Vikwazo vya Magharibi vimeshindwa kuitenga Urusi- Putin

Rais Putin amesifu makubaliano mapya na nchi za Asia, Mashariki ya Kati na Amerika Kusini akitaja washirika hao wapya kama wa kutegemewa na kuaminika.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja.

  2. Poland yakanusha tuhuma za ubaguzi wa rangi baada ya raia wa Afrika Kusini kuzuiliwa kwenye ndege

    Ndege

    Poland inasema ubaguzi wa rangi haukuwa sababu ya uamuzi wake wa kuwazuilia walinzi wa rais wa Afrika Kusini na waandishi wa habari kwa zaidi ya saa 24.

    Mzozo huo ulitokea katika uwanja wa ndege wa Chopin wa Warsaw. Ndege hiyo sasa itahifadhiwa hapo hadi Jumapili, msemaji wa uwanja wa ndege aliambia BBC.

    Takriban watu 120 walikuwa wamekwama kwenye ndege hiyo, ambao ilikuwa ikielekea kwenye mkutano wa kilele wa amani nchini Ukraine.

    Baadhi ya abiria sasa wanashuka na kwenda hotelini. Hatua za Poland zimemwacha Rais Cyril Ramaphosa, ambaye alisafiri kivyake kwenda Ukraine, bila baadhi ya maafisa wake wa ulinzi.

    Hatua hiyo ilizua hisia kali kutoka kwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Bw Ramaphosa, Meja Jenerali Wally Rhoode. "Wanatuchelewesha, wanaweka maisha ya rais wetu hatarini," aliwaambia waandishi wa habari

    "Tungelikuwa Kyiv kwa sasa lakini hivi ndivyo walivyoamua kutufanyia. Nataka muone jinsi walivyo wabaguzi." Lakini Poland imepuuzilia mbali madai hayo.

  3. Vikwazo vya Magharibi vimeshindwa kuitenga Urusi- Putin

    Putin

    Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi dhidi ya nchi yake vimeshindwa kuitenga Urusi na badala yake vimepelekea Urusi kutanua mahusiano ya kibiashara na kile alichokitaja masoko yanayoinukia na yakatokuwa na nguvu siku za usoni.

    Akizungumza katika Kongamano la kimataifa la kiuchumi, Bwana Putin amesifu makubaliano mapya na nchi za Asia, Mashariki ya Kati na Amerika Kusini akitaja washirika hao wapya wa kutegemewa na kuaminika.

    Akizungumzia mzozo kati ya nchi yake na Ukraine, Rais huyo wa Urusi amesema hivi karibuni,Ukraine itaishiwa silaha na italazimika kuzitegemea nchi za magharibi akidai kuwa Ukraine imeshindwa kupiga hatua za kijeshi dhidi ya nchi yake na kujigamba kuwa Ukraine haina misuli ya kushindana na nguvu ya jeshi la Urusi.

  4. Urusi 'haijafungia milango' kampuni za kigeni - Putin

    Putin

    Rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa akihutubia katika Kongamano la Kimataifa la Uchumi.

    Putin ameangazia suala la makampuni ya kigeni ambayo yameondoa biashara zao kutoka Urusi.

    Tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake nchini Ukraine Februari mwaka jana, zaidi ya makampuni 1,000 ya kimataifa - ikiwa ni pamoja na McDonald's, PepsiCo, H&M na Adidas - yameacha kufanya kazi nchini humo.

    Akiahutubia huko St Petersburg alisema kwamba Urusi haikuwa "inafunga milango" kwa biashara za ng'ambo ikizingatia kurudi, Kisha akaahidi kuwatnuku wale wanaoendelea na shughuli nchini Urusi akiwataja kama "wetu".

    "Lakini kwa hakika siku zijazo tutakumbuka tabia ya pekee ya baadhi ya washirika hao, Putin aliongeza.

    "Na hakika tutapatia kipaumbele maslahi ya biashara yetu ya ndani."

  5. Katika picha: Viongozi wa Afrika wakipewa maelezo na Wizara ya Ulinzi ya Ukraine

    Viongozi wa Afrika wametembelea St Michael's Square mjini Kyiv, ambako wamepata taarifa kutoka wizara ya ulinzi ya Ukraine.

    b
    b
    South African presidency
  6. 'Makombora ni ujumbe kwa Afrika'- Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine

    RUSSIAN MOD/TASS

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa lugha ya Kiingereza, akisema kwamba makombora hayo yanalenga Kyiv, na ni ujumbe kwa viongozi wa Afrika wanaotembelea Ukraine leo.

    Ujumbe wa Nukuu: Putin 'anajenga kujiamini' kwa kuzindua shambulio kubwa zaidi la kombora dhidi ya Kyiv katika muda wa wiki kadhaa, hasa wakati viongozi wa Afrika walipotembelea mji mkuu wetu.

    Makombora ya Urusi ni ujumbe kwa Afrika: Urusi inataka vita zaidi, sio amani."

    Hapo awali Jeshi la Wanahewa la Ukraine lilituma ujumbe kwenye Telegram kwamba limeharibu makombora sita ya Kinzhal, makombora sita ya cruise ya Kalibr na ndege mbili zisizo na rubani katika shambulio la Urusi la hivi punde huko Kyiv.

    Hakuna taarifa yoyote inayoashiria ikiwa kombora lililorushwa na Urusi huko Kyiv limefikia lengo lake, lakini meya wa mji mkuu wa Ukraine Klitschko aliripoti mlipuko katika wilaya ya Podil mapema leo.

    Maelezo zaidi:

  7. Kikosi cha usalama cha rais wa Afrika Kusini chazuiliwa Poland

    South African President Cyril Ramaphosa arrived in Kiev by train

    Kikosi cha ulinzi wa rais wa Afrika Kusini wamekwama katika ndege nchini Polanda kwa saa kadhaa baada ya mamlaka kuwazuia wao pamoja na waaandhi wa habari walioandamana nao kuendelea na safari kuelekea Ukraine ambako Cyril Ramaphosa anaongoza ujumbe wa amani wa viongozi wa mataifa ya Afrika.

    Ndege ya kukodishwa ya SAA iliyokuwa na watu 120 imeripotiwa kutua katika uwanjawa ndege wa Chopin mjini Warsaw mapema Alhamisi mchana.

    Mkuu wa usalama wa Ramaphosa, Meja Jenerali Wally Rhoode, ilisema serikali ya Poland inahatarisha usalama wa rais kwa kutowaruhusu kuendeklea na safari.

    "Wanatuchelewesha, wanaweka maisha ya rais wetu hatarini," aliwaambia waandishi wa habari. "Kwa sababu tungelikuwa Kyiv kwa sasa lakini wameamua kutufanyia hivi. Nataka mujioneee jinsi walivyo wabaguzi wa rangi."

    Mamlaka ya Poland haijatoa maoni yoyote kuhusiana na sualahilo ambalo limegeuka kuwa mzozo wa kidiplomasia - ingawa haijamzuia Bw Ramaphosa mwenyewe kuelekea Kyiv, ambako aliwasili kwa treni Ijumaa asubuhi.

    Alipokelewa katika mji mkuu wa Ukraine na balozi wa Afrika Kusini na mjumbe maalum wa Ukraine katika Mashariki ya Kati na Afrika, kulingana na urais wa Afrika Kusini.

    Baadaye atasafiri hadi Urusi katika azma ya Afrika ya kusuluhisha mzozo huo.

    Mmoja wa wale ambao bado kwenye ndege katika mji mkuu wa Poland ni mwandishi wa habari wa News24 Pieter du Toit, ambaye alichapisha video siku ya Ijumaa asubuhi akisema walikuwa wamekwama kwenye lami kwa karibu saa 24.

    "Wafanyakazi wa SAA wamekuwa wakifanya kila juhudisana kumsaidia kila mtu kwenye ndege hiyo.

    Hali kwenye ndege hiyo sasa imeanza kufanana na ya kambi ya wakimbizi kwani mahitaji yanapungua," alisema.

    "Kikosi cha usalama ambacho kilipaswa kumlinda rais kwenye ziara yake huko Kyiv bado kiko kwenye ndege."

  8. ICC kuchunguza tuhuma mpya za uhalifu wa kivita nchini DR Congo

    Ghasia zinazohusisha waasi wa M23 nchini DR Congo zimesababisha takriban watu milioni moja kuyahama makazi yao
    Maelezo ya picha, Ghasia zinazohusisha waasi wa M23 nchini DR Congo zimesababisha takriban watu milioni moja kuyahama makazi yao.

    Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai, ICC imesema itachunguza madai ya uhalifu wa kivita unaofanywa na makundi yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Haya yanajiri wiki kadhaa baada ya serikali ya Kongo kutoa rufaa rasmi kwa ICC kuhusu ghasia zilizohusisha waasi wa M23 ambao wamewakimbia takriban watu milioni moja katika jimbo la Kivu Kaskazini.

    Rais Félix Tshisekedi, pamoja na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, wameishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi ambalo lilianzisha tena uasi huko mwishoni mwa 2021.

    Serikali ya Kigali inakanusha hili. Mahakama ya ICC tayari imewatia hatiani viongozi watatu wa zamani wa wanamgambo kutokana na mizozo nchini DR Congo.

    Pia unaweza kusoma:

    • Mzozo wa DRC na Rwanda : M23, majirani na bahati mbaya ya DRC
    • Jumuiya ya Afrika Mashariki, majeshi na mustakabali wa amani DRC
    • Mzozo wa DRC: Je inawezekana kuyamaliza makundi ya wapiganaji Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo?
  9. Richard Branson: Safari ya ndege za anga za juu kuanza mwezi huu

    .

    Kampuni ya utalii ya safari za anga ya juu ya Sir Richard Branson ya Virgin Galactic inasema itazindua safari yake ya kwanza ya kibiashara kabla ya mwisho wa mwezi huu.

    Kampuni hiyo inalenga kuzindua safari hiyo ambayo inaitwa Galactic 01, kutoka 27 Juni hadi 30 Juni.

    Baada ya tangazo kwa wawekezaji, hisa za Virgin Galactic zilipanda zaidi ya 40% katika biashara iliyopanuliwa ya New York.

    Mnamo mwezi Mei, Virgin Orbit - kampuni tofauti ya anga inayomilikiwa na bilionea wa Uingereza - ilifungwa, miezi kadhaa baada ya misheni kushindwa.

    Virgin Galactic alisema safari ya kwanza ya ndege itakuwa ya utafiti wa kisayansi, ikibeba wafanyakazi watatu kutoka Jeshi la Anga la Italia na Baraza la Kitaifa la Utafiti la Italia kufanya utafiti wa microgravity yaani mvutano dhaifu sana katika chombo kinachozunguka.

    Kampuni hiyo ilisema safari yake ya pili ya anga ya juu itafuata mapema Agosti, na inatarajia kuendesha safari za anga za juu za kila mwezi kuanzia wakati huo.

    Inaashiria hatua muhimu kwa kampuni ya Virgin Galactic ambayo imelazimika kushinda mfululizo wa ajali na changamoto za kiufundi.

  10. Raia wa Misri akamtwa kuhusiana na boti ya wahamiaji iliyozama Ugiriki

    Karibu watu 80 wamefariki Nearly 80 na wengine karibu 600 bado hawajapatikana
    Maelezo ya picha, Karibu watu 80 wamefariki Nearly 80 na wengine karibu 600 bado hawajapatikana

    Mamlaka ya Ugiriki imewakamata watu tisa wanaoshukiwa kuwa wasafirishaji haramu kuhusiana na ajali mbaya ya kuzama kwa boti ya wahamiaji siku ya Jumanne.

    Shirika la utangazaji la Ugiriki, ERT, lilisema wote walikuwa raia wa Misri.

    Jamaa za watu waliokuwa kwenye ndege hiyo wamekuwa wakikusanyika katika mji wa bandari wa Kalamata, wakitarajia kupata wanafamilia.

    Zaidi ya watu 100 wameokolewa lakini karibu 80 wamekufa na hadi 600 bado hawajulikani walipo. Kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba karibu watoto 100 wanaweza kuwa miongoni mwao.

  11. Habari za hivi punde, Tahadhari ya uvamizi wa anga yatolewa mjini Kyiv wakati viongozi wa Afrika wakiwasili

    Wakati viongozi wa Afrika wakiwasili katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv kukutana na Zelensky, tahadhari ya uvamizi wa anga imetolewa katika mji huo na eneo hilo.

    Tahadhari hiyo imewadia baada ya jeshi la wanahewa la Ukraine kusema kuwa makombora kadhaa ya Kalibr ya Urusi yamerushwa kutoka Bahari Nyeusi na "yanaelekea kaskazini" mwa Kyiv.

    Mashambulizi ya makombora ya Urusi yaliongezeka wiki hii huko Kyiv, Odesa, na katika mji alikozaliwa Rais Zelensky wa Kryvyi Rih, na kuua watu kadhaa.

    Olexander Scherba, mwanadiplomasia wa Ukraine ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter: "Sasa ving’ora vimesikika. Putin akiwakaribisha viongozi wa Afrika mjini Kyiv."

  12. Rais wa Afrika Kusini awasili Ukraine

    .
    Maelezo ya picha, Ramaphosa alikutana na mjumbe maalum wa Ukraine kwa Afrika na Mashariki ya Kati, Maksym Subhk (kushoto)

    Video iliwekwa kwenye Twitter muda mfupi uliopita ikionyesha Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwasili katika kituo cha reli cha Nemishaeve katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv leo asubuhi.

    Alilakiwa na mjumbe maalum wa Ukraine kwa Afrika na Mashariki ya Kati, Maksym Subhk, pamoja na balozi wa Afrika Kusini nchini Ukraine, Andre Groenewald.

  13. Watengenezaji iPhone Foxconn kujitosa katika magari huku uhusiano kati ya Marekani na China ukizorota

    .
    Maelezo ya picha, Mwenyekiti wa Foxconn na Mkurugenzi Mtendaji Young Liu

    Kampuni ya kutengeneza iPhone Foxconn inaweka dau kubwa kwenye magari yanayotumia umeme na kufikiri upya mahusiano kati ya Marekani na China.

    Katika mahojiano maalum, mwenyekiti na bosi Young Liu aliiambia BBC nini mustakabali wa kampuni hiyo ya Taiwan.

    Alisema hata Foxconn inapohamisha baadhi ya maduka yake ya usambazaji kutoka China, magari ya umeme (EVs) ndiyo yatachochea ukuaji wake katika miongo ijayo.

    Huku mvutano wa Marekani na China ukiendelea kuzorota, Bw Liu alisema, Foxconn lazima ajiandae kwa hali mbaya zaidi iwapo itatokea.

    "Tunatumai amani na utulivu vitakuwa jambo ambalo viongozi wa nchi hizi mbili watazingatia," Bw Liu mwenye umri wa miaka 67 alisema, katika ofisi zake Taipei, mji mkuu wa Taiwan.

    "Lakini kama mfanyabiashara, kama Mkurugenzi Mtendaji, lazima nifikirie juu ya nini cha kufanya ikiwa hali mbaya zaidi itatokea?"

    Matukio hayo yanaweza kujumuisha majaribio ya Beijing kuizuia Taiwan, ambayo inadai kuwa sehemu ya Uchina, au mbaya zaidi, kuvamia kisiwa hicho kinachojitawala.

    Bw Liu alisema "mipango ya mwendelezo wa biashara" ilikuwa tayari inaendelea, na akadokeza kuwa baadhi ya njia za uzalishaji, hasa zile zinazohusishwa na "bidhaa za usalama wa taifa" tayari zinahamishwa kutoka China hadi Mexico na Vietnam.

  14. Video: Tazama mwanamke aliyefufuka kwenye jeneza akipelekwa hospitalini

    Maelezo ya video, Ecuador woman found alive in coffin is taken to hospital

    Mwanamke mwenye umri wa miaka 76 ambaye aliaminika kufariki kutokana na kiharusi huko Babahoyo, Ecuador, aliwashangaza jamaa waliokuwa wakimbadilisha nguo zake kabla ya mazishi yake aliposhusha pumzi.

    Bella Montoya alikuwa kwenye jeneza kwa karibu saa tano kabla ya wanafamilia kugundua kuwa bado yu hai.

    Huduma za dharura ziliitwa kwenye eneo la tukio na Bi Montoya akarudishwa hospitalini, ambako yuko katika chumba mahututi, kulingana na mwanawe.

  15. Wanajeshi wa Ukraine waharibu ndege mbili zisizo na rubani za Iran usiku

    .
    Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa amesimama karibu na ndege isiyo na rubani ya Iran (Picha kutoka maktaba)

    Vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine vimeharibu ndege mbili zisizo na rubani za Shahed za Iran jana usiku, ripoti ya asubuhi imemnukuu Jenerali Mkuu wa Majeshi ya Ukraine.

    Hapo awali, Jeshi la Anga la Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine liliripoti kwamba ndege zisizo na rubani za "Shahed" za Iran zilishambulia mikoa ya Odessa na Nikolaev.

    "Usiku wa leo, Urusi ilianzisha shambulio lingine la anga dhidi ya Ukraine – kwa kutumia ndege aina ya UAV mbili za Iran za aina ya Shahed.

    Ndege zisizo na rubani zote ziliharibiwa na ulinzi wa anga," ujumbe unasema.

    Mkuu wa Wafanyikazi pia aliripoti kuwa katika siku iliyopita kati ya jeshi la Ukraine na Urusi kulikuwa na mapigano 30.

    Hata hivyo, wakati wa vita ni vigumu kwa BBC kuthibitisha taarifa zilizotolewa na maafisa wa pande zinazozozana.

    Pia unaweza kusoma:

  16. Boti ya Kwara iliopinduka Nigeria: Akina mama walifariki wakijaribu kuokoa watoto wao

    .
    Maelezo ya picha, Aisha Mohammed alikuwa anatazamia kuwaoza binti zake

    Miongoni mwa zaidi ya watu 100 waliozama mapema wiki hii wakati mashua ilipopinduka kwenye Mto Niger katikati mwa Nigeria walikuwa wazazi wengi waliokuwa wakijaribu kuwaokoa watoto wao, mtu aliyenusurika aliambia BBC.

    Mohammed Alhassan, mwenye umri wa miaka 22, alikuwa mmoja wa watu wapatao 300 waliokuwa wakisafiri kwa boti ya mbao iliyojaa watu wengi huko Patigi katika Jimbo la Kwara.

    Wengi walikuwa wakirudi kutoka kwenye harusi. Lakini si Bw Alhassan - alikuwa anarudi kutoka sokoni.

    Haonyeshi hisia zozote anaporudi kwenye ukingo wa mto ambako alikuwa amefanikiwa kuogelea hadi salama.

    Lakini anapokumbuka wazazi waliozama na watoto wao, akiwemo dada yake na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka minane, machozi yanamtoka.

    "Wanawake walibaki nyuma wakijaribu kubeba watoto wao - baadhi yao walikuwa na watoto watatu au wanne.

    "Pia kulikuwa na baba ambao walikufa kwa njia hiyo hiyo wakijaribu kuokoa watoto wao," anasema.

    Angejaribu kusaidia kuwaokoa pia, angezama, anasema.

    Kwa hiyo aliogelea hadi mahali usalama, lakini alipofanya hivyo, aliona hali ya kutisha wakati akina mama na baba wakizama pamoja na watoto wao walipokuwa wakijaribu kuwaokoa.

  17. Urusi inashambulia mikoa ya Odessa na Mykolaiv kwa "Shaheds" - Jeshi la anga la Ukraine

    .
    Maelezo ya picha, Ndege ya kijeshi ikiwasubiri wanajeshi wa NATO

    Jeshi la anga la Ukraine linaripoti kwamba maeneo ya Odessa na Nikolaev yalishambuliwa na ndege zisizo na rubani za Shahed kamikaze za Urusi zinazotengenezwa Iran.

    "Ulinzi wa anga unafanya kazi," Jeshi la Wanahewa lilisema katika taarifa.

    Tahadhari ya angani imetangazwa katika mikoa ya Odessa, Kherson, Nikolaev na Luhansk.

    Tahadhari ya uvamizi wa anga pia imetolewa katika maeneo ya Poltava, Chernihiv na Sumy.

  18. Natumai hujambo