Wizara ya afya inayodhibitiwa na Hamas yasema watu 9,000 waliuawa huko Gaza tangu tarehe 7 Oktoba

Wizara ya afya inayodhibitiwa na Hamas huko Gaza imesema takribani watu 27 wameuawa kwa shambulio la Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

  1. Mwanamuziki maarufu kutoka Mombasa Ally B aaga dunia

    ..
    Maelezo ya picha, Mwanamuziki maarufu mjini Mombasa Ally B

    Mwanamuziki nguli wa pwani Ally B, anayefahamika kwa vibao kama vile ‘Maria’ na ‘Bembea’ amefariki dunia.

    Kulingana na Gazeti la The standard nchini Kenya , msanii huyo alifariki alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mombasa, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

    Ally B, ambaye jina lake halisi ni Ali Khamisi Mwaliguli, alikuwa mmoja wa wasanii wakubwa nchini Kenya mwanzoni mwa miaka ya 2000.

    Ally B alijiunga na siasa mwaka kwa muda mfupi 2017, akijaribu kuwania kiti cha mwakilishi wa wadi katika Wadi ya Junda huko Kisauni, Kaunti ya Mombasa. Ameombolezwa na mashabiki wake wengi, wakiwemo wasanii mashuhuri

  2. Jeshi la Israel limesema wanajeshi 15 waliuawa katika operesheni ya Gaza

    Jeshi la Israel limetangaza wanajeshi wake 15 wameuawa huko Gaza tangu Jumanne.

    Ni ongezeko la idadi ya waliokufa hapo awali ya 11 ambayo iliripotiwa na maafisa asubuhi ya leo.

  3. Habari za hivi punde, Jeshi la Israel linasema wanajeshi wake 15 waliuawa katika operesheni ya Gaza

    Jeshi la Israel limetangaza wanajeshi wake 15 wameuawa huko Gaza tangu Jumanne.

    Ni ongezeko la idadi ya waliokufa hapo awali ya wanajeshi 11 ambayo iliripotiwa na maafisa asubuhi ya leo.

  4. Watu 150 na magari 20 ya wagonjwa yavuka hadi Misri

    Mwandishi wa habari

    Hapa kwenye mpaka wa Rafah kuingia Misri kuna takribani watu 350 wanaosubiri vitambulisho vyao vikaguliwe.

    Kufikia sasa, 150 wamesafirishwa kwenye mpaka kwa mabasi. Hakuna mfumo wa kielektroniki au muhuri wa pasipoti, kila kitu kiko chini.

    Kuna afisa wa kiraia wa Kipalestina anayekagua pasi za kusafiria na kisha kuruhusu zile zilizo kwenye orodha ya watu walioruhusiwa kuondoka.

    Kutoka hapo, watasafirishwa moja kwa moja hadi upande wa Misri ambapo kutakuwa na udhibiti sahihi wa pasipoti.

    Takribani mita 20 kutoka niliposimama kuna geti lingine lililotengenezwa kwa ajili ya magari kupita.

    Tumeona magari ya wagonjwa yapatayo 20 au 30 yakipitia humo hadi Misri, yakiwabeba wale waliojeruhiwa vibaya sana.

    Kutoka hapo, watasafirishwa hadi hospitali, takribani kilomita 10 (maili 6) na kisha kupelekwa kwaajili ya matibabu zaidi.

    Unaweza kusoma;

  5. Asamoah Gyan: Nahodha wa zamani wa Ghana kumlipa fidia mke wake wa zamani baada ya kesi ya talaka

    Nahodha wa zamani wa Ghana Asamoah Gyan

    Nahodha wa zamani wa Ghana Asamoah Gyan lazima alipe fidia kwa mke wake wa zamani baada ya mahakama kutoa uamuzi kuhusu kesi yao ya talaka na kuamua kuwa yeye ndiye baba mzazi wa watoto wao watatu.

    Mahakama nchini Ghana ilimuamuru kijana huyo mwenye umri wa miaka 37 kumpa Gifty Gyan nyumba nchini Uingereza, nyumba mjini Accra, kituo cha mafuta na magari mawili.

    Gyan na mke wake wa zamani wamekuwa kwenye vita vya kisheria kwa miaka mitatu, huku kesi ya talaka ya wanandoa hao ikitolewa kufuatia madai ya mwanasoka huyo kwa mke wake kutokuwa mwaminifu na madai yake kwamba watoto wao watatu huenda wasiwe wake.

    Uchunguzi wa DNA ulikanusha madai yake. Siku ya Jumanne, mahakama iliamua kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Udinese, Rennes na Sunderland lazima pia alipe cedis 25,000 za Ghana ($2,100, £1,729) kwa mwezi kwa ajili ya malezi ya watoto.

    Ingawa wenzi hao walikuwa tayari wametengana, mahakama ilibatilisha ndoa hiyo kufuatia ombi lililojazwa na Asamoah Gyan.

    Mahakama iliamua kwamba Gifty Gyan alikuwa ametoa mchango usio wa pesa katika ununuzi wa mali hizo kwa sababu ni yeye pekee aliyekuwa akiwalea watoto wao huku Gyan akifanya biashara yake.

    Nyumba ya vyumba vinne huko Accra ilinunuliwa kwa ajili yake kabla ya ndoa yao ya 2013. Kabla ya kufunga ndoa rasmi miaka 10 iliyopita, wenzi hao walikuwa na watoto wawili.

  6. Habari za hivi punde, Vita vya Gaza: Magari ya kwanza ya wagonjwa yaliyobeba majeruhi yaingia Misri - ripoti

    Katika dakika chache zilizopita, mashirika ya habari ya Reuters na AFP yanasema magari ya kwanza ya wagonjwa yaliyowabeba watu waliojeruhiwa kutoka Gaza yameingia Misri kupitia kivuko cha Rafah.

    Mashirika hayo yanawanukuu maafisa nchini Misri.

  7. Florida: Rubani aokolewa baada ya ndege kuanguka katika eneo lenye unyevu Everglades

    Maelezo ya video, Tazama: Rubani aokolewa kutoka katika bawa la ndege kuzama majini

    Rubani mmoja ameokolewa baada ya kukaa saa tisa katika eneo la Everglades huko Florida baada ya ndege yake ndogo kuanguka.

    Florida Everglades ndio maji pekee ambapo mamba wanaokula wanadamu huishi sawa na mamba wa kawaida.

    Video iliyosambazwa na Miami-Dade Fire Rescue inaonyesha mwanamume huyo akiwa amekaa kwenye bawa la ndege, akisubiri kuokolewa, kabla ya helikopta kuja kumsaidia.

    Mwanamume huyo aliyekuwa na majeraha madogo alipelekwa hospitali.

  8. Bolivia yakata uhusiano wa kidiplomasia na Israel

    Gaza

    Bolivia imesema imekata uhusiano wa kidiplomasia na Israel kutokana na operesheni yake ya kijeshi huko Gaza.

    Naibu waziri wa mambo ya nje, Freddy Mamani alilaani hatua za Israel kuwa "uchokozi na zisizo na uwiano".

    Bolivia ni nchi ya kwanza ya Amerika Kusini kuvunja uhusiano na Israel kutokana na mzozo huo.

    Imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na kusema kuwa itatuma msaada huko Gaza.

    Nchi hiyo ilirejesha uhusiano na Israeli mnamo 2019, muongo mmoja baada ya kukatwa kutokana na mashambulio ya hapo awali kwenye Ukanda wa Gaza.

    Unaweza kusoma;

  9. Mwanaume afungwa miaka 52 jela kwa kumuua mtoto kwa tambiko Uganda

    Mikono yenye pingu

    Mahakama ya juu katika wilaya ya Iganga mashariki mwa Uganda imemhukumu mwanaume mmoja kwa kifungo cha miaka 52 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wa miaka 5 kwa tambiko za kishirikina.

    Jaji David Batema, alitoa hukumu ya kufungwa kwa Hassana Kafudde pamoja na Issa Muyita ambaye alihukumiwa miaka 25 gerezani.

    Issa ni baba wa marehemu Juma Muyita na anashutumiwa kwa kushirikiana na Kafudde kumua mtoto wake ambaye wakati alipoliuliwa alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi ya Mirembe Junior katika eneo la Kawempe mnamo mwaka 2017.

    Katika uamuzi wake, jaji Batema alibaini kuwa hukumu hiyo nzito ililenga kuzuia vitendo kama hivyo.

    Watetezi wa haki za watoto nchini Uganda wameipongoza mahakama hiyo kwa uamuzi huo.

  10. Wakenya wakasirishwa na ushuru mpya kwa wasafiri

    Baadhi ya maofisa wa mapato wanadaiwa kutumia fursa ya agizo hilo kuwanyanyasa watalii

    Wakenya wanapinga agizo la mamlaka ya mapato linalotaka kutoza ushuru bidhaa za kibinafsi au za nyumbani zenye thamani ya $500 (£400) na zaidi kutokana na watalii wanaozuru na raia wanaorejea nchini.

    Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) inasema bidhaa zote ziwe mpya au za mtumba za thamani hiyo zitatozwa ushuru.

    Maagizo hayo yamezua taharuki kwa wananchi huku Wakenya wengi wakisema kuwa hatua hiyo itawatia hofu watalii.

    Baadhi ya wabunge walisema baadhi ya maafisa wa KRA wamekuwa wakichukua fursa ya agizo hilo kuwasumbua watalii, hali inayoipa nchi sifa mbaya.

    Waziri wa Utalii Alfred Mutua alitaja hatua hiyo ya KRA kuwa mojawapo ya sababu ya idadi ya watalii wanaozuru nchini kupungua.

    “Wewe nenda Rwanda, hawakusumbui. Je, Rwanda haitoi kodi? Unaenda Afrika Kusini, na hawakusumbui. Huko Dubai, hawakunyanyasi. Kwa hivyo, kwa nini wageni wetu wanakabiliwa na changamoto kama hizi nchini Kenya? Na tunashangaa kwa nini watu hawaji Kenya,” Bw Mutua alisema.

    Ni hatua ya hivi karibuni zaidi katika msururu wa ushuru mpya ulioanzishwa na serikali ya Rais William Ruto, ukilaumiwa kwa kuzorota kwa gharama ya maisha nchini.

    Hii ni licha ya kwamba Bw Ruto alishinda uchaguzi mwaka jana kwa ahadi ya kupunguza matatizo ya kiuchumi.

  11. Utapiamlo kwa watoto waongezeka kwa 160% Nigeria - Shirika lisilo la kiserikali

    Utapiamlo ndio chanzo kikuu cha vifo vya watoto nchini Nigeria

    Utapiamlo mkali miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kaskazini-mashariki mwa Nigeria Unaongezeka kwa kasi, shirika lisilo la kiserikali limeonya.

    FHI 360 ilisema kwamba idadi kubwa ya watoto wenye utapiamlo - 15,781, walilazwa katika vituo vyake kati ya Februari na Septemba kwa ajili ya matibabu, ongezeko la karibu 160% kutoka mwaka jana.

    "Hali ya kaskazini-mashariki mwa Nigeria ni mbaya na msaada unahitajika kushughulikia mahitaji muhimu ya kiafya na lishe ya jamii, haswa wanawake na watoto," shirika hilo liliongeza.

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, Unicef, limesema hapo awali kuwa Nigeria inashika nafasi ya pili kwa kiwango cha juu cha udumavu wa watoto duniani, ambao unasababishwa na utapiamlo ulioenea hasa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

    Unicef ​​​​inakadiria kuwa watoto milioni mbili nchini Nigeria wanakabiliwa na utapiamlo, lakini ni 20% tu ya hao hupata matibabu.

    Takwimu za Unicef ​​pia zinaonesha kuwa utapiamlo unachangia asilimia 45 ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Nigeria.

    Unaweza kusoma;

  12. Netanyahu asema wanajeshi wa Israel walikufa katika 'vita vya haki'

    Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alitoa hotuba ya video kwenye mitandao ya kijamii

    Tumekuwa tukiangazia kivuko cha Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza asubuhi ya leo, lakini tumesikia maoni mapya kutoka kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

    Alikuwa akizungumza baada ya Israel kuthibitisha kwamba wanajeshi 11 walifariki katika mapigano mjini Gaza siku ya Jumanne. "Tuko kwenye vita ngumu. Vitakuwa vita vya muda mrefu.

    Tuna mafanikio muhimu ndani yake, lakini pia hasara na uchungu," anasema. "Tunajua kila askari wetu ni sawa na ulimwengu mzima. “Taifa zima la Israel linawakumbatia ninyi, ndani ya mioyo yetu.

    Sote tuko pamoja nanyi katika wakati wenu wa huzuni kuu.

    "Wanajeshi wetu walifariki katika vita vya haki, vita kwa ajili ya taifa letu. Ninawaahidi ninyi raia wa Israeli: tutaendelea hadi tutakapotimiza lengo letu, tutaendelea hadi tutakapopata ushindi."

    Unaweza kusoma;

  13. Mpangaji mkuu wa mapinduzi yaliyotibuliwa Gambia afungwa miaka 12 jela

    Lance Koplo Sanna Fadera alikanusha mashtaka wakati wa hukumu ya Jumanne
    Maelezo ya picha, Lance Koplo Sanna Fadera alikanusha mashtaka wakati wa hukumu ya Jumanne

    Afisa wa jeshi la wanamaji aliyetajwa na serikali ya Gambia kuwa mpangaji mkuu wa njama ya mapinduzi yaliyotibuliwa mwezi Disemba mwaka jana amepatikana na hatia ya uhaini na kuhukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.

    Mahakama kuu siku ya Jumanne iliamua kwamba Lance Koplo Sanna Fadera alipanga na kujaribu kupindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Rais Adama Barrow.

    Mamlaka ilikuwa imemshtaki Fadera na wanajeshi wengine saba kwa uhaini, kula njama na kuchochea uasi kwa madai ya kuhusika katika jaribio la mapinduzi ya 2022.

    Mahakama iliwaachilia huru maafisa wengine watatu wa kijeshi siku ya Jumanne.

    Mwanajeshi mwingine amekuwa akikimbia tangu jaribio la mapinduzi lililoshindwa na anachukuliwa kuwa mtoro.

    Mahakama pia ilimuachia huru afisa wa polisi na raia wawili waliokuwa wameshtakiwa kwa kuficha uhaini na kula njama ya kutenda uhalifu.

    Kabla ya Rais Barrow kuingia madarakani, nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilitawaliwa kwa miongo miwili na Yahya Jammeh, ambaye alichukua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 1994, na kuzuia majaribio kadhaa ya kutaka kumpindua, kabla ya kushindwa katika uchaguzi wa 2016.

  14. Ujerumani na EU kusaidia mapambano dhidi ya wanamgambo Afrika Magharibi

      • Author, Thomas Naadi
      • Nafasi, BBC News, Accra
    xx

    Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa Umoja wa Ulaya na taifa lake watatoa msaada wa kiusalama ili kukabiliana na vitisho vinavyotolewa na wanamgambo wa kijihadi katika kanda ya Afrika Magharibi.

    Akizungumza siku ya Jumanne katika mji mkuu wa Ghana wa Accra, Kansela Scholz alielezea wasiwasi wake kwamba wanamgambo wanaweza kuchukua fursa ya uvamizi wa kijeshi wa hivi karibuni lakini pia alisema kuwa Ujerumani na EU zinaweza kutoa vifaa na mafunzo kusaidia kudhibiti ushawishi wao katika eneo hilo.

    Kwa kuondoka kwa Wafaransa na kusitishwa taratibu kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Sahel, serikali za kijeshi katika mataifa ya Mali, Burkina Faso na Niger zinakabiliwa na changamoto kubwa katika juhudi za kuzima uasi wa kijihadi unaosababisha kuenea kwa umwagaji damu kwa nchi za Pwani ya Afrika Magharibi.

    Ghana tayari imepokea zaidi ya magari 100 ya kijeshi kutoka Umoja wa Ulaya.

    Magari hayo ambayo ni sehemu ya mfuko wa msaada wa Euro milioni 20 kwa jeshi la Ghana, yalikamatwa kutoka kwa meli nje ya pwani ya Libya ambayo ilikiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa vya silaha kwa Libya.

    Umoja wa Ulaya pia umeahidi kutoa usaidizi wa ziada katika mfumo wa ufuatiliaji wa angani, mifumo ya kivita ya kielektroniki, na ufundi wa mito kwa Ghana.

    Kansela Olaf Scholz, ambaye yuko katika hatua ya mwisho ya safari yake ya tatu katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, alisema kuwa ujumbe unaokuja wa Umoja wa Ulaya katika Ghuba ya Guinea utatoa vifaa na mafunzo yanayohitajika kusaidia wanajeshi katika kukabiliana na vitisho vya jihadi.

    Rais Nana Akufo-Addo, amesema kuwa mataifa yote yanatakiwa kujitayarisha kukabiliana na shughuli za wanamgambo, jambo ambalo kwa sasa linatia wasiwasi mkubwa.

    Tangu mwaka wa 2012, wakati vuguvugu la watu wanaotaka kujitenga kaskazini mwa Mali dhidi ya serikali lilipochukuliwa na vikundi vya Jihadi na kuenea katika nchi jirani, zaidi ya watu milioni sita wamekufa, na maelfu wameyahama makazi yao.

    Mataifa ya Pwani ya Afrika Magharibi kama vile Ivory Coast, Togo na Benin yamekuwa yakilengwa mara kwa mara na wanamgambo wenye mafungamano na IS na Al-Qaeda.

    Nchi za Pwani ya Afrika Magharibi tayari zinaweka mpango wa kukabiliana na vitisho hivyo.

    Wanaanzisha kikosi kazi cha usalama cha kimataifa chini ya mpango wa Accra utakaokuwa na makao yake kaskazini mwa Ghana ili kuzuia kuenea kwa itikadi kali kali katika eneo hilo.

    Pia unaweza kusoma:

  15. Mahakama ya Uganda yawatoza faini wanandoa wa Marekani kwa kumtesa mtoto wa kambo

    TH

    Mahakama nchini Uganda imewaamuru wanandoa wa Marekani walioshtakiwa kwa kumtesa mtoto wao wa kambo kumlipa $26,000 (£20,700) kama fidia.

    Fidia hiyo ilitokana na makubaliano ya rufaa, ambayo pia yaliifanya mahakama kuwafutia mashtaka ya biashara haramu ya ulanguzi na mateso dhidi ya wanandoa hao, jambo ambalo lingewafanya kupata kifungo cha maisha jela au kifo.

    Wanandoa hao, Nicholas na Mackenzie Spencer walikamatwa mwaka jana na kushtakiwa kwa kumtesa mvulana huyo wa miaka 10 kwa kipindi cha miaka miwili.

    Hii ni baada ya yaya wa mtoto huyo kuandikisha ripoti polisi akidai kuwa wanandoa hao walimtendea unyama mtoto huyo mara kwa mara.

    Siku ya Jumanne, walikiri mashtaka ya unyanyasaji wa kikatili, unyama au udhalilishaji, kufanya kazi bila vibali na kukaa Uganda kinyume cha sheria, ambapo walitozwa faini ya shilingi za Uganda milioni 4.86.

    Lakini uamuzi huo wa Jumanne umewakasirisha wanaharakati wa haki za watoto ambao walikiita "kejeli kwa haki".

    Mwanaharakati Proscovia Najjumba alihoji jinsi mahakama iliwaruhusu wanandoa hao "kuondoka" baada ya kukubali "walimtendea mtoto ukatili", shirika la habari la AFP liliripoti.

    Nyaraka za mahakama zilionyesha kwamba wanandoa hao walimpa mtoto chakula baridi, na kumfanya alale kwenye jukwaa la mbao lisilo na godoro .

  16. Waasi wa Mali wadai kudhibiti kambi ya Kidal baada ya kuondoka Umoja wa Mataifa

    th

    Waasi wa Tuareg wa Mali wanasema wameteka kambi katika mji wa kaskazini wa Kidal iliyoachwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.

    Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, Minusma, ulisema ulimaliza kuwepo kwake Kidal kwa haraka baada ya msafara wake wa mwisho wa walinda amani kukumbwa na mashambulizi mawili ya IED njiani kuelekea Gao, mji mwingine muhimu kaskazini.

    Muungano wa Tuareg ulidai ushindi kwenye mitandao ya kijamii, ukisema ulikuwa unadhibiti kambi ya Kidal.

    Afisa mmoja wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba waasi waliikalia kambi hiyo mara tu baada ya kuondolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa.

    Ilikuwa kambi ya tatu na ya mwisho kuhamishwa na misheni katika eneo la Kidal, ambalo limekumbwa na ghasia za wanajihadi na wanaotaka kujitenga.

    Kambi zingine mbili zilikuwa Tessalit na Aguelhok.

    Makundi yanayotaka kujitenga, ambayo hapo awali yalikubali kusitisha mapigano na mamlaka, yameanza tena uhasama katika eneo hilo.Wanapinga walinda amani kukabidhi kambi zao kwa jeshi la Mali.

    Serikali ya kijeshi ya Mali imekitaka kikosi cha Umoja wa Mataifa kuondoka nchini humo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, ikisema kuwa utume wake wa muongo mmoja dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu umeshindwa.

    Unaweza pia kusoma

  17. Habari za hivi punde, Israel yataja wanajeshi 11 zaidi waliouawa siku ya Jumanne

    th

    Jeshi la Israel limetoa orodha yake ya wanajeshi ambao wamefariki katika vita vinavyoendelea na Hamas.

    Idadi hiyo ya vifo sasa imefikia 326, wakiwemo wanajeshi 11 waliofariki huko Gaza siku ya Jumanne.Wanajeshi hao wote walikuwa na umri wa kati ya miaka 19 na 20.

    Picha za jeshi la Israel zinaonyesha majengo yaliyoharibiwa

    Jeshi la Ulinzi la Israel limetoa picha za hivi punde za operesheni yao ya kijeshi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

    Picha kadhaa zinaonyesha majengo yaliyoharibiwa na vifusi, ikionyesha ukubwa wa athari za mashambulizi ya anga na mashambulizi ya ardhini ya Israeli.

      TH
      TH

      Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

    • Tatizo la kipindupindu nchini Zimbabwe linachochewa na uhaba wa maji

      th

      Kwa miezi kadhaa sasa, Zimbabwe imekuwa ikipambana kukomesha kuenea kwa ugonjwa hatari wa kipindupindu katika miji na vijiji vyake kwa sababu nchi hiyo haina maji safi.

      "Maji yakitoka kabisa mara nyingi huwa machafu," Regai Chibanda, baba wa watoto watano mwenye umri wa miaka 46 kutoka kitongoji cha Chitungwiza, aliniambia.

      Kipindupindu, ni maambukizi makali ya kuhara yanayosababishwa na ulaji wa chakula au maji yaliyochafuliwa na bakteria Vibrio cholerae, unaweza kuenea haraka katika hali ya msongamano na chafu.

      Imekuwa aina zimwi baya kwa taifa hili la kusini mwa Afrika - mwaka 2008-2009 zaidi ya 4,000 waliaga dunia wakati ugonjwa huo ulipotokea katika kipindi ambacho tayari kilikuwa na msukosuko .

      Ilionyesha mzozo wa kisiasa na kiuchumi unaoendelea wakati mfumuko wa bei ulifikia asilimia 80 bilioni na kutangaza serikali ya kihistoria ya kugawana madaraka ambayo hatimaye ilikabiliana na hali hiyo.

      Leo mfumuko wa bei unazidi kuibua tena makali yake na ugonjwa wa kipindupindu umeenea katika majimbo yote 10 ya nchi, ambayo yanaathiri zaidi watoto, mara nyingi huachwa bila uangalizi katika joto huku wazazi wao wanapojaribu kufanya kazi.

      Mlipuko huu ulianza mnamo Februari na Oktoba ilipomalizika takwimu rasmi kutoka Idara ya Afya na Huduma ya Watoto zimeorodhesha karibu kesi 6,000 na vifo 123 vinavyoshukiwa.

      Rais Emmerson Mnangagwa, ambaye alishinda uchaguzi wenye utata mwezi Agosti kwa muhula wa pili madarakani, ameahidi mpango wa nchi nzima wa kuchimba visima.

      Hii itasaidiwa na vituo vya maji vinavyotumia nishati ya jua, hasa kuhudumia vijiji 35,000 ambavyo havina maji safi ya kunywa.

      Katika mji mkuu, Harare, wakaazi wanaweza kukaa kwa wiki, au hata miezi, bila usambazaji wa maji wa kawaida kutoka kwa Halmashauri ya Jiji la Harare.Katika kitongoji cha Harare cha Chitungwiza, zaidi ya vifo 50 viliripotiwa mwishoni mwa mwezi Oktoba - wote kutokana na kipindupindu.

    • Bolivia yakata uhusiano wa kidiplomasia na Israel kutokana na mashambulizi 'ya kiholela'

      th

      Bolivia ilisema inakata uhusiano wa kidiplomasia na Israel kutokana na mashambulizi "ya fujo na yasiyo na uwiano" dhidi ya Gaza.

      Naibu waziri wa mambo ya nje Freddy Mamani aliwaambia waandishi wa habari kwamba uamuzi wao ni "kukanusha na kulaani mashambulizi ya kijeshi ya Israel yenye fujo na yasiyo na uwiano yanayotekelezwa katika Ukanda wa Gaza".

      Kando, viongozi wa Colombia na Chile wamewaita mabalozi wao nchini Israel kwa maandamano.

      Katika chapisho kwenye X, iliyokuwa Twitter, rais wa Chile Gabriel Boric Fonts alisema nchi yake "inalaani vikali" Ukiukaji usiokubalika wa Israeli wa sheria za kimataifa za kibinadamu.

      Rais wa Colombia Gustavo Petro aliandika, pia kwenye X: "Ikiwa Israeli haitazuia mauaji ya watu wa Palestina hatuwezi kuwa huko."

      Biden na Mfalme Abdullah II wa Jordan wanajadili kupeleka misaada Gaza

      Katika saa chache zilizopita Ikulu ya Marekani imetoa maelezo ya simu kati ya rais wa Marekani Joe Biden na Mfalme Abdullah II wa Jordan.

      Viongozi hao wawili walijadili hatua za hivi punde huko Gaza na njia za kuharakisha uwasilishaji wa misaada katika Ukanda huo unaoshambuliwa na Israel na kukumbwa na matatizo mengi miongoni mwa masuala mengine kuhusu mzozo wa Israel na Palestina.

      Biden "alisisitiza umuhimu wa kulinda maisha ya raia na kuheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu, wakati Israeli inatetea raia wake na kupambana na ugaidi," ilisema taarifa hiyo.

      Rais pia "alikubali" kwamba Wapalestina hawapaswi "kuhamishwa kwa nguvu nje ya Gaza" na akatoa wito wa "amani ya kudumu na endelevu" ambayo itajumuisha kuundwa kwa taifa huru la Palestina.

      Zaidi ya nusu ya raia wa Jordan wana asili ya Palestina, akiwemo Malkia Rania ambaye katika wiki za hivi karibuni amekosoa vitendo vya Israel huko Gaza.

      Nchi hiyo ilitia saini mkataba wa amani na Israel mwaka 1994.

      Mawasiliano huko Gaza yasitishwa - kampuni ya Palestina

      Mtoa huduma mkubwa wa mawasiliano wa Gaza Paltel ametangaza "kukatizwa kabisa kwa mawasiliano na huduma zote za mtandao" katika eneo hilo.

      Hii ilitokana na ufikiaji wa kimataifa ambao "uliunganishwa hapo awali kukatwa tena," Paltel ilisema katika chapisho kwenye X., ambayo zamani ilijulikana kama Twitter.

      Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza

      • Watoto wadogo walichomwa vibaya kutokana na shambulio la anga la Jabalia - Muuguzi wa MSF

        th

        Shirika la matibabu la Médecins Sans Frontières (MSF) limeandika maelezo mafupi katika Twitter ya mmoja wa wauguzi wake wanaotoa huduma ya dharura katika hospitali ya Al Shifa katika Jiji la Gaza, ambaye aliwahudumia waathiriwa wa shambulio la anga katika kitongoji cha Jabalia.

        "Watoto wadogo walifika hospitalini wakiwa na majeraha makubwa na mabaya ya moto. Walikuja bila familia zao," alisema Mohammed Hawajreh.

        "Wengi walikuwa wakipiga kelele na kuwauliza wazazi wao, nilikaa nao hadi tukapata mahali kwani hospitali ilikuwa imejaa wagonjwa."

        MSF ilisema ilishtushwa na shambulio la anga la Jabalia na kulaani "kipindi cha hivi punde cha vurugu zisizo na maana", huku ikitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano."Imetosha!"

        'Ripoti za kuaminika' zasema kwamba kivuko cha Rafah kinaweza kufungua kwa watu wa Gaza waliojeruhiwa

        Tangu shambulio la Oktoba 7 la Hamas na jibu la kijeshi la Israel, mipaka ya Gaza imesalia kufungwa kwa kiasi kikubwa.

        Lakini vyanzo mbalimbali katika eneo hilo vimependekeza mpaka wa kusini wa Rafah huenda ukafunguliwa mapema leo ili kuruhusu baadhi ya Wapalestina waliojeruhiwa vibaya kupata matibabu upande wa Misri.

        Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilisema iliwafahamisha raia wa Uingereza waliokwama huko Gaza kuhusu kile ilichokiita ripoti za kuaminika kwamba Rafah huenda ikafunguliwa kwa ajili ya kuondoka kwa muda mfupi.

        Lakini ilisema hakuna maelezo kuhusu jinsi ufunguzi huo ungesimamiwa na nani ataruhusiwa kuondoka.

        Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller alisema "hatua nzuri i" imefanywa katika mazungumzo ya kuruhusu raia wa kigeni kuondoka.

        Misri imekuwa ikisita kufungua mpaka, ikihofia ongezeko lisilodhibitiwa la wakimbizi.

        Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza