Hali ikoje kwa Waislamu wanaofunga mara ya kwanza?

Iliyochapishwa

Waislamu duniani kote wameanza mfungo wa Ramadhani. Wengi wa Waislamu wapatao bilioni moja nukta mbili duniani watakuwa wakifunga. Kutokana na sababu za kijiografia, nchi hutofautiana muda wa kufunga kutokana na tofauti ya kuchomoza na kuzama kwa jua.

Hapa Uingereza, Waislamu hufunga hadi saa 18.

Lakini je kwa wale ambao ndio kwanza wamesilimu na huu ndio mfungo wao wa kwanza, hali ikoje?

Mtangazaji wa BBC Salim Kikeke alikutana na baadhi yao na kuandaa taarifa hii.