nataka niwashukuru Wakenya wote, milioni kumi na nne waliojitokeza kupiga kura ndio tuwe na kiongozi mwingine wa miaka ijayo," alisema Ruto.

    Kulingana na kiongozi huyo, baada ya Wakenya kupiga kura kumchagua rais wao ajaye, Mungu ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu nani atakuwa kiongozi ajaye wa nchi.

    Ruto pia aliendelea kuwapongeza viongozi kutoka vyama mbalimbali walionyakua viti mbalimbali katika uchaguzi uliokamilika.

    “Tunawapongeza viongozi wote walioshinda hata tunaposubiri kwa amani hatua inayofuata, ili kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi,” aliongeza.

    Wakati huo huo, Ruto aliwataka Wakenya kuwa na subira na IEBC huku shughuli ya kuthibitishwa katika Bomas of Kenya ikiendelea.

  2. Moto Misri: Makumi ya watu wafariki katika kanisa la Coptic

    Moto Misri

    Makumi ya watu wamefariki dunia baada ya moto kuzuka katika kanisa moja nchini Misri, wengi wao wakikandamizwa wakati wa harakati za kujiokoa.

    Maafisa wanasema idadi ya waliofariki ni takriban watu 41, huku makumi ya wengine wakijeruhiwa. Watoto wanaaminika kuwa miongoni mwa waliofariki.

    Moto wa umeme ulizuka huku waumini 5,000 wakikusanyika kwa ajili ya Misa katika kanisa la Coptic Abu Sifin, vyanzo vya usalama viliiambia Reuters. Moto huo ulizuia lango la kuingilia na kusababisha mkanyagano, walisema.

    Huduma za zimamoto zinasema kuwa moto huo umedhibitiwa. Chanzo halisi cha moto huo bado hakijafahamika.

    Hata hivyo, Padre Farid Fahmy, kutoka kanisa lingine la karibu katika kitongoji cha Imbaba, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba ilisababishwa na shoti ya umeme. “Umeme ulikuwa umekatika na walikuwa wakitumia jenereta,” alisema. "Umeme iliporudi, ulisababisha nguvu kuwa kubwa kupita kiasi." Worshippers have been explaining their moments since the blaze ignited.

    Waumini wamekuwa wakielezea matukio yao tangu moto huo kuwaka. "Watu walikuwa wakikusanyika kwenye ghorofa ya tatu na ya nne, na tuliona moshi ukitoka kwenye ghorofa ya pili. Watu walikimbia kushuka ngazi na kuanza kuanguka juu ya kila mmoja," Yasir Munir aliambia Reuters.

    “Kisha tukasikia kishindo na cheche na moto ukitoka dirishani,” alisema na kuongeza kuwa yeye na bintiye walikuwa kwenye ghorofa ya chini na kuweza kunusurika. Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi alitoa "rambirambi zake kwa familia za watu wote ambao wamekubwa na janga hilo wakati wakimuabudu Mola wao katika moja ya nyumba ya ibada".

    Ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema kuwa imetuma timu katika eneo la tukio kuchunguza chanzo cha moto huo. Wakristo wa Coptic ni takriban milioni 10 kati ya watu milioni 103 wa Misri. Copts wanadai wanakabiliwa na ubaguzi na na wao ni sehemu ndogo katika maisha ya umma ya Misri kuliko idadi yao inavyohalalisha.

  3. Raila Odinga atoa wito wa amani huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu Matokeo ya Urais

    Raila Odinga
    Maelezo ya picha, Raila Odinga

    Mgombea wa Urais wa Muungano wa Kenya Raila Odinga amewataka Wakenya kudumisha amani hata wanaposubiri matokeo ya urais kutoka kwa IEBC.

    Raila alimshukuru Mungu kwa amani ambayo imetanda nchini tangu Jumanne, Agosti 9, Wakenya walipoenda kupiga kura kuwachagua viongozi wapya.

    Akizungumza katika Kanisa la ACK St. Francis huko Karen, alikohudhuria ibada ya Jumapili, Raila alisema haikuwa rahisi kwa Azimio kupitia kipindi cha uchaguzi, lakini wanamshukuru Mungu.

  4. Vita vya Ukraine: Zelensky awaonya wanajeshi wa Urusi katika kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia

    Mwanajeshi wa Urusi katika kitu cha kinyuklia
    Maelezo ya picha, Mwanajeshi

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Urusi kwa kutumia "vitisho vya nyuklia" katika kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia - kikubwa zaidi barani Ulaya.

    Urusi iliteka mtambo huo mwezi Machi na imeshutumiwa kwa kuugeuza kuwa kituo chake na kushambulia miji ya karibu.

    Nchi zote mbili zimekua zikilaumiana kwa kuishambulia kwa makombora katika siku za hivi karibuni, na kusababisha UN kutoa tamko juu ya maafa ya nyuklia.

    Rais Zelensky anasema mwanajeshi yeyote wa Urusi ambaye atafyatua risasi kwenye mtambo huo atakuwa "mlengwa maalum". Kituo cha nyuklia sita cha Zaporizhzhia kipo katika jiji la Enerhodar, kwenye ukingo wa Mashariki wa Mto Dnieper Kusini mwa Ukraine. Urusi ilivamia Ukraine Februari 24, na kuuteka mtambo huo ndani ya siku chache.

    Moscow imeweka wafanyikazi wa Kiukreni kuendesha kituo hicho. Umoja wa Mataifa umeonya kwamba kuendelea kwa uhasama karibu na kituo hicho kunaweza kusababisha maafa ya nyuklia yatakayoathiri sehemu kubwa ya Ulaya.

    Hata hivyo Urusi imekanusha mara kwa mara kukitumia kiwanda hicho kwa shughuli nyingine. Inasema ilichukua udhibiti wa mtambo huo kuzuia uvujaji wa vifaa vya mionzi wakati wa mapigano katika eneo hilo.

  5. Bei ya mafuta Kenya haijabadilika - Epra yasema

    Bei za mafuta hazitabadilika hadi Septemba 14, shirika la udhibiti wa mafuta, Epra, limesema katika ya taarifa yake ya hivi karibuni ya kila mwezi.

    Bei hizo pia hazikubadilika mwezi Julai, baada ya kupanda kwa bei ya mafuta kwa Sh9 mwezi Juni.

    Petroli inauzwa Sh159.12, dizeli Sh140 na mafuta taa Sh127.94 jijini Nairobi.

  6. Mgombea wa chama cha Agano Waihiga Mwaure akubali kushindwa .

    Waihiga Mwaure vakubali kushindwa

    Mgombea wa chama cha Agano Waihiga Mwaure amesalimu amri .

    Akizungumza na vyombo vya habari Waihiga amesema kwamba baada ya kipindi kirefu cha kufuatilia matokeo, chama chake cha Agano kimekubali kushindwa.

    Waihiga vilevile ameitaka tume ya uchaguzi ya IEBC kumtangaza naibu wa rais William Ruto kama mshindi wa uchaguzi huu kwasababu vyombo vyote vya habari vimekuwa vikimuonesha akiongoza.

    Vilevile ameitaka tume hiyo kusimama imara na kutokubali kuingiliwa kwa mtokeo hayo ya uchaguzi.

  7. Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Johnson Sakaja ndiye Gavana mpya wa Nairobi

    Mgombea wa UDA Sakaja na mgombea mwenza wake
    Maelezo ya picha, Mgombea wa UDA Sakaja na mgombea mwenza wake

    John Sakaja ameibuka mshindi wa wadhfa wa ugavana wa mji mkuu wa Kenya Nairobi. Bwana Sakaja alimshinda mwenzake wa chama cha Jubilee kutoka Muungano wa Azimio Polycarp Igathe baada ya kujipatia kura 699,392. Bwana Igathe alijipatia kura 573, 516.

    Edwin Sifuna kutoka chama cha ODM alijipatia kura 716,876 na kuidhinishwa kuwa seneta wa jiji la Nairobi baada ya kumshinda mwenzake wa UDA Margeret Wanjiru. Wanjiri alijipatia kura 524,091.

    Kwa upande wa Mwakilishi wa wanawake katika Jiji la Nairobi, mgombea wa chama cha ODM Esther Passaris (ODM) alijipatia kura 698,929dhidi ya mpinzani wake wa karibu Millicent Omanga wa UDA, ambaye alijipatia kura 586,246.

  8. Natumai Hujambo