'Mnapaswa kunifuata mimi, muache kuitisha familia yangu!’- Uhuru Kenyatta
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema nyumba ya mwanaye wa kiume imevamiwa na watu wasiojulikana Ijumaa jioni, na watu wasiojulikana, waliodai kuwa ni maafisa wa upelelezi (DCI)
Moja kwa moja
'Mnapaswa kunifuata mimi, muache kuitisha familia yangu!’- Uhuru Kenyatta

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema nyumba ya mwanaye wa kiume imevamiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Bw Kenyatta amesema: ‘’nimepigiwa simu na mtoto wangu wa kiume akaniambia kuwa wakati alipokuwa akitaka kutoka nyumbani kwake aliambiwa kuna watu wanaodai kuwa ni maafisa wa upelelezi DCI, waliokuwa ndani ya gari lenye nambari za usajili za Sudan wanaotaka kuzungumza naye’’
Bw Uhuru amesema alimwambia mwanaye asitoke nyumbani kwake na badala yake aliamua kwenda kwa mwanaye kuwaona watu hao.’’ Nilitaka niende niwaulize ni nini wanatafuta kwa mwanangu’’, alisema.
Hata hivyo anasema alipofika alikuta tayari watu hao wameondoka.
Bw Kenyatta amesema ‘'Mnapaswa kunijia mimi, muache kuitisha familia yangu!’’…Msifikirie mnaweza kunitishia, mnaweza kutokubaliana nami …lakini sitaruhusu familia yangu kushambuliwa’’, alisema.
Wiki hii mama yake Uhuru Kenyatta, Mke wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mama Ngina Kenyatta aliondolewa walinzi wake suala lililoibua hisia miongoni mwa Wakenya.
Akizungumzia suala hilo Bw Kenyatta alisema ‘’Usidhani unaweza kumtishia mwanamke mkongwe na wajukuu zake ili kunitisha mimi…Unafahamu nilipo saa 24, njoo nijie mimi’’
Rais William Ruto amekuwa akimshutumu Uhuru Kenyatta kufadhili maandamano ya upinzani nchini yanayoongozwa na kinara wa upinzani Raila Odinga.
Mwanaume auawa kwa tuhuma za kuiba mkate

Chanzo cha picha, BURE EBIMOTIMI
Imegundulika kuwa mwanaume mmoja aliyedungwa kisu na umati wa vijana wengine hadi akafa, kwa tuhuma za kuiba mkate nchini Nigeria, alikuwa na matatizo ya kiakili.
Hii ilithibitishwa na baadhi ya jamaa na majirani wa Ebimotimi Freeborn Opuofoni.
BBC iligundua kuwa haukuwa hata mkate ulioibiwa, bali ilikuwa ni Madiga kulli, aina ya chakula cha unga kinacholiwa katika sehemu ya jimbo la Bayelsa nchini Nigeria.
Madiga ni chakula kinachotengenezwa na waoka mikate wa kienyeji ambacho ni sawa na mkate, lakini ni huwa na ugumu zaidi na watoto na watu wazima huula na siagi au bila kikavu.

Maelezo ya picha, Madiga ni chakula kinachofanana na mkate ambacho Ebimotimi Freeborn alishutumiwa kuiba Ndugu wa karibu wa familia yake, Kenneth Amewuga alisema Freeborn alikuwa na bidii na alihitimu chuo kikuu na matokeo mazuri sana.
Alisema hatahivyo kuwa “marehemu alifahamika mtaani kwake kuwa ni mgonjwa wa akili, ambapo wakati mwingine huwanyang’anya watu simu, si kwa ajili ya kuziuza bali kuzitupa barabarani au kuziharibu”.
Aliongeza kuwa “tabia yake ilimfanya baba yake kuwa na wasiwasi, kabla ya kifo cha chake miaka michache iliyopita.
Tukio hilo liligusa moyo wangu'
Kifo cha Freeborn kilikuwa msiba mkubwa kwa familia yake, ambao waliomboleza msiba wake.
Mmoja wa ndugu zake, Beauty Edisemi Opufoni, aliambia BBC huku akitokwa na machozi kwamba kifo cha kaka yake kiliwasikitisha na kumuacha katika hali ya mshangao, kwa sababu hakuwahi kumletea kifo hapo awali.
Alisema ingawa kaka yake alitumia miaka mitatu hadi minne baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, Mungu hakukusudia apate kazi.
Jeshi la polisi mjini Bayelsa linasema kuwa limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mtu huyo mwenye umri wa miaka 32.
Msemaji wa Polisi wa Bayelsa, SP Asinim Butswat, alitoa taarifa kwamba watu waliokamatwa ni miongoni mwa majambazi waliompiga vijana.
‘Hatutaruhusu polisi kuua watu kiholela,’ asema rais Ruto

Chanzo cha picha, EPA
Rais William Ruto amewaonya maafisa wa polisi dhidi ya mauaji ya kiholela ya waandamanaji wanaoipinga serikali, huku - kwa upande mwingine - pia akisisitiza kwamba kila mtu lazima afuate sheria.
Akizungumza katika ziara yake katika Kaunti ya Murang'a siku ya Ijumaa, Rais amesisitiza kuwa kuwa serikali yake itakabiliana na wale wanaovunja sheria iwe katika maafisa wa usalama au umma kuhusiana na maandamano yanayoendelea kuongozwa na upinzani.
Alirejelea kuhusu ahadi aliyoitoa baada ya kula kiapo cha urais ambapo aliahidi kutokomeza utovu wa nidhamu na kuhakikisha utawala wa sheria unazingatiwa na kuongeza kuwa ataleta utulivu nchini.
Mkuu huyo wa nchi aliongeza kuwa hakuna mtu atakayeruhusiwa kusababisha ghasia, fujo na uharibifu wa mali na kuondoka nazo.
“Hatutaruhusu kuvunja sheria na kuua watu kiholela. Vile vile tulivyosema tutaondoa mauaji ya kiholela ni sawa na jinsi tulivyojitolea kuhakikisha hakuna adhabu. Huwezi kuharibu mali, kusababisha ghasia na machafuko na [usiwajibike] ... hautaweza! Rais Ruto alionya.
“Tunaomba maafisa wetu wa kulinda sheria wawe waangalifu, wasimame na ninataka kupongeza vyombo vyetu vya usalama kwa kuwa na weledi wa jinsi ambavyo vimewashughulikia watu hawa. Wahalifu lazima washughulikiwe kwa uthabiti, na kuhakikisha kuwa kila mtu anaheshimu utawala wa sheria."
Akiwatetea maafisa wa usalama ambao wameshutumiwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, Bw Ruto alisema wanafanya tu kazi yao ya kuhakikisha kuna amani na utulivu.
Mlindalango wa PSG na mkewe washambuliwa na kuporwa Paris

Chanzo cha picha, XAVIER LAINE/POOL/GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Mwezi uliopita Gianluigi Donnarumma akisherehekea ushindi wa taji la PSG akiwa na mshirika wake mjini Paris Mlindalango wa Italia na Paris St-Germain Gianluigi Donnarumma na mwenzake wameshambuliwa na kuibiwa nyumbani kwao mjini Paris.
Wanandoa hao walilengwa na watu kadhaa na kufungwa kwenye nyumba yao katika wilaya ya nane katikati mwa mji mkuu, vyanzo vya polisi vimeambia vyombo vya habari vya Ufaransa.
Wanaripotiwa kutorokea kwenye hoteli iliyo karibu.
Kengele ililia na wafanyakazi wa hoteli waliowaondoa wawili hao na kuwapeleka hospitalini.
"Uchunguzi umefunguliwa kuhusu mashitaka ya wizi wa kutumia silaha katika genge lililopangwa na ghasia zilizokithiri kufuatia matukio yaliyotokea usiku wa kuamkia leo mahali pa Bw Donnarumma," msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris aliambia BBC.
Ripoti ambazo hazijathibitishwa kwenye tovuti ya habari ya Actu17 zinasema washambuliaji waliondoka na vito, saa na bidhaa za ngozi za kifahari zenye thamani ya takriban €500,000 (£430,000).
Mwanasoka huyo alijeruhiwa kidogo huku mpenzi wake, mwanamitindo Alessia Elefante, akiripotiwa kuwa hajajeruhiwa, duru zililiambia Shirika la habari la AFP.
Katika taarifa, wakala wake alisema Gianluigi Donnarumma, 24, na mpenzi wake "wameshtushwa na kile kilichotokea lakini wanaendelea vizuri chini ya hali mbaya. Wote wanasaidia polisi kwa maswali yao".
Ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema kitengo maalum cha polisi cha BRB cha Ufaransa kinacholenga wizi wa kutumia silaha na wizi kimeanza uchunguzi.
Raila adai Kalonzo Musyoka anazuiliwa na polisi nyumbani kwake

Chanzo cha picha, Raila Odinga/facebbook
Kiongozi wa upinzani na Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga amedai kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka yuko katika kizuizi cha nyumbani.
Haya pia yalithibitishwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kalonzo Paloma Gatabki ambaye alisema kwamba Makamu wa Rais huyo wa zamani amezuiliwa nyumbani kwake tangu Jumanne jioni.
"Wawakilishi wa muungano wetu Mhe Opiyo Wandayi na Mhe Jeremiah Kioni leo wamemtembelea Mhe Kalonzo Musyoka kufuatia kuzuiliwa kwake nyumbani," alisema Odinga.
Hatahivyo hakuna tamko lolote kutoka kwa serikali kuthibitisha au kukanusha kuzuiliwa kwake.
Kenya sio taifa la polisi, mashirika ya kutetea haki za binadamu yaonya

Chanzo cha picha, GMG
Takriban watu 37 wameuawa na wengine 60 wamejeruhiwa tangu maandamano ya upinzani dhidi ya serikali nchini Kenya yalipoanza mwezi Machi, yamesema mashirika ya haki za binadamu.
Wakati huo huo taasisi ya usimamizi wa mienendo ya polisi nchini Kenya IPOA imeonya kuwa maafisa waliohusika na ufyatuaji wa risasi watawajibishwa.
Nashirika ya haki za binadamu yameelezea matatizo yanayowakumba polisi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa malipo ya malupulupu ya kazi, kufanya kazi saa nyingi, kupandishwa vyeo, matatizo ya afya ya akili, mambo yanayoweza kusababisha mienendo ya ukatili wakati wanapokabiliana na waandamanaji.
Mashirika hayo pia yalimlaumu Waziri wa usalama wa ndani Kindiki Kithure na Inspekta Mkuu wa Polisi Japheth Koome kwa kutotangaza wazi , idadi ya watu waliofariki, mwaliojeruhiwa, na madai ya kukamatwa kwa watu wakati wa maandamano na hivyo kuwasilisha taarifa hizo kwa IPOA kwa ajili ya uchunguzi.
Unawez apia kusoma:
- Maandamano Kenya: Tunachofahamu kufikia sasa
Maandamano Kenya: Upinzani wafanya mkutano na mabalozi

Chanzo cha picha, Kalonzo Musyoka/Twitter
Mmoja wa viongozi wakuu wa Muungano wa Azimio La Umoja One Kenya Kalonzo Musyoka Ijumaa amefanya mkutano wa faragha na wanadiplomasia kadhaa nyumbani kwake , jijini Nairobi Ijumaa.
Mkutano huo unakuja huku kukiwa na hali ya wasiwasi miongoni mwa mataifa na mashirika ya kigeni juu ya kuenea kwa ghasia na kupoteza maisha ya watu wakati wa maandamano ya kupinga serikali yanayoongozwa na muungano wa Azimio.
Haijajulikana ni nini hasa Bw kalonzo amezungumza na wanadiploamasia wa kigeni
Taarifa zinasema kuwa wanadiplomasia hao walikuwa ni kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Denmark.
Mapema wiki hii wanadiplomasia kutoka Marekani, Uingereza, Canada, Ujerumani na nchi nyingine tisa waliutaka Muungano wa Azimio la Umoja na serikali kutatua tofauti zao kwa amani.
Mwanaume Muingereza apatikana na hatia ya mauaji ya mke aliyekuwa mgonjwa mahututi Cyprus

Chanzo cha picha, FAMILY PHOTOGRAPH
Maelezo ya picha, Janice na David Hunter waliishi pamoja kwa zaidi ya miaka 50 Mwanamume wa Uingereza aliyemuua mkewe aliyekuwa mgonjwa sana nyumbani kwao Cyprus amepatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.
David Hunter, mwenye umri wa miaka 76, alishtakiwa kwa mauaji lakini aliondolewa baada ya kumkasirisha Janice Hunter mwenye umri wa miaka 74 nyumbani kwao karibu na Paphos mnamo Desemba 2021.
Mchimbaji madini mstaafu kutoka Ashington, Northumberland, alitekeleza kifo cha kusaidia kujiua cha mkewe, ambaye alikuwa na saratani ya damu, ambaye alikuwa amemsihi amalize masaibu yake.
Atahukumiwa tarehe 27 Julai.
Wakili wa Hunter alidai kuwa mteja wake alimsaidia Bi Hunter kujiua kwasababu alikuwa akiteseka na alimwomba afanye hivyo.
Majaji watatu katika mahakama ya wilaya ya Paphos hawakumpata na hatia ya mauaji lakini na hatia ya kuua bila kukusudia.
Bw Hunter aliiambia BBC kuwa alikuwa "mwenye furaha " baada ya uamuzi huo kutolewa.
Zelensky wa Ukraine amfuta kazi balozi wake nchini Uingereza Prystaiko baada ya kukosolewa

Chanzo cha picha, PA MEDIA
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfuta kazi balozi wa nchi yake nchini Uingereza.
Vadym Prystaiko hivi karibuni alikosoa jibu la rais kwa mzozo juu ya shukrani kwa msaada wa kijeshi wa Uingereza.
Alikuwa ameita ahadi ya Bw Zelensky ya kumshukuru waziri wa ulinzi wa Uingereza kila asubuhi "kejeli zisizofaa".
Kyiv haikutoa sababu rasmi ya kufutwa kazi lakini alithibitisha kuwa Bw Prystaiko hakuwa balozi tena.
Mapema mwezi huu, Ben Wallace alisema ameionya Ukraine kwamba washirika wake "si Amazon", akisema Kyiv inahitaji kuonyesha shukrani kwa silaha ilizopokea ili kuwashawishi wanasiasa wa Magharibi kutoa zaidi.
Alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa kilele wa Nato baada ya Rais Zelensky kukosoa muungano wa kijeshi kwa kuchelewa kuifanya Ukraine kuwa mwanachama.
Matamshi ya Bw Wallace yalichochea hasira mjini Kyiv na baadaye akasema maneno yake "yamepotoshwa kwa kiasi fulani".
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alijibu kwa kusema "ameshangazwa" na jinsi Ukraine inavyothamini uungwaji mkono wa Uingereza.
“Hatutarajii mtu yeyote kutupigania, tunaomba tu vifaa,” alisema na kuongeza “Ben anaweza kunipigia simu na kuniambia chochote anachotaka,” aliiambia Sky News.
Alikuwa katika wadhifa wake London tangu 2020 lakini siku ya Ijumaa Bw Zelensky alitoa amri ya rais kutangaza kufutwa kwake, akisema pia ameondolewa kama mwakilishi wa Ukraine katika Shirika la Kimataifa la Maritime.
Rais Zelensky amewafuta kazi mabalozi wake hapo awali, na kuwafukuza watano mara moja mwaka mmoja uliopita katika kile kilichoonekana kama mabadiliko.
"Tunawezaje kuonyesha shukrani zetu?" Bw Zelensky alisema akijibu maoni ya waziri wa ulinzi. "Tunaweza kuamka asubuhi na kumshukuru waziri. Hebu aniandikie na aniambie jinsi ya kumshukuru."
Bw Prystaiko alisema wiki jana kumekuwa na "kejeli kidogo" katika jibu la rais wake, ambalo aliamini kuwa "sio sawa".
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Kwa Picha: Kongamano kubwa zaidi la wanawake duniani mjini Kigali
Zaidi ya watu 6,000, wengi wao wakiwa wanawake, kutoka takriban nchi 170 wamekutana mji Kigali Rwanda katika mkutano wa siku nne -Women Deliver huku ukifuatiliwa na wanaweke wengine 200,000 kwa njia ya mtandao . Huu ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa wanawake duniani unaolenga kupigania haki zao mbalimbali, kufanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye mkutano huo:

Chanzo cha picha, Women Deliver
Maelezo ya picha, Ellen Johnson Sirleaf mwenye umri wa miaka 84 alikuwa Kigali kushiriki mkutano huu muhimu kuhusu haki za wanawake duniani. 
Chanzo cha picha, Women Deliver
Maelezo ya picha, Uwanja wa BK Kigali Arena, uliwapokea wageni 
Chanzo cha picha, Women Deliver
Maelezo ya picha, Malala Yousafzai aliyetunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel na akiwa na Maliha Khan, mkuu wa Women Deliver. 
Chanzo cha picha, Women Deliver
Maelezo ya picha, Simbine Graca Machel, mjane wa rais wa zamani wa Msumbiji Samora Machel, na Nelson Mandela wa Afrika Kusini, mwanaharakati wa haki za mtoto wa kike. 
Chanzo cha picha, Women Deliver
Maelezo ya picha, Miss Universe 2019 Miss Universe Zozibini Tunzi (mwenye mavazi ya bluu) alihudhuria hafla hiyo 
Chanzo cha picha, Women Deliver
Maelezo ya picha, Maliha Khan (aliyevaa nguo nyekundu) na Jeannette Kagame (wakimsalimia mtoto) 
Chanzo cha picha, Women Deliver

Chanzo cha picha, Women Deliver

Chanzo cha picha, Women Deliver
Maelezo ya picha, Katika Kituo cha Mikutano cha Kigali, kulikuwa na maandamano ya wafuasi wa uavyaji mimba 
Chanzo cha picha, Women Deliver
Maelezo ya picha, Nafasi ya 'Selfie' na vijana Mkutano huu umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitatu tangu 2007, na mkutano huu wa Kigali ulikuwa wa sita, baada ya mingine huko London, Washington DC, Kuala Lumpur, Copenhagen, na wa mwisho mwaka 2019 ulifanyika Vancouver, Canada.
Mkutano wa mjini Kigali, uliomalizika Alhamisi, imevutia watu wengi zaidi kuliko ile ya awali, kulingana na waandalizi.
Katika mitandao ya kijamii kama Instagram na Twitter, kuna picha na jumbe nyingi za washiriki waliofurahia mafanikio ya mkutano huo na kushangazwa na uzuri wa Kigali na mapokezi mazuri nchini Rwanda.
Gavana wa Sudan atoa wito kwa Darfur kuchukua silaha

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Makumi kwa maelfu ya watu wametoroka mzozo wa Darfur na kuelekea nchi jirani ya Chad. Gavana wa Darfur na kiongozi wa zamani wa waasi Minni Arko Minnawi amerudia wito wake kwa raia katika eneo hilo kuchukua silaha ili kujilinda, akisema "hali ya sasa inalazimu hilo", Chombo cha habari Al Arabiya kimeripoti.
Alisema utawala huu ulikuwa unaongoza juhudi za kusitisha mapigano kati ya Rapid Support Forces (RSF) na jeshi, haswa huko Darfur.
Mzozo huo sasa uko katika mwezi wake wa nne.
Bw Minnawi ametoa matamshi sawa na hayo siku za nyuma, na kuzua hofu kwamba Darfur, ambayo imegawanywa katika majimbo matano, inaweza kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe huku kukiwa na ongezeko la mivutano ya kikabila.
Kwingineko nchini humo, mapigano makali yaliripotiwa kati ya jeshi na RSF huko Khartoum, Omdurman na Bahri, miji mitatu inayounda mji mkuu wa Sudan.
Walioshuhudia mjini Khartoum walisema jeshi lilifanya mashambulizi "makali zaidi ya anga" kuwahi kushuhudiwa dhidi ya vikosi vya RSF katika maeneo kadhaa. Jeshi lilisema kuwa liliwaua wapiganaji 18 wa RSF katika mapigano huko Omdurman na Khartoum.
Mapigano mapya pia yaliripotiwa huko Nyala, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini, baada ya mapigano kutulia.
Mapigano hayo yameendelea licha ya kufanyika kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya jeshi na wawakilishi wa RSF katika mji wa Jeddah wa Saudia.
Soma zaidi:
Waandamanaji wachoma moto ubalozi huku Iraq ikimfukuza balozi wa Sweden baada ya Quran kuchomwa

Chanzo cha picha, Muhannad Al-Azzawi
Serikali ya Iraq imemuamuru balozi wa Uswidi mjini Baghdad kuondoka huku mzozo wa kidiplomasia kuhusu tukio la hivi karibuni la kuchomwa moto kwa Quran mjini Stockholm ukizidi kuendelea.
Waandamanaji katika mji mkuu wa Iraq walivamia ubalozi wa Uswidi kwa mara ya pili siku ya Alhamisi na kuchoma makao yake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uswidi alielezea maandamano hayo kuwa "hayakubaliki kabisa".
Mamia ya watu walivunja ubalozi huo baada ya kusikia kuwa mkimbizi Mkristo amepewa kibali na polisi wa Uswidi kuchoma moto Quran huko Stockholm kwa mara ya pili.
Katika tukio hilo Salwan Momika alikanyaga kitabu takatifu cha Quran nje ya ubalozi wa Iraq lakini hakukichoma moto.
Mwezi uliopita alichoma nakala yake nje ya msikiti mkuu wa Stockholm.
Pia maandamano ya Stockholm yaliruhusiwa kuendelea baada ya mahakama kubatilisha marufuku ya polisi, kwa sababu ya haki ya kisheria ya uhuru wa kukusanyika.
Waislamu wanaichukulia Quran kuwa kitabu chenye neno la Mwenyezi Mungu na wanaona uharibifu wowote wa kimakusudi au kuonyesha kutoiheshimu kuwa tukio la kuudhi kweli kweli.
Tazama jinsi waandamanaji walivyovunja ubalozi wa Sweden:
Maelezo ya video, Tazama: Waandamanaji walichoma moto ubalozi wa Uswidi mjini Baghdad Soma zaidi:
Naugua mafua makali asema kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema anaugua mafua makali ambayo yalimpata mwanzoni mwa wimbi la tatu la maandamano ya kupinga serikali.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha NTV kwa njia ya simu Bw Odinga hata hivyo alisema anaendelea vyema na kuongeza kuwa kutoonekana kwake na kutoshiriki kwa viongozi wengine wakuu wa upinzani katika maandamano hayo kunamanisha ni maandamano ya Wakenya.
''Maandamano sio ya baba, ya Martha au ya Kalonzo au ya mtu mwingine. Maandamano ni ya Wakenya wote’’, alisema Odinga
Maandamano hayo yameitishwa na upinzani kupinga gharama ya juu ya Maisha na muswada wa fedha wa 2023 uliozuiwa na mahakama baada ya bunge kuunga mkono.
Rais William Ruto amesema kwamba serikali yake itaendelea kulinda usalama na demokrasi ya taifa la kenya kwa hali na mali.
Mashirika ya haki za binadamu yametaja idadi ya waliofariki katika maandamano nchini Kenya kufikia watu 30 tangu maandamano ya kuipinga serikali yaanze wiki mbili zilizopita.
Melezo zaidi:
Viongozi wa Ukraine na Ethiopia wajadili mzozo wa Urusi

Viongozi wa kisiasa wa Ukraine na Ethiopia wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu kwa mara ya kwanza kabisa, ujumbe wa Twitter kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky ulisema.
Mazungumzo kati ya Bw Zelensky na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed yalifanyika baada ya Urusi kujiondoa katika makubaliano ambayo yaliruhusu usafirishaji wa nafaka wa Ukraine kwa njia salama.
Kumekuwa na wasiwasi juu ya athari za uamuzi huu kwa usalama wa chakula katika nchi maskini.
"Nilimjulisha mpatanishi kwamba Ukraine imesambaza karibu tani 300,000 za chakula kwa Ethiopia chini ya Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi na tani nyingine 90,000 za nafaka chini ya mpango tofauti wa ‘Grain From Ukraine’," rais wa Ukraine alisema katika tweet yake.
"Nilisisitiza kuwa Ukraine bado iko tayari kubaki mdhamini wa usalama wa chakula duniani."
Tweet ya Bw Abiy kuhusu simu hiyo ilikuwa ya kifupi zaidi.
Aliandika: "Nimekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Zelensky leo ili kujadili masuala ya pande mbili na ya kimataifa yenye maslahi ya pamoja na njia za kuleta amani kati ya Ukraine na Urusi."
Soma zaidi:
Man Utd yakamilisha usajili wa Andre Onana kwa pauni milioni 47.2

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Andre Onana alicheza chini ya kocha wa United Erik ten Hag huko Ajax, akishinda mataji matatu ya ligi. Manchester United wamekamilisha usajili wa mlinda mlango Andre Onana kutoka Inter Milan kwa kima cha pauni milioni 47.2m.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 27, ametia saini mkataba wa miaka mitano, na chaguo la kuongezwa kwa miezi 12.
Mkataba huo una thamani ya pauni milioni 43.8 pamoja na nyongeza zinazoweza kufikia za pauni milioni 3.4.
Kipa huyo wa zamani wa Ajax anatazamiwa kuungana na kikosi cha United katika ziara yao ya kujiandaa kwa msimu mpya nchini Marekani.
"Kujiunga na Manchester United ni heshima kubwa," alisema. "Nimejitahidi sana maishani kufikia ufanisi huu, nikikabilianam na vizuizi vingi njiani.
Onana atachukua nafasi ya David de Gea kama mlinda mlango wa kikosi cha kwanza cha United, baada yaMhispania huyo kuondoka mwezi huu wa Julai wakati mkataba wake ulipokamilika baada ya miaka 12 katika klabu hiyo.
"Huu ni mwanzo wa safari mpya kwangu, na wachezaji wenzangu wapya na malengo mapya ya kupigania, alisema Onana.
"Manchester United ina historia ndefu ya makipa mahiri, na sasa nitafanya kila niwezalo kuandikisha historia yangu katika miaka ijayo,"Onana aliongeza.
Onana alicheza chini ya kocha wa United Erik ten Hag kwa kipindi cha miaka saba na nusu huko Ajax, na kushinda mataji matatu ya ligi.
Pia unaweza kusoma:
Travis King:Mwanajeshi wa Marekani aliyevuka mpaka kuingia Korea Kaskazini, hayupo kazini wala likizo - Pentagon

Chanzo cha picha, Reuters
Wizara ya ulinzi ya Marekani inasema inamchukulia mwanajeshi Travis King kuwa "hayupo kazini na hayupo likizo" baada ya kuvuka mpaka na kuingia Korea Kaskazini.
Maafisa pia walikiri hawakuwa na habari kuhusu hali yake au mahali alipokuwa akishikiliwa.
Awali, Ikulu ya White House ilisema Marekani ilijaribu kuwasiliana na Korea Kaskazini kupitia "njia nyingi" lakini haikupata jibu.
King alikimbia kuvuka eneo la mpaka lenye ulinzi mkali siku ya Jumanne.
Haijulikani ikiwa ameasi au anatarajia kurudi.
Tovuti ya habari yenye makao yake mjini Washington ya Messenger ilisema kuwa imeona ripoti ya ndani ya serikali ya Marekani ambayo ilieleza matendo ya King alipovuka mpaka.
Ilinukuu ripoti hiyo ikisema King alikimbia hadi kwenye jengo upande wa Korea Kaskazini.
Inasemekana aligonga mlango kwa nguvu, na wakati hakukuwa na jibu, alikimbia kuzunguka nyuma na kuingia kwenye gari.
Kisha mara moja akasafirishwa, kulingana na tovuti.
Wataalamu wanasema mwanajeshi wa ngazi ya chini kama huyo atakuwa na thamani ndogo ya kijasusi na propaganda kidogo, ambayo inaweza kusababisha Korea Kaskazini kumwachilia - lakini kitakachomtokea bado hakijafahamika.
Christine Wormuth, mkuu wa Jeshi la Marekani, ameelezea "wasiwasi mkubwa" kwa Travis King na jinsi anaweza kutibiwa.
Aliambia Jukwaa la Usalama la Aspen: " Kusema ukweli, nina wasiwasi juu yake."
Mgogoro huo unawadia wakati wa mvutano haswa na Korea Kaskazini.
Uhusiano na Marekani umeporomoka katika miaka ya hivi karibuni, kwani imefanyia majaribio makumi ya makombora yenye nguvu zaidi yanayoweza kubeba vichwa vya nyuklia.
Katika ushauri wake wa usafiri, Marekani inawaambia raia wake wasisafiri hadi Korea Kaskazini - mojawapo ya mataifa yaliyojitenga zaidi duniani - kutokana na "hatari kubwa inayoendelea ya kukamatwa" na "tishio kubwa la kuwekwa kizuizini bila makosa".
Pia unaweza kusoma zaidi:
Mchina ahukumiwa baada ya ufichuzi wa BBC Malawi

Maelezo ya picha, Lu Ke alisema alitengeneza video zake ili kueneza utamaduni wa Wachina Mahakama ya Malawi imempata na hatia raia wa Uchina kwa mashtaka mengi yakiwemo ulanguzi na kushirikisha watoto katika burudani.
Lu Ke, ambaye pia anajulikana kwa jina la Susu, amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela, ambacho tayari ametumikia akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Ameamriwa kuondoka nchini ndani ya siku saba na amezuiwa kurejea tena.
Alikamatwa mwaka jana kufuatia ripoti ya uchunguzi wa BBC Africa Eye.
Ripoti hiyo ilimuonyesha akiwarekodi watoto wa Malawi wakitengeneza video za salamu za kibinafsi, baadhi zikiwa na maudhui ya ubaguzi wa rangi.
Video hizo zilikuwa zikinunuliwa kwa hadi $70 (£55) kwenye mitandao ya kijamii ya Uchina na majukwaa ya intaneti.
Wakati habari za video zake za kuudhi zilipoibuka, alikimbilia nchi jirani ya Zambia huku mamlaka ya Malawi ikitoa kibali cha kukamatwa kwake.
Alikamatwa na kupatikana na hatia ya kuingia nchini humo kinyume cha sheria na kisha kurejeshwa nchini Malawi.
Alinyimwa dhamana na amekuwa chini ya ulinzi wa polisi hadi hukumu yake siku ya Alhamisi.
Alikabiliwa na mashtaka 14 dhidi yake, yakiwamo ya kununua watoto kwa ajili ya matumizi ya burudani, ulanguzi wa watoto, matumizi haramu ya mtandao na mila potofu ya kijamii.
Hata hivyo, Lu Ke alikanusha kutengeneza video za kudhalilisha.
Katika utetezi wake, mahakama iliambiwa tayari alikuwa amelipa kwacha ya Malawi 16m ($16,000; £12,500) kwa serikali ili kuwafidia waathiriwa wake na kwa shughuli za uwajibikaji katika kijamii.
Lu Ke alijitetea akisema ametengeneza video zake ili kueneza utamaduni wa Wachina kwa jamii ya eneo
Marekani yasema Ukraine inatumia vizuri mabomu ya kutawanyika

Chanzo cha picha, Magnum Photos
Ikulu ya White House imethibitisha kuwa Ukraine inatumia mabomu ya cluster yaani ya kutawanyika ya Marekani dhidi ya vikosi vya Urusi nchini humo.
Msemaji wa Usalama wa Kitaifa John Kirby alisema maoni ya awali yanaonyesha kuwa yanatumiwa "ipasavyo" kwenye nafasi za ulinzi za Urusi wakati wa operesheni.
Mabomu aina ya cluster hutawanya mabomu mengi na yamepigwa marufuku na zaidi ya mataifa 100 kutokana na tishio lao kwa raia.
Marekani ilikubali kuyasambaza ili kuongeza silaha kwa Ukraine.
Ukraine imeahidi mabomu hayo yatatumika tu kuwaondoa wanajeshi ambao ni adui wa Urusi.
"Wanayatumia ipasavyo," Bw Kirby alisema.
"Wanayatumia ipasavyo na ukweli ni kwamba yana athari kwa safu ya ulinzi ya Urusi hasa katika ujanja wao wanaotumia. Nadhani naweza kuachia hapo."
Marekani iliamua kutuma mabomu ya kutawanyika baada ya Ukraine kuonya kwamba inaishiwa na silaha wakati wa mashambulizi yake ya majira ya joto, ambayo yamekuwa ya polepole na ya gharama zaidi kuliko wengi walivyotarajia.
Rais Joe Biden aliita uamuzi huo "mgumu kwelikweli", huku washirika wake Uingereza, Canada, New Zealand na Uhispania wakipinga matumizi yake.
Idadi kubwa ya silaha iliyotumwa ni mizinga yenye kiwango cha chini cha 2.35% cha "kutolipuka", rejeleo la asilimia ya mabomu ambayo hayalipuki mara moja na yanaweza kubaki tishio kwa miaka.
Silaha hizo ni nzuri zinapotumiwa dhidi ya wanajeshi kwenye mahandaki na maeneo yenye ngome, kwani zinafanya maeneo makubwa kuwa hatari sana kusongea kutoka eneo moja hadi jingine ukiwa ndani hadi yaondolewe.

Chanzo cha picha, Reuters
Urusi imetumia mabomu kama hayo hayo ya kutawanyika nchini Ukraine tangu ilipoanzisha uvamizi wake kamili mwaka jana, ikiwa ni pamoja na katika maeneo ya kiraia.
Akijibu uamuzi wa Marekani wa kutuma mabomu hayo, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema nchi yake ina silaha zinazofanana na hizo na zitatumiwa "ikiwa zitatumika dhidi yetu".
Oleksandr Syrskyi, jenerali wa Ukraine anayesimamia operesheni mashariki mwa nchi hiyo, aliambia BBC wiki iliyopita kwamba vikosi vyake vinahitaji silaha "kusababisha uharibifu mkubwa kwa wanajeshi wa adui wa kutembea kwa miguu".
Soma zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya leo 21/07/2023
