Droo: Manchester United wapewa Reading, Arsenal Preston Kombe la FA

Chanzo cha picha, Rex Features
Iliyochapishwa
Manchester United watakutana na Reading katika hatua ya klabu 32 bora michuano ya Kombe la FA baada ya droo kufanywa Jumatatu.
Mkufunzi wa Reading ni beki wa zamani wa Manchester United Jaap Stam.
Chelsea nao watakutana na mshindi kati ya Petersborough na Notts County.
Michuano hiyo ya raundi ya tatu itachezwa kati ya 6 na 9 Januari, 2017.
West Ham watakuwa wenyeji wa Manchester City kwenye mechi itakayokutanisha klabu za Ligi za Premia, huku wenzao Everton wakiwa wenyeji wa Leicester City.



























