Mdahalo Uingereza wafana
Watu maarufu wanaongoza katika kampeni za kutaka na wasiotaka Uingereza ijiondoe katika umoja wa Ulaya wamepambana vikali katika mdahalo wa televisheni ikiwa ni siku moja kabla ya kura ya maoni kupigwa hapo kesho.
Masuala ya uchumi na uhamiaji yamejitokeza zaidi katika madahalo huo uliohudhuriwa na washiriki zaidi ya elfu sita.
Meya wa zamani wa London Boris Johnson anayetaka Uingereza ijiondoe katika Umoja wa Ulaya ametetea uamuzi wake wa kutaka Uingereza ijiondoe katika Umoja huo.
Naye meya wa sasa wa London Sadiq Khan kutoka chama cha Labour yeye anapinga Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.
Hadi sasa utafiti unaonyesha mchuano utakuwa mkali katika kura ya maoni itakayopigwa hapo kesho kwa wale wanataka na wasiotaka Uingereza ijiondoe katika Muungano wa Umoja wa Ulaya.
Na kuchambua zaidi kuhusu kura hiyo ya maoni hapo Kesho Regina Mziwanda amezungumza na mchambuzi wa masuala ya Ulaya Ahamed Rajabu kutoka London na kumuuliza mdahalo huo wa televisheni umebadilisha chochote kwenye misimamo ya wanaotaka Uingereza ijiondoe na wale wasiotaka ijiondoe?