Netanyahu azuru Gaza na kutangaza 'hakuna kitakachotuzuia'
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amekuwa akizuru ukanda wa Gaza, ambapo alizungumza na wanajeshi na kutembelea moja ya mahandaki ambayo yamefichuliwa .
Netanyahu alisema: "Tuko hapa Gaza na wapiganaji wetu mashujaa. Tunafanya kila juhudi kuwarudisha waliotekwa nyara, na hatimaye tutawarudisha wote.
"Tuna malengo matatu kwa vita hivi: kuwaondoa Hamas, kuwarudisha watu wote waliotekwa nyara na kuhakikisha kwamba Gaza haiwi tishio kwa taifa la Israel tena."
Aliendelea: "Niko hapa kuwaambia marafiki zangu hapa, kwa wapiganaji wa hapa, ambao wananiambia mambo yale yale, na ninarudia hii kwenu, wananchi wa Israeli: tunaendelea hadi mwisho - hadi ushindi.
"Hakuna kitakachotuzuia, na tuna hakika kwamba tuna nguvu,nia na dhamira ya kufikia malengo yote ya vita, na tutaweza."
Unaweza pia kusoma









