'Jaribio la kuvunja rekodi ya Dunia ya Guinness lageuza mikono ya mwanamke kuwa meupe'

Chanzo cha picha, Subair Enitan
Mwanafunzi wa Nigeria ambaye alikuwa amedhamiria kuweka rekodi mpya ya kuosha nguo kwa kutumia miko yake amerekodiwa akiwa na sura tofauti sana baadaye.
Katika video inayosambaa mtandaoni, Subair Enitan anaonekana akipumzika kwenye kitanda kufuatia kile anachosema kuwa ni mud awa saa 58 kwenye beseni la kuosha nguo siku ya Jumatatu, akiwaonyesha marafiki mikono yake iliyokunjana na myeupe.
Kundi la rekodi za dunia la Guinness bado halijatoa maoni yoyote kuhusu ombi la Bi Enitan, lakini aliambia vyombo vya habari siku ya Jumatatu:
Ujumbe wa Nukuu: Nimeridhishwa sana kukamilisha kazi hiyo mbele ya mama yangu, marafiki na wafanyakazi wenzangu ambao walijaa kwenye ukumbi huu kuonyesha upendo na kuunga mkono azma yangu."
Nimeridhika sana kuwa nimemaliza kazi hiyo mbele ya mama yangu, marafiki na wafanyakazi wenzangu waliojaa kwenye ukumbi huu kuonyesha upendo na kuunga mkono azma yangu."
Harakati za kuvunja rekodi ya dunia ya Guiness imeikumba Nigeria katika miezi ya hivi karibuni.
Mpishi mashuhuri Hilda Baci alianzisha mtindo huo alipopika mfululizo kwa zaidi ya saa 93, lakini miezi mitano baadaye alishindwa na mpishi wa Ireland Alan Fisher ambaye alisimamia zaidi ya saa 119.
Hivi majuzi, mwanamke wa Nigeria anayeitwa Helen Williams aliweka rekodi mpya ya kutengeneza wigi refu zaidi lililotengenezwa kwa mikono - lenye urefu wa 351.28m (1,152ft 5in).














